News alert:Mgombea urais NCCR- Mageuzi Azomewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

News alert:Mgombea urais NCCR- Mageuzi Azomewa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TandaleOne, Oct 16, 2010.

 1. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,617
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Send to a friend Friday, 15 October 2010 07:40 0diggsdigg

  Patricia Kimelemeta, Kigoma
  MGOMBEA urais kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, Hashimu Rungwe jana alipata wakati mgumu baada ya wananchi wa kijiji cha Nguruka kilichopo nje kidogo wa Mji wa Kigoma kumwambia wazi kuwa hawamhitaji, bali wanamtaka David Kafulila kuwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini.

  Hatua hiyo imekuja baada ya mshereheshaji wa kampeni hiyo kumpa nafasi ya kuzungumza na wananchi kwenye kiwanja cha shule ya msingi Nguruka, mara baada ya Rungwe kuinuka, wananchi hao walianza kuondoka huku wakisema wao wamekuja kumsikiliza Kafulila na si mgombea mwingine wa chama chochote.

  "Haaa, huyu, hapana, hatuwezi kumpa, bora angekuwa Mbatia, lakini sio huyu, hapana," zilisikika sauti za wananchi hao huku mmoja aliyezungumza na waandishi wa habari na kujitambulisha kwa jina la Faraj(37) alisema kuwa, mgombea huyo hajawahi kufika kwenye vijiji hivyo, jambo ambalo limewafanya wananchi hao kuguna.

  "Hatuwezi kumpa kura zetu huyu, bora angekuwa James Mbatia lakini sio huyu, hatujawahi kumuona hata siku moja, kama ni hivyo bora tumpe mgombea mwingine wa urais lakini sio huyu, hatumjui ila za ubunge tutampa Kafulila," alisema Faraji.

  Kwa mujibu wa Faraji, walidhani anayewania nafasi hiyo ni mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia badala yake amekuja mtu mwingine asiyejua matatizo yao.

  Naye mwananchi mwingine wa kijiji hicho, Ramadhan Rajab (54), alisema kuwa nafasi ya urais inamtaka mtu ‘smati’ ambaye anaweza kuzungumza na wadau mbalimbali katika kutetea maslahi ya wananchi, hivyo basi kitendo cha kumpa Rungwe nafasi hiyo wakati anafuga ndevu kinaweza kuwafundisha tabia mbaya.

  "Huku kwetu usafi ni kitu muhimu, hatuwezi kuruhusu mtu kufuga ndevu ndefu kiasi hiki na anashindwa kuzitunza, huu ni uchafu, hatuwezi kumpa,"alifafanua.

  Hata hivyo, Rungwe alijaribu kuwasihi wananchi hao wamsikilize huku akisema kuwa, serikali iliyopo madarakani inapaswa kupumzishwa.

  "Naomba mnisikilize ndugu zangu, tulieni kwanza niwaambie kitu nataka tuwapumzishe hawa manyang'au, hawafai,"alisema Rungwe.

  Alisema, serikali ya awamu ya nne ya chama tawala kimeshindwa kusikiza kero za wananchi, badala yake wamekaa madarakani kwa ajili ya maslahi yao binafsi.

  Alisema, kutokana na hali hiyo wananchi wana haki ya kuwanyima kura kwenye kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

  Wakati huo huo Rungwe amepata wakati mgumu kufanya kampeni kwenye maeneo mengine ya Jimbo la Kigoma baada ya kukosa usafiri na kulazimika wakati fulani kutumia daladala.

  Rungwe ambaye alifika mkoani Kigoma Oktoba saba mwaka huu, baada ya kuachwa na ndege zaidi ya siku mbili, alikodi gari ndogo ya kubeba abiria aina ya teksi ambayo aliitumia maeneo ya mjini Kigoma huku akishindwa kwenda vijiji vilivyo nje ya mkoa.

  Tatizo hilo la usafiri kwa mgombea huyo lilingia katika hatua nyingine pale alipochukua gari la mgombea ubunge na kulazimisha gari hilo kulitumia kwenye mikutano yake na kuwatelekeza waandishi wa habari waliokuwa wakitumia gari hiyo kwenye msafara huo.
  Chanzo:Mwananchi
   
 2. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135

  Funny boy! haha!
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kheeee heeee heeee... Duniani kuna mambo!
   
 4. N

  Njaare JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2010
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  He! Hii kali. Kufuga ndevu ni tabia mbaya!!!!!??????

  Au Bado kuna watu wanatafuta akina baba warembo?
   
 5. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ingekuwa busara sana kama NCCR wangeamua kutosimamisha mgombea na badala yake wamuunge mkono Dk Slaa... Fundisho kwa mapandikizi wote...
   
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Na huyo slaa ndie nani?
   
Loading...