News Alert: Mbeba Vibuyu wa Rais afariki?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,695
40,721
Jamani habari ambazo bado hazijathibitishwa toka ndani zinasema kuwa yule mganga maarufu (siyo daktari) wa Rais Kikwete ambaye amekuwa akimsaidia kwa namna mbalimbali kwa miaka sasa amefariki dunia. Habari hizo ambazo zinatoka karibu na chanzo kabisa cha Mbeba Vibuyu huyo zinasema Mzee huyo (jina limekumbatiwa) alifariki muda kidogo uliopita (sijui kama ni siku, miezi).. Kwa vile habari hizi zina unyeti wa Usalama wa Taifa nimeshindwa kupata msemaji wa Serikali au kiongozi yeyote kuzungumzia. Naomba mwenye data zaidi za msiba huu wa msaidizi maalum (ndiyo cheo chake kilikuwa) wa Mkuu ili tutoe rambirambi.

Maswali yenu yote jibu ni "Sijui"!

M. M.
 
Sijui, lakini habari kama hizi ungekuwa unatupasia sisi akina yakhe tuzifikishe mahali kama hapa kwanza, au unasemaje? Kwa mstakabali wa mambo mazito ya taifa, habari kama hii tunaiweka wapi, A au Z?
Hii ni kwa maoni yangu tu, pengine kwa kukuonea gere! Hii haina maana kuwa huruhusiwi kushiriki katika mambo kama haya, lakini inapozidi kiasi (? sijui kipimo gani); hapo linakuwa tatizo.

Nisamehe kama nimekosea.
 
yeah, hii ni habari nzito sana.. hasa mshauri wa karibu wa Rais anapofariki mtu ambaye alikuwa anamtegemea kumfikisha alipofika. On the other hand, yaweza kupelekwa kwenye vibweka vya wakubwa!
 
Sijui, lakini habari kama hizi ungekuwa unatupasia sisi akina yakhe tuzifikishe mahali kama hapa kwanza, au unasemaje? Kwa mstakabali wa mambo mazito ya taifa, habari kama hii tunaiweka wapi, A au Z?
Hii ni kwa maoni yangu tu, pengine kwa kukuonea gere! Hii haina maana kuwa huruhusiwi kushiriki katika mambo kama haya, lakini inapozidi kiasi (? sijui kipimo gani); hapo linakuwa tatizo.

Nisamehe kama nimekosea.

kwenye udaku na nyepesi nyepesi

mkjj under the bekt kaka
 
Naona wikendi imeshaanza....aaah mi ngoja nimtafute bosi wangu nione kama ataniruhusu niondoke. Kichwa kinaniuma
 
pole wenzio tukijisia kuondoka tunachomoka tu halafu unatuma text!! on the other hand.. hawa jamaa hawachelewi kukupa likizo ya kudumu kabla tu ya Krismasi.. so miye siondoki hadi kengele ilie!!
 
"habari hizi zina unyeti wa usalama wa taifa".....yaani wakina "maalim kisisina" nao siku hizi kwenye ma-corridor makuu?. Ama kweli TZ ipo kwenye karne ya 21!!.
 
"habari hizi zina unyeti wa usalama wa taifa".....yaani wakina "maalim kisisina" nao siku hizi kwenye ma-corridor makuu?. Ama kweli TZ ipo kwenye karne ya 21!!.

Ndo maana mara nyingi humu wana JF huandika hivi sijui watz nani katuroga??

Sasa jama mkuu wa kaya na wabeba vibuyu tena??

Safari bado ndefu sana!
 
ahhh yaani imo kati kati mwa udaku na vibweka vya wakubwa
sasa kama ni kweli does it mean ndio itakua mwanzo wa kushuka kwa huyo muungwana?ama ndio nafasi ya kazi itatangazwa kwa wengine wenye required sifaz?
 
Its coming up... lakini jamani tusiwe wanafiki.. mambo ya vibuyu yapo na yameendelea kuwapo.. sasa kwanini tunaogopa kuyazungumzia..?
 
Nasikia mbeba vibuyu alizidi omba omba. Alipopewa furushi la mwisho akaanguka nalo. Lakini kama msemavyo, hivyo ni vibweka vya wakubwa tu.
 
Hivi Kwa Nini Mchizi Kila Akitaka Kwenda Nje Kwanza Anaenda Kwa Babu[sijui Al Marhum Sasa] Bagmoyo Na Akirudi Tu Kabla Hajafanya Chochote Kwa Babuu..sasa Hizi Ruti Zitaisha ...msiba Mkubwa Sheikh!!!
 
Lakini Wakuu Kamati Ya Ufundi Ya Mzee Humu Ni Habari Nzito..na Mwaka Jana Tulikuwa Na Thread Maalum Iliyoongelea ....jinsi Kamati Yake Ya Ufundi Ilivyofanya Kazi Pamoja Na Kampeni Zake..hadi Kafara Zake ..kama Mod Anaweza Anaweza Kuibua Ile Thread!!!
 
Mzee Mwkjj

Ibilisi yule mkuu wa vibuyu anafurahi sana akisikia watu wakitia shaka kuhusu kuwepo kwake.
Elim Dunia.
Naona kuna watoto wengi sana humu hawajui umuhimu wa wasaidizi wa Rais.
Kuabudu nguvu za vibuyu ni imani yenye wafuasi wengi sana hapa duniani, Tanzania nayo haiko nyuma kwa hilo.
Nisha wahi sema msafara wa rais una watu wengi sana wakiwemo makuwadi na wabeba hirizi au vibuyu, nilikuwa sitanii.
Subirini kidogo! Mtasikia habari kwamba kuwadi wa rais apigwa chini.
Acha rais wa nchi, maaskofu wa makanisa wenye kofia majoho na mikongojo yao wanawabeba vibuyu!
Mguu mmoja ndani mwingine nje.
Mkuu wa vibuyu mwenyewe akiitwa kuja kukalia kiti cha Askofu au rais anafurahi kweli kwani ni wasaa wake wa kuwa vuruga viongozi hao akili kiasi cha hata wao wenyewe kushindwa kufaidi rojo.

mambo ya imani hizi za giza yamo katikati ya heshima na utukufu wa viongozi wengi Tanzania, ni mzigo kwao na kwetu pia.
 
Yule bwana aliyemdondosha pale jukwaani MZA, ilikuwa ni vibuyu vilivyogongana; kibuyu kilichoshindwa kikadondoka chini.

Sijui yule bwana aliishia wapi; bado yumo lupango ama aliachiwa?
Wao wangekubali tu, kuwa kibuyu chake kilikuwa zaidi ya hicho chao wakubwa.
 
acha visa kumtaja jina huyo mzee ishakuwa big deal


halafu mnataka ukweli na uwazi

give me a break
 
Back
Top Bottom