Baada ya Kutoka Ufaransa na Italy, JK kuelekea China Jumatatu

ndo raha ya kuchagua raisi kijana...safari tutazilipia na pia lazma aonyeshe kuwa bado damu ya chemka....
 
Jamani hali ni mbaya hapo nyumbani, wiki iliyopita nilikuwa Dar na nimemsikia mtu wa makamo kidogo ndani ya daladala akitamka kwa sauti na kwa kujiamini kwamba anaombea ikibidi muungwana avute now maana safari hii mpka 2015 ni ishu!Cha kuustaajabisha zaidi asilimia kubwaa ndani ya daladala ile walionekana kuunga mkono kwa vicheko na vichombezo ziada.

Mjumbe hauwawi!!!!!!!!!!
 
...acheni kina kilitime wamtetee na point yao anaitangaza Tanzania,sijawahi kuona lame excuse kama hii wazee na sijui anatutangaza vipi...jamani mwee huyu JK ni matatizo tuu na sijui anafikiria saa ngapi matatizo mazito kama rushwa na umaskini kama anasafiri kiasi hicho

Kuamini JK ndio wakufikiria tu kuhusu maendeleo ya nchi! ni mtindio wa ubongo/akili pia!!! JK sio katibu mkuu wa wizara ya miundo mbinu, sio mkugurugenzi wa ICT pale wizarani, sio kiongozi wa Costech, sio Principal wa CoET, DIT, UCC, sio mtaalamu wa ICT... so contribution yake ni ndogo,,, hao waheshimiwa niliowataja hapo juu na wengine ndio watuambie wao wamefanya nini ndio tuje kwa JK!!

Mnaoweza kupata mwana JF mmoja, anipatie ushahidi ambao hao wataalamuwa taasisi za ICT wamepeleka proposal ngapi kwa head of state yeyote awe Julius,Ali,Ben,Jakaya wakazi-reject?

Kwani leo hii how much George Bush is involved with day 2 day running of his country?,,, Wataalamu wanafanya mambo jamaaa analetewa report; hapa kwenu kila kitu rais, wewe mikono nyumba, saa kumi na moja grocery,

Nitaendelea kusema watu wengi wanaotuangusha ni wataalamu/wasomi wetu!!! sehemu mbalimbali, hata mikataba, masahihisho ya mikataba kwa kalamu ni wataalamu wetu tu wanaotuangusha!!!
 
Kuamini JK ndio wakufikiria tu! ni mtindio wa akili pia!!! JK sio katibu mkuu wa wizara ya miundo mbinu, sio mkugurugenzi wa ICT pale wizarani, sio kiongozi wa Costech, sio Principal wa CoET, DIT, UCC, sio mtaalamu wa ICT... so contribution yake ni ndogo,,, hao waheshimiwa niliowataja hapo juu watuambie wao wamefanya nini ndio tuje kwa JK!!

Kilitime, sina mashaka na uwezo wako wa uelewa lakini nashawishika kukuuliza kama unafahamu katiba yetu inampa madaraka makubwa kiasi gani Raisi wetu? Hao wote uliowataja ni nani anawapa kibarua, especially wakurugenzi na makatibu wakuu? Hujasikia baadhi yao wakijitapa kuwa 'by the way sijachaguliwa na wananchi nimeteuliwa na Raisi na ni yeye mwenye uwezo wa kuiondoa' au wengine wakisema 'raisi ameniamini hadi akanipa madaraka'
Sasa hapo unadhani wa kumshika shati ni nani kama sio Raisi ambaye sisi ndo waajiri wake moja kwa moja?
 
. WFP BOOST FOR SMALL FARMERS
. ROME

Tanzania is among African countries lined up for World Food Program(WFP) pilot project to improve production of small farmers, President Kikwete was told here today. The WFP Executive director, MS Sheeran, told the President during bilateral talks last evening, that the project due to roll out next year was designed to create guaranteed market and provide micro credit for farmers.

The project, to be supported by US billionaire Bill Gates and UN former SG Koffi Annan, also seek to evolve an insurance scheme that would reduce risk to samll holder farmers.

President Kikwete, reassured MS Sheenan that he would provide personal leadership to ensure that the project succeded. He offered to sell 20,000 tonnes of cereals from the Strategic Grain Reserve(SGR) to the WFP which supports refugees in the country.

REUTERS.
 
Rafiki yangu, tuko nyuma kwa kuwa sisi wananchi wenyewe tunampa raisi wajibu ambao sio wake!!! tukidhani yeye ndiye anatakiwa kufanya feasibility study, design, implementation and commissioning ya miradi ya Miundo Mbinu na mingine mingi!!! hilo ni tatizo kubwa sana kwa Watanzania...

Kupenda kujumlisha, jumlisha mambo kirahisi tu sijui ni uvivu sio nini??!!! ingekuwa wananchi kwa kupitia vyombo vya habari panapotekea tatizo wanataja bayana kwamba hapa aliyelala ni Kilitime, ni Mkurugenzi X,

Semeni, hapa idara x, imeboronga, sema hapa head of x ministry/institution ameboronga then people will be accountable!!! hata ukiteuliwa na rais lakini majukumu yalishaandikwa kwamba unafanya nini na uko accountable for what?
nchi watu wangefanya kazi,,, lakini vyombo vyetu vya habari pamoja na wasomi wengi kila kitu serikali,,, and what is serikali,,,ni jitu kubwa ambalo rais tu ndiye anawajibika... it is wrong,,, wengi wenu mko majuuu,,, blanders zikitokea wanahiti- to the responsible department au leader... sio kila kitu serikali, rais etc... hii inasababisha viongozi wa vitengo kulala.

Nchi imefika mahali hata jambo la serikali za mitaa halitatuliwi na serikali za mitaa, linasubiri serikali kuu, na hiyo serikali kuu yenyewe, mpaka president, prime minister aje...

Nawaasa wasomi, mkidhani tatizo la Tanzania ni la president aliyepo madarakani kwa miaka miwili ni upuuzi mtupu,,, tuna matatizo ya msingi yakuangaliwa kwa makini, bila jaziba,ukereketwa,ungunguri,ungangari,u-mpaka-kieleweke,u-saa-ya-ukombozi-ni-sasa etc..
 
Heshima mbele, Kilitime, ukisoma kwa makini kifogo post yangu, hakuna niliposema kuwa raisi afanye yote hayo, nilichomaanisha ni kwua Rais ana uwezo mkubwa wa kuteua viongozi wengi ambao wanatakiwa wafanye hayo...so hapo hujanijibu kwa nini tusimulize Rais iwapo hao aliowaweka, na sisi kwa kufuata approach yako tukiwauliza wanadai kuteuliwa na Rais, na sidhani kama utahitaji kukumbushwa ni kina nani mkuu!

Kupenda kujumlisha, jumlisha mambo kirahisi tu sijui ni uvivu sio nini??!!! ingekuwa wananchi kwa kupitia vyombo vya habari panapotekea tatizo wanataja bayana kwamba hapa aliyelala ni Kilitime, ni Mkurugenzi X,

Semeni, hapa idara x, imeboronga, sema hapa head of x ministry/institution ameboronga then people will be accountable!!! hata ukiteuliwa na rais lakini majukumu yalishaandikwa kwamba unafanya nini na uko accountable for what?

again, Kilitime, sidhani kama umesahau, watu wamepiga makelele sana kuhusu mikataba, na hususan Karamagi, mkataba upo hapa, sahihi ni ya kwake, unadhani tupige kelele kiasi gani, kama tunaona yeye ameshindwa kuwajibika, tunamuuliza Raisi aliyemweka pale, kwa sababu elewa Rais ni mwajiriwa wa Watanzania wote, kwa hiyo siamini kama tumekuwa wavivu kama unavotoa hizo allegations hapo!

nchi watu wangefanya kazi,,, lakini vyombo vyetu vya habari pamoja na wasomi wengi kila kitu serikali,,, and what is serikali,,,ni jitu kubwa ambalo rais tu ndiye anawajibika... it is wrong,,, wengi wenu mko majuuu,,, blanders zikitokea wanahiti- to the responsible department au leader... sio kila kitu serikali, rais etc... hii inasababisha viongozi wa vitengo kulala.

Hapo tunazungumzia serikali kwa maana ya the excecutive, umesahau siasa/civics/dev studies? kuna mihimili mingapi ya utawala? si tunauliza mhimili wenye mamlaka ya utendanji.watu wote hawawezi kuwa 'serikali' in the strict sense, ndo maana huwa unasikia 'serikali imeagiza. imeonya, imeelekeze,' nk, kwani ni wewe in person unashiriki yote hayo? si kuna watu tumewaweka pale ili watekeleze hayo? Halafu apo kwenye wekundu, mi nilikuwa sijui kama hapa JF inajulikana nani yupo majuu na nani yupo nyumbani mkuu!

Nchi imefika mahali hata jambo la serikali za mitaa halitatuliwi na serikali za mitaa, linasubiri serikali kuu, na hiyo serikali kuu yenyewe, mpaka president, prime minister aje...

Nawaasa wasomi, mkidhani tatizo la Tanzania ni la president aliyepo madarakani kwa miaka miwili ni upuuzi mtupu,,, tuna matatizo ya msingi yakuangaliwa kwa makini, bila jaziba,ukereketwa,ungunguri,ungangari,u-mpaka-kieleweke,u-saa-ya-ukombozi-ni-sasa etc..

Kumbuka mkuu, bado the final accountability inabaki kwa ofisi kuu...RAIS...yeye ndo mwenye madaraka ya mwisho kuamua hatima ya nchi yetu..kama anshindwa tunajitahidi kumkumbusha kuwa hapa sivyo, akishindwa ndo wananchi wanaweza kuamua sasa tumbadili!
 
Kuna taarifa za Jk kuahirisha hiyo safari ya China na kuamua kupata mapumziko mafupi ya faragha "mafichoni" ili aweze kutafakari mkutano wa CCM. Kwa walio karibu hebu tupeni nyeti za uamuzi huo, maana ilikua akitoka kuzika tu atimue.
 
wengi wenu mko majuuu,,,

Kumbe ukiwa majuu Utanzania wako unakuwa hafifu au.............sasa wale wanaofanya kwenye balozi zetu nao wakati wao ni kama huu. Waambie kwa lugha nyepesi basi.
 
Nakulilia Tanzania,

Maoni yangu yalikuwa ya Jumla na sio kukusahihisha wewe as individual, naheshimu sana mchango wako as well as your perception regarding president as an individual responsible for everything,,,

Nilichojaribu kuweka ni another side of the same coin.

Thanks
Kilitime
 
Kumbe ukiwa majuu Utanzania wako unakuwa hafifu au.............sasa wale wanaofanya kwenye balozi zetu nao wakati wao ni kama huu. Waambie kwa lugha nyepesi basi.

Du nadhani sikumaanisha hivyo mkuu!!! umenisingizia,,, nilisema huko majuu, kukitokea tatizo anayewajibishwa, anayelaumiwa na anaambia ni yule aliye-direct responsible na idara/kitengo na anatakiwa kuwa kujibu,

huko Bongo, kila kitu Rais, hata utupaji wa takataka pale mtaani mwangu,,,, ni rais ndiye hajaleta gari ya kuondoa taka...
 
Kuna taarifa za Jk kuahirisha hiyo safari ya China na kuamua kupata mapumziko mafupi ya faragha "mafichoni" ili aweze kutafakari mkutano wa CCM. Kwa walio karibu hebu tupeni nyeti za uamuzi huo, maana ilikua akitoka kuzika tu atimue.

Bora apumnzike na ulimbukeni wake anafuja pesa ya walipa kodi tu.
 
Kilitime

Kama hukumaanisha hivyo ni vizuri wote ni Watanzania wenye haki sawa then I will take it back.
 
Kumbe ukiwa majuu Utanzania wako unakuwa hafifu au.............sasa wale wanaofanya kwenye balozi zetu nao wakati wao ni kama huu. Waambie kwa lugha nyepesi basi.

Mkuu Dua,

Heshima mbele, ninamuamini sana mkuu Killtime kuwa hawezi kusema hayo akiwa na maaana ya hayo, ingawa hii imekuwa tatizo sana hapa forum wananchi wengi wanaamini kuwa ukiwa nje ya bongo, basi huna authority ya kuongela ishus za bongo,

hata Waziri mkuu mwenyewe unakumbuka alivyomjibu Mkuu Mwanakijiji, alitanguliza hiii hoja finyu na NONESENSE!
 
. WFP BOOST FOR SMALL FARMERS
. ROME

Tanzania is among African countries lined up for World Food Program(WFP) pilot project to improve production of small farmers, President Kikwete was told here today. The WFP Executive director, MS Sheeran, told the President during bilateral talks last evening, that the project due to roll out next year was designed to create guaranteed market and provide micro credit for farmers.

The project, to be supported by US billionaire Bill Gates and UN former SG Koffi Annan, also seek to evolve an insurance scheme that would reduce risk to samll holder farmers.

President Kikwete, reassured MS Sheenan that he would provide personal leadership to ensure that the project succeded. He offered to sell 20,000 tonnes of cereals from the Strategic Grain Reserve(SGR) to the WFP which supports refugees in the country.

REUTERS.

Hivi unafikiri hili lilitokana na uwepo wake kule au nitayari lilishafanyiwa makubaliano ya kuisaidia Tanzania kwenye nyanja hiyo kabla ya uwepo wake huko!.
 
m15.jpg Hizi ni dalili gani kwa rais wetu kusinzia msibani?Ndio kushindwa uongozi au mawazo?Au ndio atimiza ile kauli yake ya kuwa wapinzani hawamfanyi akose usingizi.Angalia hiyo attachment,halafu fikiria ingelikua wewe ungefanyaje?Picha kwa hisani ya bwana Michuzi Blog.
 
Wandugu tusilalamike sana kuhusu Safari za Mh. Rais, Bali tuangalie tunachoweza kufanya ili asitishe safari hizo kwani imeonekana Karibu Miaka Miwili Sasa tumesema humu kuhusu Safari za vingozi Nje Lakini Ndiyo Kwanza Zimeongezeka ,Je swali la kujiuliza kupiga kelele hapa kuhusu safari zake kunasaidia?Kwa wenzetu wa nigeria hizo safari zake ndiyo ingekuwa neema na angejikuta siku moja Anabaki huko huko alikokwenda ziarani hasa kwa mwenendo huu Nchi Unaoenda nao Lakini sisi wacha tutulie na kupiga kelele sana na hatujui nini tufanye kulisimamisha hili Kama Rais wetu asivyojua Umasikini wetu unatokana na nini pamoja na kuwa na kila Rasimali inayowatajirisha wengine Nje ya Nchi Hii.
 
View attachment 752Hizi ni dalili gani kwa rais wetu kusinzia msibani?Ndio kushindwa uongozi au mawazo?Au ndio atimiza ile kauli yake ya kuwa wapinzani hawamfanyi akose usingizi.Angalia hiyo attachment,halafu fikiria ingelikua wewe ungefanyaje?Picha kwa hisani ya bwana Michuzi Blog.
Sidhani Kama amesinzia anawaza Pipa Jumatatu na Mengi yanayomkabili kwa hivi Sasa.Nafikiri Sasa hivi unauelewa msemo wa mwasisi kwamba huko si kwa kukimbilia.
 
Back
Top Bottom