News Alert - Mashamba ya Ballali yavamiwa

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,816
679
Kuna habari kwamba wananchi wa Mbweni wamevamia mashamba ya Ballali na kugawana. Polisi wameenda kuwatimua.

Hii kali kweli, wananchi wanachukua kilicho chao.

Wenye habari zaidi tujulisheni.
 
kama hii habari ni kweli, basi tujue kwamba mafisadi wametufikisha safari waliyoianzisha. kwani matokeo ya
ufisadi ni wananchi kuanza kujichukulia kwa nguvu kile
ambacho wanaimani kwamba wamedhulumiwa.
 
Ni makosa kwa wanachi kujichukulia sheria mkononi. Endapo Ballali ana documents halali za kumiliki mashmaba yale zilizotolewa na serikali, basi inabidi serikali itekeleze wajibu wake ikiwa ni pamoja kusimamia uhalali wa documents inazotoa kwa kuwachukulia hatua ya kisheria wavamizi hao.
 
Ukweli au ndio nyepesi???????wekeni data...au kama mpo ktk eneo la tukio semeni tupo ktk eneo la tukio....
 
Hii habari ni kweli, nime confirm, kwa walioko TZ wanaweza kuangalia taarifa ya habari.
 
Ninapenda kutibitisha hizi habari kwamba ni kweli wananchi wamefanya Uhalifu huo . Nasema ni uhalifu kwa kuwa ni mali za Ballali no matter what lakini kisheria ni mali yake .
 
Ninapenda kutibitisha hizi habari kwamba ni kweli wananchi wamefanya Uhalifu huo . Nasema ni uhalifu kwa kuwa ni mali za Ballali no matter what lakini kisheria ni mali yake .

Ni kweli- mali halali zilizopatikana kwa njia haramu. Kama kweli serekali ina ushahidi wa kutosha kuhusu Balali basi wamnnyang'anye hayo mashamba, majumba aliyojenga, magari aliyonunua na hela zote zilizoko kwenye akaunti zake.
 
That's bullying unless otherwise! The government should peacefully take appropiate procedures to resolve all the corruption charges against our 'Future Chokoraa'. He'll definately leave a mark for others to follow
 
Kuna habari kwamba wananchi wa Mbweni wamevamia mashamba ya Ballali na kugawana. Polisi wameenda kuwatimua.

Hii kali kweli, wananchi wanachukua kilicho chao.

Wenye habari zaidi tujulisheni.

Hata mimi nimeambiwa kuwa hili limetokea na naona MC ameweka pia palek kuwa hii habari imesemwa ITV. Tunakoelekea huko sijui kwani kuna watu wengi wanapenda kuona justife ikifanyika na isipofanyika ndio haya yanatokea.

Nadhani kina Karamagi, Mramba na Mgonja wanaona hili.
 
Sawa ni uhalifu, wamekiuka sheria lakini message sent! Kina Mramba, Mgonja, ANBEM, Kagoda etal.. wote wake wakae tayali, lazima warudishe kilicho chetu, ikitoka hapo hatua inayo fuatia, ni kuitia ma VX yao mwizi na kuyapiga mawe, hadi vibaka wa hela zetu washuke tuwashughulikie kama vibaka wengine wa kuku na miwa!
 
Hizi ni salamu kwa mjomba. Tumia sheria kuturudishia chetu toka kwa mafisadi au tutatuchua wenyewe.Safi sana
 
Naona watanzania mnajifunga magoli wenyewe. Mnavyomsulubu Balali, attention inaondoka kwenye issue kubwa. Na big fish wataendelea kupeta tu.
 
There is a lot of pending issues hazina majibu .Buzwagi hadi sasa ni kimya. Yaani haraka Ballali kaondolewa kaachwa Karamagi mwenye ushahidi wa kutosha wa kuweka sahihi kule UK . Jamani ama kweli kama kama wewe si mwanamtandao.Sasa Watanzania wanasahau yote soon wataimba sifa kwa JK na kusahau kwamba wanachezewa tu na hakuna wa kushitakiwa wala nini .
 
kama kweli hili limetokea ninapata mashaka sana.

Yaani watanzania ninaowajua mimi wanaweza kuwa na ujasiri wa kufanya hivi!-Watanzania wale wapole, ambao wako tayari kugeuza shavu la upande wa pili. hataaa hapa si bure kuna namna.

Mimi ninajiuliza kama kweli hili jambo limetokea ni nani atakuwa behind this?.

Hapa kuna namna, mojawapo ya namna inaweza kuwa ni kudivert attention ili Balali aonekane ndiye mkosa mkuu na jamii ikae kumwandama yeye pekee.

au inaweza kuwa behind wanasiasa uchwara wanaotaka eti ionekane wananchi wamekasirika sana na tukio la BOT.


lakini kwa yeyote ambaye ameongoza move hii atakuwa ameramba garasha, hii siyo stratergy ya ushindi hata kidogo.

dawa ya kumsulubu balali na wenzake ni kuwasimamisha kizimbani tu au mamlaka zizuie mali yao kihalali.
 
There is a lot of pending issues hazina majibu .Buzwagi hadi sasa ni kimya. Yaani haraka Ballali kaondolewa kaachwa Karamagi mwenye ushahidi wa kutosha wa kuweka sahihi kule UK . Jamani ama kweli kama kama wewe si mwanamtandao.Sasa Watanzania wanasahau yote soon wataimba sifa kwa JK na kusahau kwamba wanachezewa tu na hakuna wa kushitakiwa wala nini .


Lunyungu hii ni kweli kabisa, unajua kuna mambo mengine yanasikitisha sana. Angalia issue ya Prof Mahalu, Brother Ditto, Karamagi na Buzwagi, Richmond, ni kama zinaelea elea tu, na ni kama zinataka kuwekwa kapuni. I am starting to belive that hii ya Balali inatumika kama issue ya ku cover up yote. aanza kuelewa polepole ni kwanini Balali alikataliwa kujiuzulu au kujiuzulu kwake kulikuwa kunafichwa, naona kama lengo lilikuwa ni kumtangaza kuwa amefukuzwa ili story yake ifunike mengine yote!!
Hizo issue nyingine tukizisahahu kweli tutakuwa wa ajabu sana. I wonder tunakwenda wapi!
 
1. Hayo mashamba yana ukubwa gani?
2. Yako katika hali gani? yameendelezwa au ni msitu wa chatu?
3. Na je aliyapata kihalali?

Wananchi kuvamia maeneo ni jambo la kawaida haswa kama maeneo ambayo ni msitu na yanaonekana yamekaa muda mrefu bila kuendelezwa au mmiliki wake kutoonekana sehemu husika. Issue kama hii ilitokea kibamba zamani kidogo, ambapo 'serikali ya kijiji' iliamua kuyagawa maeneo ambayo hajaendelezwa.
baada ya hapo kilichotokea watu waliuawa (kwa kupigwa risasa na walinzi) wenyewe walijitokeza na kuweka ulinzi,
then serikali ya kijiji ikasalimu amri.

Issue inakuzwa kwa sababu ni balali! lengo na madhumuni ni nini! kuwafanya wananchi wasahau!

Nahisi watafanikiwa kama juhudi za makusudi hazitafanyika kupuuza mambo ambayo si muhimu na kuelekeza juhudi katika yale ambayo yanatikiwa majibu! Richmond! Buzwagi! BOT n.k

Vyombo vya habari vikatae kununuliwa! Madhara yanayopatikana yanaumiza wananchi wote ikiwa pamoja na waandishi wenyewe!
 
LINK HIII!!!http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2008/01/20/106674.html

Balali aanza kuporwa mali

2008-01-20 09:58:34
Na Mashaka Mgeta na Job Ndomba​

Aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT), Dk. Daudi Balali bado mzimu mkali umezidi kumuandama kufuatia mashamba yake kuanza kuporwa.

Wananchi wenye ghadhabu, wamevamia maeneo ya ardhi anayomiliki Dk.Balali, katika kijiji cha Maputo, Kata ya Bunju, nje kidogo ya Jijji la Dar es Salaam na kuanza kujigawia viwanja bila presha.

Hatua hiyo imefikiwa jana, ikiwa ni siku chache baada ya taarifa ya ukaguzi wa BoT, iliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bw. Ludovick Utouh, kubaini upotevu wa takribani Sh bilioni 133 kupitia Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA).

Ufisadi dhidi ya fedha hizo uliofanyika chini ya uongozi wa Dk. Balali, ulisababisha Rais Jakaya Kikwete, kutengua uteuzi wake (Balali) na kumfuta kazi katika nafasi ya Gavana wa BoT.

Katika tukio la jana, wananchi waliokadiriwa kufikia 200, walivamia mashamba mawili yenye ukubwa unaokadiriwa kuwa zaidi ya hekta 15 kila moja, kisha kugawana vipande kwa madai kuwa, ununuzi wake, ulifanywa kwa kutumia fedha `zilizoporwa\' BoT.

``Walipofika hapa walianza kujiorodhesha majina, kisha wakagawana eneo lote wakidai kuwa shamba hili lilinunuliwa kutokana na fedha za BoT,`` alisema mlinzi wa shamba la Bw. Balali, lililopo katika kijiji cha Maputo, kata ya Bunju, Bw. Stoni Madembo.

Bw. Madembo, aliyeanza kulinda shamba hilo miaka mitatu iliyopita, alisema wananchi hao, walikuwa na shoka, panga, majembe na fyekeo, lakini hapakuwa na vurugu wala machafuko.

Alisema mmoja wa wakazi hao, aliorodhesha majina ya watu waliokuwa wanahitaji ardhi, huku mwingine akihesabu hatua ishirini kwa ishirini katika eneo hilo, na kuzimilikisha kwa raia waliokuwapo.

``Baada ya kugawana, walisema eneo la nyumba ndogo ninayoishi, nitachukua mimi, lakini wakati huo nilikuwa nimeondoka kwenda kutoa taarifa kwa Diwani,`` alisema.

Pia, Bw. Madembo, alisema baada ya kumtaarifu Diwani wa kata hiyo, aliwasiliana na msimamizi wa ardhi ya Bw. Balali, aliyemtaja kwa jina moja la Bw. Kiwanga.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Maputo, Bw. Michael Mgongolwa, alikiri kuwepo kwa tukio hilo, na kumtambua mtu aliyehusika katika uandikishaji majina ya wahitaji wa maeneo katika shamba la Bw. Balali, kuwa ni Bw. Seleman Bwatu.

Alisema mpango wa kugawana ardhi ya Bw. Balali, ulijulikana tangu juzi, alipopata taarifa kupitia kwa diwani wa kata ya Bunju.

Bw. Mgongolwa, alisema diwani huyo, alimpigia simu saa 3 usiku, akitaka kujua usahihi wa taarifa za kuwapo mpango huo.
Alisema, alifika katika eneo la tukio na kuwakuta wananchi wakiendelea kugawana ardhi hiyo.

``Nilipowahoji kuhusu uhalali wa kugawana ardhi hiyo, walianza kunirushia maneno, wengine wakitaka kunipiga na kusema kwa kuwahoji hivyo, mimi sifai kuwa kiongozi, nikaona ili kujiokoa, nikaondoka,`` alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo, waliwasiliana na polisi waliofika katika eneo la tukio na kukuta baadhi ya wananchi wakiwa wameondoka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Bw. Jamal Rwambow, alisema hadi kufikia jana jioni, alikuwa hajapata taarifa kutoka kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kawe, kuhusiana na tukio hilo.

SOURCE: Nipashe


http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2008/01/20/106674.html
 
Back
Top Bottom