News Alert: Kima kipya cha mishahara

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Nasikia Serikali imetangaza kima kipya cha chini cha mishahara... kama kuna mtu tayari anajua ni kiasi gani...?
 
UMESIKIA ! ooh, mie bado mkuu sijasikia ! kila mwezi zakhia anatangaza kima cha chini, lakini najiuliza wanaopata hiko kima cha chini ni akina nani ?
 
Hivi ni vima vya chini vya sekta binafsi, siunajua makampuni ya magabacholi hayalipi hata 48,000/- Tsh.

Na mishahara hii ni tofauti kulingana sekta,,, yaani Kilimo, habari na mawasiliano, etc. etc... sasa kiwango cha chini kabisa ni 65,000/- lakini sekta ya habari ni 250,000/- kunaweza kuwa na variation kidogo....
 
Data kamili ni hizi hapa,
Serikali imetangaza viwango vipya vya mishahara ya kima cha chini ktk sekta binafsi ambapo wafanyakazi wa ndani watalipwa sh 65,0000 kwa mwezi. wahudumu wa baa na nyumba za wageni watalipwa 80,000, nyongeza hiyo ya mshahara imetangazwa na bwana Chiligati ambaye ni waziri wa kazi ajira na maendeleo ya vijana. ameendelea kusema kuwa sekta ya madini,usafiri, na mawasiliano kima cha chini kitakuwa 350,000. wandishi wa habari watalipwa 250,000, kwa wale waliopo taasisi za dini wanatakiwa kulipwa 150,000 kwa mwezi aidha vyombo vya habari vya dini waliomba sana kiwango kiwe kidogo kwavile watu wake wanatoa huduma za kiroho. kwenye sekta ya afya wafanyakazi wanao uza madawa watalipwa 120,000, wakati makampuni ya kigeni ya ulinzi kima chao cha chini kitakuwa 105,000 mpaka 80,000 kulingana na ukubwa wa kampuni. kwenye sekta ya kilimo kima cha chini kitakuwa 65,000 na upande wa sekta ya maji hasa mabaharia wa meli za mizigo kima chao cha chini kitakuwa 225,000
 
Hicho KCC kitaanza lini? kama ni mwezi huu kwa bajeti ipi? lakini kama ni mwakani,basi sio habari tuendelee na suala la Buzwagi na BOT, isije hii kitu ikasahaurisha Wadanganyika masuala ya Buzwagi na ufisadi mwingine.
 
inaanza lasmi November mkuu ila isije ikawa ajenda yakutusahaulisha buzwagi na Bot
 
inaanza lasmi November mkuu ila isije ikawa ajenda yakutusahaulisha buzwagi na Bot

Na mimi nilikuwa najiuliza kwa bajeti ipi hasa

Jambo jingine, wanapoweka kima cha chini cha wafanyakazi wa ndani na wahudumu wa baa..tangu lini serikali ikaweza kufatilia kuona kama kweli wanalipwa kima hicho?

na kwa upande wa mahaousegirl/boy, je itakuwa sasa wanalala na kula kwao ama mshahara huo unakuwa unajumuisha nini?
 
siunajua serikali inabwatuka tu ovyo ovyo kwanza hawa wafanyakazi wa ndani na baa sijui kama wanachama chao cha kuwatetea. Serikali yenyewe ianze kwa kuonesha mfano maana wafanyakazi wake nao wako hoi. Ila sijajua kama mshahara wa h/girl unajumuisha na misosi na maradhi au la naona kwa hilo chiligati hajafafanua
 
inaanza lasmi November mkuu ila isije ikawa ajenda yakutusahaulisha buzwagi na Bot

Ndio hivyo Taifa Stars imeshindwa kutasahulisha machungu tulio nayo, so wamakuja na hiii, tupoe kwa muda, wao wanaendelea.
Then mabilioni ya JK, then Mama Atabeba mtoto aliye achwa na Mama yake, Drama/Arts/ Usanii somo nzuri nyie hamjui tu. Eti mnapenda Uchumi na sayansi, shauri yenu, mimi nimeisha anza kujifunza Drama naweza kuwa Fresh Prince of Bel Air? au Schawaz...or Marehemu Reagan
 
Data kamili ni hizi hapa,
Serikali imetangaza viwango vipya vya mishahara ya kima cha chini ktk sekta binafsi ambapo wafanyakazi wa ndani watalipwa sh 65,0000 kwa mwezi. wahudumu wa baa na nyumba za wageni watalipwa 80,000, nyongeza hiyo ya mshahara imetangazwa na bwana Chiligati ambaye ni waziri wa kazi ajira na maendeleo ya vijana. ameendelea kusema kuwa sekta ya madini,usafiri, na mawasiliano kima cha chini kitakuwa 350,000. wandishi wa habari watalipwa 250,000, kwa wale waliopo taasisi za dini wanatakiwa kulipwa 150,000 kwa mwezi aidha vyombo vya habari vya dini waliomba sana kiwango kiwe kidogo kwavile watu wake wanatoa huduma za kiroho. kwenye sekta ya afya wafanyakazi wanao uza madawa watalipwa 120,000, wakati makampuni ya kigeni ya ulinzi kima chao cha chini kitakuwa 105,000 mpaka 80,000 kulingana na ukubwa wa kampuni. kwenye sekta ya kilimo kima cha chini kitakuwa 65,000 na upande wa sekta ya maji hasa mabaharia wa meli za mizigo kima chao cha chini kitakuwa 225,000

..kwahiyo kama mtu una housegirl na shamba boy,unatakiwa ku-fork out 130,000/= kwa mwezi.

..deal liko hapa,je?kama we si mfanyabiashara na ni mtumishi wa kawaida wa kampuni au serikali,inakuwaje?

..yaani,je?vima vingine vinaongezeka vipi?au vipi?

..kwa kuwa hii ina ripple effect!

..ngoja tuone!
 
inaanza lasmi November mkuu ila isije ikawa ajenda yakutusahaulisha buzwagi na Bot

Sikumbuki hii issue kama kama hipo kwenye Budget ya 2007/2008.
Nafikiri wanajaribu kuwasahulisha wananchi masuala ya ufisadi.Wamejaribu kuwatumia makatibu na mawaziri kuzunguka nchi nzima kufunika issue ya ufisadi bila mafanikio. Wameona hakieleweki ufumbuzi ni kutumia idea chovu ya wezi "ukifukuzwa na mbwa mtupie kipande cha nyama."
 
Hivi mnajua watachukizwa kuwa hakuna aliye notisi kuwa wamewaongezea zaidi watu wa madini kima cha chini...? laki tatu na nusu hivi si mchezo, watawaambia kama hawajali sekta hiyo wangeongeza kiasi hicho.. wapinzani hawana hoja!
 
jamani na kule kwetu SMZ vipi KCC kikoje? mwenye data atuupdate

Habari za kawaida
Posted Date::6/21/2007
Zbar waongeza mishahara kima cha chini
Na Salma Said, Zanzibar

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imeongeza kima cha chini kutoka Sh50,000 hadi Sh60,000 kwa mwezi ikiwa ni nyongeza ya Sh10,000.

Akiwasilisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha wa 2007/2008 katika kikao cha Baraza la Wawakilishi jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na anayeshughulikia Fedha na Uchumi, Dk Mwinyihaji Makame Mwadini, alisema serikali imeongeza mshahara ili kuwapunguzia makali wafanyakazi wa kima cha chini.

Dk Makame alisema pamoja na ongezeko hilo, pia Serikali pia inapendekeza kuongeza posho ya usafiri kutoka Sh5,000 hadi Sh10,000 kwa mwezi na kiwango cha chini cha posho ya nyumba kitakuwa Sh3,600 kwa mwezi na kufanya jumla ya mshahara na maposho kufikia Sh 73,600 kwa mfanyakazi wa kima cha chini.

Mishahara kwa wataalamu na wafanyakazi wote wenye elimu ya kuanzia shahada ya kwanza na waajiriwa wapya wa kiwango hicho sasa watalipwa kuanzia Sh110,000 kwa

mwezi kwa mujibu wa ongezeko hilo la mishahara.

Waziri Makame alisema zoezi la uunganishaji mishahara na posho halikufanyika ili kusubiri mapendekezo ya kazi ya utafiti wa mageuzi ya utumishi. Alisema baada ya kukamilika kwa utafiti huo, zoezi hilo sasa litafanyika katika ujao mwaka wa fedha.

Alisema kiwango cha mshahara kitakachoanza kukatwa kodi kitaanzia Sh80,000 badala Sh60,000 za sasa.

Alisema Serikali kwa mwaka ujao wa fedha inapendekeza kuongeza malipo ya msaada kwa wazee kutoka Sh500 hadi Sh 3,000 pamoja na kuzingatiwa maslahi ya wastaafu kwa kupandisha kima cha chini cha pensheni kutoka Sh7,500 hadi Sh 15,000.

Kwa mujibu wa bajeti hiyo, SMZ kwa mwaka wa fedha 2007/2008 imepanga kutumia jumla ya Sh276.001 bilioni.

Kikao cha Baraza la Wawakilishi kimeahirishwa hadi Jumatatu ijayo ili kutoa nafasi kwa wajumbe kuweza kupitia bajeti hiyo kabla ya kuanza kuchangia.

source....http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=47
 
Serikali ya jamhuriya muunao w Tanzania,imetangaza rasmi kima cha chini cha mshahara katika sekta binafsi huku wafanyakazi wa majumbani wakipangiwa Sh 65,000, wafanyakazi wa sekta ya madini Sh 350,000 na wahudumu wa baa na nyumba za kulala wageni Sh 80,000 kwa mwezi na kitaanza kutumika rasmi Novemba Mosi.

Viwango hivyo vipya vimetokana na utafiti uliofanywa na Bodi ya Uchunguzi wa Mishahara katika sekta binafsi, ambayo iliteuliwa Aprili mwaka huu na Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, John Chiligati pichani , kufuatia Sheria mpya ya Kazi namba 7/2004, kifungu namba 35 (1).Akitangaza mishahara hiyo jijini Dar es Salaam jana, Waziri Chiligati, alisema viwango hivyo vipya vya kima cha chini vitahusu wafanyakazi wa sekta binafsi pekee.

Alisema mishahara hiyo mipya inagusa sekta zote ikiwemo ya kilimo, madini, afya, biashara na viwanda, ulinzi wa makapuni binafsi, huduma za usafiri na mawasiliano, maji, pamoja na wafanyakazi wa majumbani na mahotelini.

Tunatoas pongezi kwa serikali kwa hili la kupandisha mishahara, ingawa tu tungewaomba wajaribu kuangalia kama viwango vilivyopandishwa kama vinaweza kwenda sambamba na kupanda kwa bei ya vitu, otherwise hongera kwa serikali ya CCM, kwa hili!
 
Data kamili ni hizi hapa,
Serikali imetangaza viwango vipya vya mishahara ya kima cha chini ktk sekta binafsi ambapo wafanyakazi wa ndani watalipwa sh 65,0000 kwa mwezi. wahudumu wa baa na nyumba za wageni watalipwa 80,000, nyongeza hiyo ya mshahara imetangazwa na bwana Chiligati ambaye ni waziri wa kazi ajira na maendeleo ya vijana. ameendelea kusema kuwa sekta ya madini,usafiri, na mawasiliano kima cha chini kitakuwa 350,000. wandishi wa habari watalipwa 250,000, kwa wale waliopo taasisi za dini wanatakiwa kulipwa 150,000 kwa mwezi aidha vyombo vya habari vya dini waliomba sana kiwango kiwe kidogo kwavile watu wake wanatoa huduma za kiroho. kwenye sekta ya afya wafanyakazi wanao uza madawa watalipwa 120,000, wakati makampuni ya kigeni ya ulinzi kima chao cha chini kitakuwa 105,000 mpaka 80,000 kulingana na ukubwa wa kampuni. kwenye sekta ya kilimo kima cha chini kitakuwa 65,000 na upande wa sekta ya maji hasa mabaharia wa meli za mizigo kima chao cha chini kitakuwa 225,000

Miye nashangazwa na tofauti ya kima cha chini kati ya sekta na sekta ili hali hawa wote gharama zao za maisha ya kila siku ni zile zile. Ukienda kununua kilo ya nyama, kilo ya mchele, kulipia karo ya mtoto ya shule, kulipia pango, umeme au hospitali ya kulipia bei ni zile zile bila kujali kama wewe kima chako cha chini cha mshahara ndiyo kidogo kuliko vyote. Utakamuliwa bei zile zile! Kama ni kweli basi kwa mara nyingine tena siri kali imechemsha!
 
Back
Top Bottom