Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,474
- 39,987
Chama cha Msalaba Mwekundu nchini kimeendelea kupokea misaada ya kukipa uwezo wa kukabiliana na majanga yanayotokana na mafuriko ambayo yamesababisha maelfu ya watu kukosa makazi, chakula bora, na kuweka hatari maisha ya wananchi wengi wao wakiwa ni wazee, kina mama na watoto.
Awamu ya Pili ya michango inayochangwa kwa kuhamasishwa na mitandao ya JamiiForums.com, mwanakijiji.com, Issamichuzi.blogspot.com na kuratibiwa na kusimamiwa na Mtandao wa Wanataaluma Tanzania TPN imekabidhiwa kwa chama hicho siku ya Jumamosi mchana na kupokelewa na Mkurugenzi wa Maafa wa Chama hicho Bw. Joseph Kimaryo.
Akikabidhi michango hiyo Dr. Maua alifafanua kwa wananchi kuwa Chama cha Msalaba Mwekundu hakiendeshi kampeni ya Red Alert inayoendeshwa na Vodacom Foundation na hivyo kuondoa mchanganyiko ambao umetokea. Alisisitiza kuwa juhudi za kuwachangia waathirika ni za kila Mtanzania pasipo ulazima wa kutumia kwa makusudi kauli za kuwachanganya watu.
Misaada iiliyowasilishwa siku ya Jumamosi inafanya kiasi cha misaada ambayo imeshapatikana hadi hivi sasa kufikia thamani ya Shilingi milioni saba.
Zifuatazo ni baadhi ya picha za tukio hilo. Harambee hii inaendelea hadi tarehe 11 mwezi wa Pili ambapo tunatarajia michango zaidi itakuwa imepatikana. Mtu yeyote anaweza kuchangia kwa kupitia mitandao yote mikubwa ya simu nchini kwa kutuma neno "TPN" kwenda namba "15522" ambapo mtu atakatwa shs 250 kujiandikisha (mara moja tu) na kukatwa Shs 150 kwa siku thelathini bila ulazima wa kujisajiri tena bali atapokea uthibitisho wa kukatwa kiasi hicho kila siku.
Dr. Maua Daftari akikabidhi awamu ya pili ya misaada ya wadau wa kuchangia Chama Cha Msalaba Mwekundu cha Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi wa Maafa wa Red Cross Bw. Joseph Kimaryo
Bw. Mtsimbe anaelezea kuwa michango ya awamu ya pili imefikia gharama ya Shs milioni 5 ikiwa ni vitu mbalimbali kama vinavyoonekana.
a kipindupindu. Madawa hayo yana dhamani ya Zaidi ya TZS Millioni 1.3."> Mkurugenzi Mtendaji wa CAPS Limited na Mdau wa TPN Mzalendo Peter Marealle akikabidhi madawa ya choo kwa Mlezi wa TPN kwa ajili ya matumizi ya vyo vya Wahanga wa Mafuriko. Dawa hizi zinaua wadudu wote na harufu mbaya na hivyo kuzuia uwezekano wa magonjwa ya Kuhara na kipindupindu. Madawa hayo yana dhamani ya Zaidi ya TZS 1.3 milioni.
Dr. Maua Daftari akikabidhi awamu ya pili ya misaada ya wadau wa kuchangia Chama Cha Msalaba Mwekundu cha Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi wa Maafa wa Red Cross Bw. Joseph Kimaryo na kushoto ni Rais wa TPN Bw. Sanctus Mtsimbe