Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,732
- 40,839
Maamuzi ya kwanza kabisa yaliyotolewa kwenye kikao cha NEC Butiama ni hatua mahususi za kumuenzi Baba wa Taifa. Bado napitia nyaraka fulani kwani nilikosa kusikiliza vizuri sehemu ya kwanza (matatizo ya kiufundi) lakini naamini mambo makubwa mawili yaliamuriwa.
a. Kuchapisha maandishi, hotuba, na kazi za Mwalimu katika mkusanyiko maalum ili watu wengi waweza kuzipata (??)
b. Kuiagiza serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhakikisha kuwa Butiama inakuwa makao makuu ya wilaya Mpya wakati wilaya ya Bunda itakapogawanywa.
Maamuzi mengine ni pamoja na kuanzisha vyuo vya itikadi ya chama ili wanachama wa CCM wajue chama chao vizuri na pamoja na kuimarisha jumuiya za Chama (Vijana, Wanawake, na Wazazi)
Maamuzi hayo ya kumuenzi Nyerere yanaenda kinyume na madai ya Makamba na Kingunge kuwa NEC imeenda Butiama kama kikao cha kawaida na badala yake kimefanya maamuzi ya kumuenzi Nyerere ikiwa ni ishara ya Chama hicho kufufua mawazo na fikra za Mwalimu ambazo watu wengi wameona kuwa kimezisahau.