News Alert: Spika amwomba radhi Makinda

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Mapema leo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Samuel Sitta amemuomba radhi Naibu wake kwa kutumia neno "kukurupuka" alipomtaka asiongoze mjadala muhimu wakati alipotaka kwenda Marekani.
 
rrooo. iri rinawaigi kweri ni miapari ya kudakiaga. siri tvt rimeretaga iro riapari raripunge. rroo.
 
Alikurupuka kusema Naibu wake asikurupuke... na yeye inabidi akurupushwe... teh.
 
huo ndio uungwana ukikosea au kuteleza kukubali na kujirekebisha.


haya ni magumu kuyaona kwa wapinzani wao daima ni wasafi na wenzao ni wakosefu.
 
JF tukisema, tunaonekana wote ni wapinzani, ni wazi Sitta alikurupuka na huo ndio uungwana. Siku zote nasema nafasi ya spika wa Bunge Stta haimfai kwani hajakomaa kisiasa na nafasi hiyo inahitaji mtu mwenye busara na taaluma ya sheria, Public administration na zingine za uongozi
 
rrooo. iri rinawaigi kweri ni miapari ya kudakiaga. siri tvt rimeretaga iro riapari raripunge. rroo.

what language is this? huu sio uwanja wa ZE COMEDY! people are in serious talk here! na wewe kuwa serious kidogo! andika kitu kinacho eleweka
 
Nimesikia baadaye leo ndio lile sakata la Richmond linaanza bungeni,Mzee Mwnakijiji na wengine wenye taaluma ya mambo ya IT mtusaidie kutuunganisha ili tuweze kupata matangazo live tukiwa ofisini kwani nahisi tuta miss sana kuona hili songombingo.
 
Nimesikia baadaye leo ndio lile sakata la Richmond linaanza bungeni,Mzee Mwnakijiji na wengine wenye taaluma ya mambo ya IT mtusaidie kutuunganisha ili tuweze kupata matangazo live tukiwa ofisini kwani nahisi tuta miss sana kuona hili songombingo.

Report tayari inasomwa bungeni na Dr. Mwakyembe

Rostam yumo kwenye kashfa
Yona
Msabaha
 
Mh. Zitto aliadhibiwa kwa kusema waziri muongo. Sasa kwa nini SIX asiadhibiwe kwa kusema Naibu wake amekurupuka??? Muongo = Kakurupuka. Au kwa kuwa ameshika mpini......
 
Mtanzania, sijui nisiende hii safari? I just feel like waiting to see the end.
I gotta go... lets wait and see.
 
Mtanzania, anzisha thread mpya kwa ajili yanayotokea bungeni sasa hivi kuhusu ripoti ya Mwakyembe. Maana kwa sasa hizi topic zimeingiliana sana tutashindwa kufatilia. Naomba kutoa hoja.
 
Nasikia kivumbi kimeanza wanao angalia live tunaomb mtu-update nini kinaendelea.
 
Jamani hivi hakuna radio inayotangaza wengine tuko maofisini hatuoni live angalau hata tungesikiliza radio
 
Mkurupukaji akikurupuka anadhani wote ni wakurupukaji. anakurupuka kuongea akidhani na wenzie hukurupuka. suppose akiondoka leo bungeni kwa namna yoyote Anna atashindwa kuliendesha Bunge? Au Bunge litasimama hadi Bwana Yesu arudi kumfufua huyu ndugu six.
 
what language is this? huu sio uwanja wa ZE COMEDY! people are in serious talk here! na wewe kuwa serious kidogo! andika kitu kinacho eleweka

Ndiyo matatizo ya kuruhusu watu wenye majina ya ajabu. Pamoja na kuwa tunatumia majina ya kujibandika katika ukumbi huu, lakini sioni sababu yoyote ya mtu kujiita mabangi. Mara nyingi tusitegemee mchango wowote wa muhimu katika kupambana na mafisadi toka kwa mwanachama kama huyu.
 
Mkiangalia tarehe hii ilikuwa ni siku chache (masaa as a matter of fact) kabla ya kukaangwa kwa kina Lowassa... just to refresh your memories.
 
Tueleweshe.
Je Makinda alitaka kuwaokoa Marichmond? Kukurupuka kulihusu nini hasa?
 
Back
Top Bottom