News Alert: Mtanzania wa Gitmo (Fupi) kushtakiwa NY | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

News Alert: Mtanzania wa Gitmo (Fupi) kushtakiwa NY

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 21, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 21, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mtuhumiwa wa Ughaidi Ahmed Ghailani ambaye amekuwa akishikiliwa huko Guentanamo atakuwa ni mtuhumiwa wa kwanza kutoka gereza hilo kushtakiwa katika mahakama ya Kiraia huko New York. Uamuzi huo unakuja siku chache tu kabla Rais Kikwete hajakutana na Rais Obama mjini Washington DC.

  Ghailani alikamatwa huko Pakistani miaka michache iliyopitwa akidaiwa kuhusika na ulipuaji wa Ubalozi wa US mjini Dar-es-Salaam na kujihusisha na mtandao wa ughaidi wa Al-Qaida.

  Kushtakiwa kwa Ghailani kwenye mahakama ya kiraia kunaweka uwezekano wa hatimaye kuweza kuhamishiwa Tanzania ambako pia anatakiwa.
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  May 21, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Safi sana. Funga maisha huyo ghaidi
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  May 21, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nyani Ngabu,
  Wangejua tu kwamba ni mbeba unga nadhani hata wasingefika huko!..
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  May 21, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  unajua jamaa alikuwa set up big time.. sidhani kama ni ghaidi wa kupewa attention hiiyo yote.. ni yale yale ya kutaka kuchangamkia tenda ya haraka haraka kumbe vingine vimeshavunda..
   
 5. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  New York ni venue tu, atakuwa wa kwanza kushitakiwa katika mahakama ya kiraia Marekani nzima, period.
  Mkutano wa Obama na Kikwete unahusiana nini na huyu gaidi? Hiyo point ingehusika kama suspect angekuwa supported na Tanzania au amesababisha diplomatic tensions between them. Vinginevyo ni kitu kinaelea elea tu.

  Kivipi? Kwa nini? Unataka kusema angeshitakiwa jeshini ndio angekufa asirudi Tanzania au unataka kusema sasa watakuja kum hand over kwa TZ? What do you mean? How? Ha ahaaaaaaa Duuu, wana habari wetu mtu anaweza akajitungia tu kitu. Kama Michuzi aliyeandika Daily News kwamba Obama na Kikwete wanakutana katika kipindi ambacho Obama yuko under pressure ya Waafrika. Kivipi, hakusema, kajitungia sentensi ipo ipo tu.

  Hii story nzima ilishawekwa hapa na QM anyway.
   
 6. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Hakuna uhusiano wowote kati ya kupelekwa Mahakamani kwa Ahmed Ghailani na Mkutano wa Marais Kikwete na Obama hapo baadaye leo.

  Ahmed Khalfani Ghailani anapelekwa Mahakamani kwa sababu tu Utawala wa Obama unataka kuonyesha kuwa suala zima la Guantanamo linafanyiwa kazi...Siku nzima ya Jana kumekuwa kuna kutokuelewana kati ya Senate,Congress na Uongozi wa White House kuhusu kufungwa kwa Gereza Kuu la Guantanamo.

  Wamarekani wengi hawataki wafungwa waliopo Guantanamo waletwe ndani ya Marekani...inaonekana kwa walio wengi uamuzi wa kufunga Gereza la Guantanamo ulikuwa wa haraka na wa kutafuta umaarufu wa kisiasa kuliko ukweli mzima kuwa ni wapi watakwenda wafungwa hao....Italy na France kila moja imekubali kuchukua wafungwa wawili tu,inasemekana wafungwa wengi watapelekwa Florence,Colorado kwenye gereza lenye ulinzi mkali (supermax)

  Rais Obama Asubuhi hii pamoja na mambo mengine atatoa Hotuba kubwa kuhusu "ugaidi" na hatima ya Wafungwa wa Guantanamo,hotuba ambayo itajibiwa na Makamu wa Rais wa Zamani Dick Cheney ambaye anaona kufungwa Guantanamo ni makosa makubwa....

  Kuna Baadhi ya waaangaliaji wa karibu wa masuala ya siasa wanasema "kufungwa kwa Guantanamo" na "kusambazwa habari/picha za torture kutoka kwenye vyombo vya sheria" ni kosa kubwa lililofanywa na utawala wa Obama!
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  May 21, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Hizi ligi zingine mnalazimisha tu jamani. Ni wapi paliposemwa kuna uhusiano kati ya mkutano wa Kikwete na Obama na huyu ghaidi?
   
 8. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  They may have valid reasons to go down this road. Never underestimate human beings wakuu.
   
Loading...