News Alert: Sheria ya Ndoa kupingwa Mahakamani

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Wanaharakati wa haki za binadamu nchini Tanzania, wameamua kufungua kesi mahakamani ambapo wanataka kifungu cha 13 cha sheria ya ndoa ya 1971 ambacho kinaruhusu binti wa miaka 14 kuolewa kuwa ni kinyume na Katiba na mikataba ya Kimataifa ambayo Tanzania imeridhia. Kesi hiyo ambayo mshitakiwa mkuu ni Mwanasheria Mkuu wa serikali inalengo la kutaka mahakama "itangaze" kuwa umri wa vijana kuoa/kuolewa ni kuanzia miaka 18. Unaweza kuisoma sheria hiyo ya ndoa hapa chini au kwa kubonyeza SHERIA YA NDOA YA 1971

Sehemu ya kifungu hicho inasema:

13.-(1) No person shall marry who, being male, has not attained Minimum age the apparent age of eighteen years or, being female, has not attained
the apparent age of fifteen years.
(2) Notwithstanding the provisions of subsection (1), the court shall,
in its discretion, have power, on application, to give leave for a
marriage where the parties are, or either of them is, below the ages
prescribed in subsection (1) if-
(a) each party has attained the age of fourteen years; and
 
Wanaharakati wa haki za binadamu nchini Tanzania, wameamua kufungua kesi mahakamani ambapo wanataka kifungu cha 13 cha sheria ya ndoa ya 1971 ambacho kinaruhusu binti wa miaka 14 kuolewa kuwa ni kinyume na Katiba na mikataba ya Kimataifa ambayo Tanzania imeridhia. Kesi hiyo ambayo mshitakiwa mkuu ni Mwanasheria Mkuu wa serikali inalengo la kutaka mahakama "itangaze" kuwa umri wa vijana kuoa/kuolewa ni kuanzia miaka 18. Unaweza kuisoma sheria hiyo ya ndoa hapa chini au kwa kubonyeza SHERIA YA NDOA YA 1971

Sehemu ya kifungu hicho inasema:

Hata wakishinda, utekelezaji wake huko vijijini utakuwaje?

Wakati mwingine kama huwezi kuisimamia sheria ni bora kuiacha kama ilivyo.

Sikujua TZ unaweza kuoa mtoto wa miaka 15.
 
Now you know, nakumbuka wakati wakubwa zangu wa miaka 25 kwenda juu walivyokuwa wanavisarandia vitoto vya darasa la saba... kumbe ilikuwa halali..
 
Hapo ina nichanganya kidogo,
Kwani najua kuna sheria Tz inayo sema ukingonoana na binti/kijana (hasa hasa binti) mwenye umri chini ya miaka 18 hata kama karidhia kosa ni kwamba ume mbaka na ni kifungo jela miaka 30!

Mbona hapa sasa naona mkinzano mkubwa?
 
i hope wataweka sheria ya muda wa kuanza kuzini pia. kwani kinachompelekea mtu kuowa ndio hicho kinachopatikana kwenye kuzini. wakizuia ndoa pia tunataka watuoneshe vipi watazuia uzinifu? au ndio maendeleo ya development tena? kuwa na bf na gf ni ustaarabu?. langu jicho.why cant we be free to let everyone do what she or he like? especially katika mambo yanayowakilisha matamani ya kimaumbile?. akina under age ina maana ndio wauchune mpaka miaka 18? maana wengine kuzini kwao ni haramu.si muda mrefu! ila what if.........
 
ukingonoana na binti wa umri huo ni kosa, ukiamua kumchukua jumla jumla si kosa...

Huo ni mkoragano kabisa! mi nilidhani hapo mantiki ni kwamba huyo binti anakuwa bado mdogo kwa ajili ya hayo mambo, kumbe ukichukua jumla inabadili umri jama?

Nadhani hii si sahihi, kuna shida kubwa mahali!
 
tukiwaambia hawa watawala wetu kuwa sheria zetu ni za ajabu wanasema "hatuwapongezi kwa kazi nzuri".
 
ukingonoana na binti wa umri huo ni kosa, ukiamua kumchukua jumla jumla si kosa...

3yf08w0.gif
 
Hata wakishinda, utekelezaji wake huko vijijini utakuwaje?

Wakati mwingine kama huwezi kuisimamia sheria ni bora kuiacha kama ilivyo.

Sikujua TZ unaweza kuoa mtoto wa miaka 15.

Taratibu ndio mwendo...tunapiga hatua ado ado. Kwanza sheria ibadilishwe then hizo kesi za vijijini zitashughulikiwa zinazowezekana hivyo hivyo.
 
Back
Top Bottom