News Alert: Pingamizi la Serikali latupwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

News Alert: Pingamizi la Serikali latupwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 23, 2007.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 23, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Serikali yakwama mahakama kuu uchaguzi wa madiwani
  Na Nora Damian

  MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali ombi la serikali la kuomba mahakama hiyo isisikilize ombi lililowasilishwa na vyama vinne vya upinzani nchini vinavyotaka kuzuia kufanyika kwa uchaguzi wa madiwani katika kata 16, uliopangwa kufanyika Jumapili ijayo.


  Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Njengafibili Mwaikugile wa mahakama hiyo na aliongeza kuwa mahakama hiyo leo itasikiliza maombi yaliyowasilishwa na vyama vinne vya upinzani ili kuamua uchaguzi huo usitishwe au la.


  �Hoja zilizowasilishwa na serikali kupinga mahakama isisikilize maombi ya upinzani kwamba isimamishe uchaguzi, hayakupaswa kuletwa sasa kwa sababu hoja zinazungumzia maombi yenyewe, walipaswa kuleta wakati wa kusikiliza maombi yenyewe,� alisema Jaji Mwaikugile.


  Jaji Mwaikugile pia alipinga madai yaliyowasilishwa na serikali kwamba maombi ya wapinzani yameletwa chini ya kifungu ambacho sio sahihi na kusema kwamba kifungu hicho ni sahihi.


  �Kifungu hicho cha nne cha Sheria ya Haki za Msingi na Wajibu wa watu ni sahihi kwa kuwa mtu akiona haki zake za kikatiba zinavunjwa hakuna, kifungu kingine kinachoweza kutumika zaidi ya hiki,� alisema.


  Juzi Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliwasilisha pingamizi katika mahakama hiyo akitaka kutupiliwa mbali kwa ombi la vyama vinne vya upinzani vinavyotaka kuzuia kufanyika kwa uchaguzi wa madiwani katika kata 16, uliopangwa kufanyika Jumapili ijayo.


  Wakiwasilisha hoja zao kwa zamu, mawakili watatu wa serikali, Joseph Ndunguru, Paul Ngwembe na Abraham Senguji walidai kuwa maombi ya upinzani yamepitwa na wakati na kwamba yanapingana na ibara ya 74 (6) (d) ya katiba ya nchi.


  Katika ombi lao la msingi, vyama vya Chadema, TLP, NCCR-Mageuzi na CUF pia vinaitaka mahakama kuizuia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuendesha Uchaguzi wa Madiwani.
   
 2. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2007
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  naam tusubiri kifyatacho, mara nyingi hapa wengi hushahingiria baadae matokeo ya mahakama huwa chungu na yasiofaa.

  tuvute subira tuangalie nini kitakuwa baada ya kusikiliza shauri
   
 3. K

  Katibu Tarafa JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2007
  Joined: Feb 16, 2007
  Messages: 980
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  wanauma na kupuliza utafikiri panya
   
 4. K

  Koba JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2007
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  hey Mwanakijiji, do you sell Viagra stuff? lol I went and looked at your webpage and saw that , It cracked me up. The page is really nice, good job on it!
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Oct 24, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  sometimes... na uzee huu ndio maana wengine tunazidiwa kete kirahisi rahisi..
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Oct 25, 2007
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  ahahahahahahahahahaaaa......haya bwana
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Oct 26, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kesi ya wapinzani kuhusu uchaguzi yapigwa mweleka mahakamani
  Na Nora Damian (Mwananchi)


  MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali maombi ya vyama vinne vya upinzani kupinga uchaguzi mdogo wa madiwani unaotarajiwa kufanyika kesho.


  Badala yake, mahakama imesema uchaguzi uendelee kama kama ulivyokuwa umepangwa.


  Uamuzi huo ulitolewa jana baada ya mahakama hiyo kumaliza kusikiliza hoja za wakili wa upinzani, Mpare Mpoki na mawakili watatu wa serikali, Joseph Ndunguru, Paul Ngwembe na Abraham Senguji.


  Jaji Njengafibili Mwaikugile alisema mahakama imefikia uamuzi huo kwa sababu walalamikaji hawakupeleka ushahidi zaidi ya kuwasilisha idadi ya watu.


  “Hakuna ushahidi unaoonyesha kwamba kundi hilo la watu 50,000 lipo, kundi hilo ni la kufikirika tu, wapo lakini hawapo,” alisema Jaji Mwaikugile.


  Alisema kuna idadi nyingine ya wapigakura kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, wanaohitaji haki ya kupiga kura na mahakama ikisimamisha uchaguzi, itakuwa imewanyima haki yao ya msingi.


  Baada ya kutolewa uamuzi huo, Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema, alisema hawajaridhika na wataendelea kupigania haki zao za msingi.


  Naye Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Haki za Binadamu, Salum Bimani alisema wataendelea na madai yao ya kutaka Katiba ibadilishwe kwa sababu madai yao ni ya msingi hayajafanyiwa kazi.


  Awali, akiwasilisha hoja zake wakili Mpoki alisema, ombi la kutaka uchaguzi usimamishwe linatokana na kesi waliyofungua mahakamani hapo wakitaka watu 50,000 waandikishwe kabla ya kufanyika uchaguzi.


  Wakiwasilisha hoja zao kwa zamu, mawakili wa serikali walisema tume ndio iliyopewa uwezo wa kuandaa uchaguzi na kuandikisha wapiga kura, zoezi la kuandikisha ni refu linachukua siku 120 na linahitaji kupitia hatua mbalimbali.


  Katika ombi lao la msingi, vyama vya Chadema, TLP, NCCR-Mageuzi na CUF, vilikuwa vinataka mahakama kuzuia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuendelea na uchaguzi wa madiwani, utakaofanyika kesho.


  Kuhusu ombi la msingi, Jaji Mwaikugile alisema kesi ya msingi ya iliyowasilishwa na walalamikaji ni kwamba, watu waongezwe katika dafutari la kudumu la wapiga kura ambalo alisema litasikilizwa Februari 15, mwakani. Kesi hiyo ilifunguliwa Oktoba 5, mwaka huu
   
Loading...