News Alert: Pinda atangaza kuanza kukutana na waandishi!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,675
40,555
Well, kila baada ya miezi mitatu kuwapa maelezo juu ya maamuzi ya baraza la mawaziri. However vikao vya baraza la mawaziri vinafanyika kwa kawaida mara moja kwa wiki.
 
what difference does it makes? Huyu jamaa hana tofauti yoyote na viongozi wengine. Ni same kanzu different shekh. Haina tofauti na wanaCCM wengine.
 
suala si kukutana na waandishi wa habari ,suala ni kuja kuwaeleza watanzania mambo wasityoyajua ila serikali imeyafanya na siyo kuja kuongea mambo ambayo watanzania wanayajua.

tunahitaji kuona nchi ikienda mbele na siyo kuwa hapa tulipo,nimechoka kuona nchi inaendeshwa kisannii bila ya kuwa na vision,ni bora na Mkapa alikuwa akiforsee mambo kuhusu kukusanya Kodi na masuala ya MEM na mambo ya millenia.

Nimekuja kugundua ni kwanini serikali ya sasa imeshindwa kuwapa watanzania nini wanachotaka,na nadhani mhe. Rais hajui hili

1.Mabadiliko ya mara kwa mara ya Barza la Mawaziri ynaathiri utendaji Mzima wa watendaji kazi katika Wizara,naomba nikupe Mfano mmoja hapa,wakati Mhe. Msolla alipowekwa pale(hana uwezo) Wizara ya Elimu ya juu alipangua wakurugenzi wote na kuweka ambao yeye anwataka ili wamsaidie,hii inaweza kuwa sawa ila kuweka mtu mpya ni sawa na kurudisha jambo nyuma sababu itambidi mtumishi huyu ajifunze kwanza kazi ile kabla ya kuendelea mbele,wakabawa wizara sama thing happen.Na hili suala lisipochukuliwa hatu basi nchi haitaendelea,suala la uongozi serikalini limekuwa la kisiasa,akija waziri basi naye anapanga watu wake??hili suala ndilo linamuangusha JK kama hajui.

2.Tabia ya Mawaziri kuingilia utendaji kazi katika wizara,kama kutafuta makandarasi,kuweka watu wao ili wafanye kazi flani na yenyewe inachangia kuwavunja moyo watumishi wa umma,Mfano,Mama sitta alivyokuwa pale wizara ya Elimu alimpa kazi Mtoto wake ya Uconsultant wa IT ili wanafunzi waweze kupata matokeo kwa njia ya SMS,huku tayari wataalm wa pale walikuwa na Njia Mbadala ya kulifanyia kazi suala hili.

nimemamliza
 
Wakati huo huo serikali imeteua wasemaji wa wizara ambao ndio watakuwa wanatoa taarifa kwa waandishi kuhusu mambo yanayohusu wizara hizo. Salva amesema jana kuwa wameteuliwa wasemaji 22 na ni wizara ya Mambo ya Nje tu ambayo msemaji wake hajateuliwa bado; Maura Mwingira?????
 
Wakati huo huo serikali imeteua wasemaji wa wizara ambao ndio watakuwa wanatoa taarifa kwa waandishi kuhusu mambo yanayohusu wizara hizo. Salva amesema jana kuwa wameteuliwa wasemaji 22 na ni wizara ya Mambo ya Nje tu ambayo msemaji wake hajateuliwa bado; Maura Mwingira?????

Mwanakijiji,Suala sio wasemaji?Je watasema ukweli kuhusu mambo yanayohusu Mstakabali wa taifa,siyo aulizwe swali ajibu,hilo muulizeni waziri.

Mie nakwambia Kimbele mbele cha Salva kitamponza tu,Hivi Salva na Waziri nani Mkubwa,Manaake amekuwa akitoa kauli nzito,hasa majuzi alipoongelea suala la Balali.Aliniogopesha

Kuhusu kuteuliwa ,hawajateuliwa wameongezewa kazi tu..sababu hao wote walikuwa kama Principal Information Officer wa wizara,sasa badala ya kuzunguka na safari za mawziri huku na kule sasa watakuwa wanakujibu live,hivi yule aliyekujibu Ndege inapaa yuko wapi kwa sasa??kanyamaza
 
Pamoja na ufinyu wa kufahamu waziri mkuu, wizara na idara za serikali zinafanyaje kazi, lakini naona ugumu kuelewa umuhimu wa waziri mkuu kukutana na waandishi wa habari na hasa pale atakapokuwa anatoa majibu yasiyoridhisha. Wakati huo huo nashindwa kuelewa hawa wasemaji walioteuliwa shughuli yao itakuwa nini.
1. Je, ni kusema waziri katika wizara hiyo hawezi kufanya hiyo kazi?
2. Je, naibu waziri hawezi kufanya hiyo kazi?
3. Je, katibu mkuu shughuli yake ni nini?
4. Ina maana wizarani hakuna maofisa mahusiano (Public Relation Office/Officers)?
5. Je hawa walioteuliwa ni waajiriwa katika wizara husika au wameteuliwa watu kutoka seheme/wizara zingine kwenda kufanya hiyo shughuli?
6. Huo uteuzi ni cheo au majukumu tu? Kama ni cheo ni watanzania bado tubebe gharama hizo baada ya mawaziri, manaibu mawaziri karibu 60?
7. Ni taarifa gani watakuwa wanatoa ambazo huko nyuma kutokuwepo kwao kulifanya zishindikane kutolewa?
Naomba mwanga zaidi kama kuna anayefahamu.
 
Back
Top Bottom