Lucchese DeCavalcante
JF-Expert Member
- Jan 10, 2009
- 5,471
- 733
Wakulu haya tena leo EPL ndio inaanza sasa nimeona nianzishe special thread ya The Magpies or The Toon na keshokutwa Jumatatu vijana wanaanzia kule old Trafford dhidi ya Manchester United. Newcastle United Fc ni moja ya vigogo wa soka England na hata ulaya ikiwa na mafanikio ya kufika nusu fainali kwenye Champions League msimu wa 2003-2004 na pia fainali ya UEFA Interoto Cup msimu wa 2001-2002.
TOON-MATES ... The boys gather for group snap
Miongoni mwa wachezaji mahiri kabisa kuwahi kuchezea timu hii ni pamoja na 'Wor Jackie' Milburn, Bobby 'Dazzler' Mitchell, Paul Gascoigne 'Gazza', Kevin Keegan, Andy Cole, David Ginola, Les Ferdinand, Alan Sherear, Nicky Butty, Damien Duff, na Michael Owen...
Kikosi cha sasa kimesheheni wachezaji mahiri na maarufu kama Alan Smith, Sol Cambell, Shola Ameobi, Kevin Nolan and Peter Løvenkrands. Pia wako na mchezaji wa Congo Kazenga Lua Lua mdogo wake mchezaji mahiri wa Congo Lomana LuaLua.
Karibuni sana mashabiki wa The Toon