Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,378
- 39,319
Muda mfupi ujao nitazungumza na mmoja wa wabunge ambao majimbo yao yameathiriwa vibaya na mvua kubwa ambazo zimesababisha mafuriko makubwa. Mafuriko haya licha kuleta madhara kwa makazi ya watu lakini kwa kiasi kikubwa yamefuta mazao na shughuli zote za kilimo katika majimbo hayo kiasi kwamba mwaka huu wawezekana kabisa ukawa wa njaa ambayo chanzo chake siyo ukame bali mvua nyingi...
Wakati tunapigia kelele ufisadi katika ofisi na taasisi mbalimbali, kwa wenzetu walioko katika majimbo haya wanachojali sasa hivi ni mablanketi, vyandarua, mahali pa kulala, na chakula. Pindi nikikamilisha mahojiano hayo yatarushwa baadaye ili sisi kama Watanzania tuwe tayari kutoa msaada unaowezekana.
Sasa hivi baadhi ya wabunge hao wameanza kuomba misaada toka kwa wafadhili na watu wa nje (wazungu) ili watuonee huruma. Je sisi Watanzania tulioko nje tunaweza kujitokeza kusaidia wananchi wenzetu waliopatwa na mafuriko? Au ni rahisi kulaumu kuhusu ufisadi lakini ukifika wakati wa kuhesabiwa tunafyata na kugwaya kana kwamba siyo sisi tunaozungumza?
Wakati wa maneno umepita (ndivyo nilivyosema mwishoni mwa mwaka jana); mambo ya kulaumu tu hayatoshi; mambo ya kujifanya tuna haki zaidi kuliko walioko nyumbani nayo haitoshi; wakati wa kujifanya tunajua siasa zaidi na Katiba zaidi, na sheria zaidi nao umepitwa; kwa mtu mwenye njaa na asiye na mahali pa kulaza kichwa chake la muhimu siyo EPA, RADA, TAnesco n.k kwake ni nani rafiki yake wa kweli wakati wa dhiki!
Je wana JF mtasimama mkiitwa na mmojawapo wa wabunge hawa kutoa msaada siyo wa "hali" bali wa "mali"! Misaada ya "hali" ni kama picha ya samaki ukutani kwa mtu mwenye shida.
Ndugu zangu kinachoendelea sasa hivi ni Katrina yetu kwenye majimbo hayo.
Natoa changamoto!!...