News Alert: Balozi Mpya Uingereza - Radhia Msuya

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,928
Mkuu wa Idara ya Marekani na Ulaya kwenye Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Radhia Msuya ameteuliwa kuwa Balozi Mpya wa Tanzania nchini Uingereza akichukua nafasi ya Balozi wa sasa ambaye atapangiwa kazi nyingine Ikulu.

Kwa mujibu wa Taarifa zilizopatikana kutoka Ikulu Jijini Dar, Balozi Msuya ambaye kabla ya nafasi yake ya sasa alikuwa kwenye ubalozi huo wa Uingereza amekuwa akifanya kazi nzuri ambayo inasemekana ilichangia sana katika kufanikisha ziara ya Rais wa Marekani nchini karibu mwezi mmoja zaidi uliopita.

"Balozi Radhia amekuwa akifanya kazi nzuri na Rais ameonelea kuwa wakati umefika kwa Bi. Msuya kubeba jukumu hilo zito" Alisema ofisa mmoja wa Ikulu ambaye alikataa kutaja jina lake.

Mwandishi wa habari hizi alipojaribu kumpata Balozi Radhia mapema asubuhi ya leo msaidizi wake amesema kuwa Balozi Msuya amepokea taarifa za kuteuliwa kwake kwa mshtuko mkubwa lakini pia kwa unyenyekevu na hivi sasa anajaribu kuanza mipango ya kurudi Uingereza kuanza jukumu lake hilo jipya.

Muda mfupi uliopita Balozi Msuya ametuma taarifa kwa vyombo vya habari akikiri kuwa kuteuliwa kwake ni imani kubwa ya Rais Kikwete kwake na yuko tayari kufanya kazi yake kwa uadilifu akiwatumikia Watanzania wote bila kujali asili zao, dini, au makabila.

KLHN inampa pongezi za dhati Balozi Radhia kwa uteuzi wake huo mpya.
 
Hongera kwako mama.
Lakini hivi kwa nini aondolewe Maajar. Naanza kujiuliza iwapo ameondolewa kutokana na uhodari wa msuya au alikuwa na udhaifu kwenye kazi yake?
 
Isije ikawa ni ile ya siku ya wajinga, maana haijatulia kabisa.

Yean Mkuu lazima uwe na hadhari - lakini naona baada ya changa la macho kule Butiama hii habari ni kweli.

Ninaloomba kama kuna mtu anajua wasifu wake huyu Bi Balozi mpya atuandikie hapa tuweze kumjua.
 
Taarifa hii ni nzuri kwa siku maalumu kama ya leo.Heri yao wale wanaosadiki na kuamini kila linalonenwa. Nice try!
 
Haiwezekani, ni siku ya wajinga. Mwanakijiji usije ukafanya watu wapate ugonjwa wa moyo kwi kwi kwi!!!!

Mama Majaar hawezi kuondolewa kwasasa.
 
Yean Mkuu lazima uwe na hadhari - lakini naona baada ya changa la macho kule Butiama hii habari ni kweli.

Ninaloomba kama kuna mtu anajua wasifu wake huyu Bi Balozi mpya atuandikie hapa tuweze kumjua.
Si inasemekana ni mwan jf..sasa kuna noma gani kama akitupa wanachama cv yake?
 
Haiwezekani, ni siku ya wajinga. Mwanakijiji usije ukafanya watu wapate ugonjwa wa moyo kwi kwi kwi!!!!

Mama Majaar hawezi kuondolewa kwasasa.
Hata mimi nashangaa sana kwani huyu mama amefanikisha uimarishaji wa CCM huko ma UK kwa kushiriki kikamilifu!
 
Hapana bana, ngoja wengine tu-reserve comment zetu maana hii siku (April`s first) kama alivyosema muungwana Fundi hapo juu ina matatizo yake.

So Bi. Radhia I will catch up with you kesho! and try to offer my insights-if any!

Happy fools day to you all!
 
Kweli haya ni mambo ya 1/4!

Content zenyewe zimekaa kushoto kushoto ... Radhia hawezi kuwaandikia wana habari kuwajulisha kuteuliwa kwake.

Maajar hawezi kutoka Ubalozini aende Ikulu, labda angesema anarudi Foreign Affairs ili kupangiwa kazi nyingine.

Swali la kizushi, Maajar kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi alikuwa Wakili wa kujitegemea, je, ubalozi wake ukitenguliwa inakuwaje? Anarudi kuwa Lawyer ama anapelekwa Foreign Affairs kukaa bench?
 
Keil,

Mama Majaar ni katika mabalozi ambao angalau wanachapa kazi zao vizuri kwahiyo hawezi kuondolewa na kurudishwa nyumbani labda kama wanataka kumpa kazi kubwa zaidi. Mwanakijiji kachemsha kwa kutumia jina la Majaar maana rahisi kila mtu kuona hapa kuna kitu sio sahihi.

Kuhusu swali lako, ni kwamba huyu mama sasa ni mfanyakazi wa serikali kwahiyo hata akirudishwa nyumbani ataendelea kuwa mfanyakazi wa serikali na kupelekwa popote Ikulu au foreign au hata kwenye wizara zingine.
 
Mwulizeni Lunyungu maana magodoro ya bwana mkubwa yanajulikana.
 
Kwa maadili ya fools day ni kwamba ukimaliza kudanganya mwishoni kabisa unatamka baya kuwa Tarehe mosi April huwa ni siku kubwa ya wajinga duniani. Usiposema hivyo watu wana haki ya kuaminika ulichokiandika na baadaye usilalamike ukiitwa mzushi au mwongo kama jambo lenyewe litathibitika kwamba ni uongo!
 
Mbona siku yenyewe ni mapema tu kwa saa za huku kwetu bongo! Acha wajiingize tu!
 
hata mimi nimeteuliwa na raisi kuwa katibu tarafa nchini venezuwela,karibuni wote kwa mapumziko mafupi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom