News Alert: Serikali yatoa orodha ya Mikoa inayoongoza kwa matumizi ya bangi

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
2,000
NOVEMBA 6 , 2019

Serikali imesema matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi bado ni tatizo nchini, huku yakishika kasi katika mikoa ya Mara, Tanga, Morogoro, Arusha, Kagera na Ruvuma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, akitoa taarifa ya hali ya dawa za kulevya kwa mwaka jana, alisema katika kipindi hicho vyombo vya dola kwa kushirikiana na wananchi walikamata tani 24.3 za bangi na watuhumiwa 10,061.

“Dawa za kulevya aina ya mirungi nayo imeendelea kutumiwa na watu wa rika mbalimbali hapa nchini, kwamba kwa mwaka 2018 vyombo vya dola vilifanikiwa kukamata tani 8.97 za mirungi zikiwahusisha watuhumiwa 1,186,” alisema.

Alisema katika kipindi cha mwaka jana, kesi 7,592 zikiwa na watuhumiwa 10,979 zilifunguliwa katika mahakama mbalimbali nchini, huku kesi 7,174 zilizowahusisha watuhumiwa 11,045 ziliendelea kusikilizwa.
 

Sandiego

JF-Expert Member
Dec 18, 2018
755
1,000
Ndio maana hio mikoa wagombea wa serikali za mitaa na vijiji wamekatwa sana!!
 

Msingida

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
7,949
2,000
WHO wameondoa bange kwenye kundi la madawa ya kulevya.
Hiyo ni mmea kama mimea mingine ya dawa za kutibu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom