News Alert: "Nitambueni kama Rais, tutazungumza"

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Hatimaye Rais Mugabe naye anatumia sharti linalotumiwa na Karume kuwa hadi umtambue kama Rais ndiyo wataweza kukaa chini kuzungumza. Baada ya kuwasili kutoka Misri, Mugabe anasema yuko tayari kuzungumza lakini hadi wamtambue kwanza kama Rais.
 
Kesho utasikia anataka wananchi waulizwe kama wataikubali serikali ya mseto kwa kutumia kura ya maoni. Sijui Mh.Pinda pinda asimwambie mambo hayalingani.
 
Hatimaye Rais Mugabe naye anatumia sharti linalotumiwa na Karume kuwa hadi umtambue kama Rais ndiyo wataweza kukaa chini kuzungumza. Baada ya kuwasili kutoka Misri, Mugabe anasema yuko tayari kuzungumza lakini hadi wamtambue kwanza kama Rais.

Mzee naona umesahau kuweka source ya hiki kipande cha habari......si unajua tena kina nanihino lazima watakuomba source....Lol

On a serious note, it appears that these African leaders use the same playbook to stay in power.....It's weird how similar things are from country to country....e.g. haste inaugurations without even inviting regional dignitaries....remember Salmin Amour...Mwai Kibaki.....now Mugabe...the similarity here is that all this takes place after a contoversial vote....
 
Ujinga uliofanyika Kenya, umeanza kuitafuna Afrika. Kama Kibaki angeshughulikiwa ipasavyo mugabe asingekuwa na jeuri hii ya kusema ujinga huu. Sasa leo Mugabe atasema hivi, kesho Museveni atafanya hivyo hivyo na baadaye utaendelea kuwa mchezo huu huu. This is African solution to African problems!
 
Hatimaye Rais Mugabe naye anatumia sharti linalotumiwa na Karume kuwa hadi umtambue kama Rais ndiyo wataweza kukaa chini kuzungumza. Baada ya kuwasili kutoka Misri, Mugabe anasema yuko tayari kuzungumza lakini hadi wamtambue kwanza kama Rais.

Ni vyema Tsvangrai akatekeleza hilo ombi la mzee Mugabe haraka ili mzozo wao uishe na tuachane na zimbabwe turudi tz kushughulikia MATATIZO YETU , hasa swala la CUF na CCM zanzibar.
 
Hatari ya wafrika kuwanyenyekea marais wetu bila kuwepo mtu wa kuwakosoa, na wanafikia kujiamini kuwa wao tu wenye akili kiliko watu wote ktk nchi zao, inafikia mahali raisi anaugua ogonjwa wa akili kama Mugabe, na kwa unafiki wa watu waliomzunguka, wanaendelea kukubali awaongoze si kwa manufaa ya nchi bali yao binafsi. Mugabe ni ngonjwa wa akili
 
I believe the resolute of Zimbabwean people, Mugabe and his henchmen will be defeated by any means whatever the case. They live in borrowed time and they know it.
 
Ujinga uliofanyika Kenya, umeanza kuitafuna Afrika. Kama Kibaki angeshughulikiwa ipasavyo mugabe asingekuwa na jeuri hii ya kusema ujinga huu. Sasa leo Mugabe atasema hivi, kesho Museveni atafanya hivyo hivyo na baadaye utaendelea kuwa mchezo huu huu. This is African solution to African problems!
kama kuna kitu kinaudhi, ni hawa madikteta wanaoshindwa uchaguzi halafu, wanaganda kwenye madaraka , na wale walioshinda wanakuw amawaziri mkuu eti kwa litania ya serikali za mseto.
 
Hatimaye Rais Mugabe naye anatumia sharti linalotumiwa na Karume kuwa hadi umtambue kama Rais ndiyo wataweza kukaa chini kuzungumza. Baada ya kuwasili kutoka Misri, Mugabe anasema yuko tayari kuzungumza lakini hadi wamtambue kwanza kama Rais.

Nashukuru Mwanakijiji kwa kuona hilo, kuwa kinachofanyika Zimbabwe hakina tofauti ya msingi na kinachofanyika katika nchi nyingi za Bara letu, Tanzania ikiwemo. Pengine bado hatujachelewa kujiuliza sasa kwanini Mugabe tu ndio anasikika?
 
Baba mmoja, Mama mmoja, yeye anafuata nyayo tu au kwa maana nyingine katupa dongo kwa muungwana lakini safari hii dongo lake limepoa na ana sababu nzuri tu za kupoza makali yake.
 
...Naona mzee Robby anawawekea mitego washkaji na hapo ndipo watakapopoteza muelekeo...

Mkimtambua kama raisi then mkaongea na akikataa hiyo serikali ya mseto??? Mnakuwa hamumtambui tena??? Mugabe kawatia kabali ya tumbo hapo wasipokuwa makini wataishia kuhara tu...
 
Mzee kawaweza. Mugabe iko akili!
 
Back
Top Bottom