News Alert: Mengi awafungulia mashtaka waandishi!

Inavyoonyesha yanaandika ukweli, kama kuna mtu kakashifiwa angeenda kutafuta haki yake mahakamani, kama hawakwenda, wamepima uzito! Ndio maana yeye katangulia. Nadhani yupo tayari kwa hilo, why do u doubt him?
mm naogopa usije ukatwambia magazeti yake ni kama injili,na wahariri wake ni akina Mathayo, Luka na Yohana.
 
Hivi ni kwa nini kesi za ku publish udaku zinaenda high court of Tanzania halafu makesi ya mabilioni ya Mawaziri, makesi yanayohusu kuhujumu uchumi wetu sote, yanaenda kwa mahakimu wakazi ambao wanavurunda vurunda mara wanatoa bail based on expired documentation mara wanapandisha na kushusha recognizance amount ovyo ovyo mara wanamwachia mtu kesho yake wanamtafuta?

Hizi kesi za fulani kanikandia kwenye tabloid lake mi nadhani ndo zingeenda kule kwa mahakimu wa uchochoroni wasiojua wanachokifanya.

Kuhani wasalaam!

Naongana na wewe. Kuongezea hapo kwa nini isiundwe special tribunal kudeal na mafisadi kama kweli Uongozi wa JK Huko serious? Kwa sababu hapa tunaongelea kuhusu hizi kesi zinazotishia uhai wa uchumi wa Tanzania. Ikiundwa tribunal hili hizi kesi ziwezi kwenda haraka na hiyo tribunal hiwe katika rank moja na Mahakama kuu.

Shadow.
 
kuna biashara kubwa sana kuhusu mengi na Ra na wahindi wengine, wahindi hawa wanunua data za mengi kwa bei kubwa, sasa wanauziwa karasha badala ya data halafu wanazichapisha kwenye magazeti yao, megi naye ananunua data kuhusu mafisadi ila yeye amekuwa mwangalifu sana kwenye ununuzi na uchapishaji. kwa jinsi mengi anavyowaandama hawa mafisadi ni jinsi hiyo hiyo data za mengi kwa mafisadi zinavyopanda bei. dalali mkuu kwenye haya manunuzi ni MCHUNGAJI CHRISTOPHER MTIKILA!!!!!
 
Watu wengine bwana!! Yeye hajaenda mahakamani kushitaki owners wa hayo magazeti, amewafungulia mashitaka, waandishi na wahariri wake. Sasa kule mahakamani ndo watasema kama owners ndo waliowatuma waandike hizo kashfa au sehemu walipopata hizo habari.
Pili sijawahi msikia akisema kuwa magazeti yake yanaandika ukweli tupu, hasa kwa kuwa yeye sio mwandishi wala mhariri wa magazeti yake. Sasa kama kuna mtu anaona magazeti yake yameandika uongo au kashfa, wawafungulie mashitaka wahariri na waandishi wa magazeti yake.
 
Nilibahatika kumuona wakili Ngalo akisoma taarifa ya kesi hizo kwenye ITV. Taarifa inajulisha amelishwa maneno. Alikuwa akisoma huku anajiumama. Taarifa hiyo ilisomwa kwa dakika 8!.
Huu ni udhibitisho wa yale maneno ya Adam Malima. Sijawahi kuona taarifa ya Ikulu ikisomwa inside news kwa dakika 8!.
Pamoja na ukweli kuwa ITV ni ya Mengi, na ana uhuru wa kuitumia atakavyo, news inabaki kuwa news, kuna professionalism ndani yake. Hiyo taarifa kusomwa yote as if it was a live event, breaking news or development news was wrong proffessional.
Jinsi ilivyokuwa ndefu, nikamkumbuka marehemu John Mdolwa aliyekuwa mhariri mkuu ITV,
Angekuwepo, isingeachwa kama ilivyo hata kama Mengi angelazimisha, Mdolwa angesema "Its unprofessional".
Kuhusu kesi, Mzee Mengi anapenda sana kulianzisha ili kuuthibitishia umma, how clean he is, na akikuta somewhere somehow he is dirty, atazifuta baadhi ya kesi. Mfano hai ni ile kesi dhidi ya gazeti la Mtanzania baada ya kuandika habari kuwa licha ya Mengi kuwa ni Tajiri, lakini ana madeni kibao!. Mzee alifungua kesi, alipoonyeshwa document ya benki kuthibitisha, aliifuta kesi kimya kimya.
Ila pia kitu kizuri, kuna baadhi ya waandishi wanaomchambua sana lakini wanabaki salama na mahali penye usalama, si pengine zaidi ya humu jamvini.
Idumu JF.
 
Pamoja na ukweli kuwa ITV ni ya Mengi, na ana uhuru wa kuitumia atakavyo, news inabaki kuwa news, kuna professionalism ndani yake. Hiyo taarifa kusomwa yote as if it was a live event, breaking news or development news was wrong proffessional.
J.

Umeongea vizuri sana Pasco. Lakini hapo nilipopigia mstari ndiyo ambapo panakosewa na ndipo ambapo palimfanya Sitta amsaidie Mengi. Sitta alisema kuwa Mengi ana haki ya kufanya hivyo kwa sababu TV ni yake. Huo siyo ukweli na ni mkakati wa kuharibu ukweli. Maana TV ni mali ya Mengi lakini masafa ya kurushia ni ya nchi na ndiyo maana anapewa masharti kibao. Kwa mfano katika sheria ya vyombo vya habari (leseni ya kuendesha chombo cha habari) mpaka sasa hivi ni lugha mbili tu zinaruhusiwa Kiingereza na Kiswahili. Mengi akitangaza kichaga sheria inamkamata hata kama TV ni yake. Kingine ni ustaarabu wa chombo cha habari chenyewe, hivi kwa nini chombo cha habari kwa umma kitumike kwa ajili ya kujibu ugomvi wa wamiliki. Chombo kiko pale kuhabarisha habari zinazotokea na siyo kutoa taarifa za matukio ya wamiliki wake. Hivyo kwa mtazamo wa kibiashara hiyo ni kutowatendea haki walaji wa habari. Hebu fikiria mzungu wa Uingereza afungue chombo chake hapa kwetu halafu kila siku awe anaonyesha jinsi aidha alivyobambikiwa kodi au alivyoombwa rushwa au alivyonyimwa kibali cha uwekezaji mahali fulani (sina maana chombo chake kisitoe taarifa za namna hiyo, maana yangu ni kwamba zile tu zinazomhusu yeye) unafikiri umma watanzania ungesemaje?.
 
Hivi, habari zinazotangazwa kuhusu serikali kwenye TBC zinachukua muda gani? au kwa vile TBC ni ya seriikali basi wanaweza kutangaza habari za Rais, Waziri, Waziri Mkuu n.k bila kutangaza habari za BAKWATA au TEC?
 
hapa nashangaa.. alipozungumza na waandishi wa habari tu watu wakasema kwanini asiende mahakamani, kawasikiliza kaenda mahakamani wengine wanashangaa kwanini ameenda mahakamani! Inanikumbusha ule wimbo wa "ooh jamani, binadamu hatosheki, hata ukimpa nini, milele hatorudhika ah!"..

Kwa kuwa Mengi ni muumini mzuri wa press freedom, na kwa kuwa ni mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa vyombo vya habari, nilitarajia kuwa angeenda kwanza kwenye Baraza la Habari kwa mujibu wa code of conduct ambayo wadau wa masuala ya habari nchini wanataka ifuatwe. Kwenda Mahakama Kuu naona imekuwa ni hatuaya juu sana
 
mm naogopa usije ukatwambia magazeti yake ni kama injili,na wahariri wake ni akina Mathayo, Luka na Yohana.

Si lengo langu kumtetea Mengi, sifungamani na kila kitu vyombo vyake vya habari vinachoandika au kutangaza isipokuwa pale wanaporipoti ukweli. Hata hivyo lengo langu ni kusisitiza kuwa haki inaweza kupatikana mahakamani kwa yeyote anayekashifiwa. Kama kuna watu walisita basi walijitafiti na kugundua kuwa hawana kesi. Dk.Slaa alishapewa muda kuwaomba radhi baadhi ya mafisadi wa EPA na wengine la sivyo wangemshtaki, alipowaambia watangulie mahakamani wakafyata mpaka leo, walijitafiti wakaona yatafumuka mengi bora waache. Hata hivyo sidhani kama Mengi ameshtaki yote waliyoandika, yenye ukweli kayabana. Mtindo wa watu kununua vyombo vya habari kutekeleza matakwa yao ya kisiasa na kibiashara ni lazima ufe. Waandishi wa habari wanaokubali kununuliwa kwa ajili ya kuchafua watu, nao pia ni lazima wakumbane na mkondo wa sheria, mpaka watakapofahamu maana ya taaluma yao na maadili na miiko yake.
 
Hivi, habari zinazotangazwa kuhusu serikali kwenye TBC zinachukua muda gani? au kwa vile TBC ni ya seriikali basi wanaweza kutangaza habari za Rais, Waziri, Waziri Mkuu n.k bila kutangaza habari za BAKWATA au TEC?

Kwa hiyo Mengi kwako ni serikali? Mzee Mwanakajiji wewe ni mchambuzi mzuri naogopa usije ukawa umeanza mambo ya akina Salva na Ulimwengu waliyofanya kutupikia Kikwete kwa miaka 10. Tumekuja kupakuliwa kumbe mtu mwenyewe hajakomaa hata maswali madogo tu anashindwa kujibu.
 
Back
Top Bottom