New Zealand kuleta sheria mpya ya umiliki wa silaha

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern amesema mnamo siku chache zijazo atatangaza sheria mpya kuhusu umiliki wa bunduki katika nchi hiyo, baada ya shambulizi kwenye misikiti miwili ambamo watu 50 waliuawa.
Katika mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na shambulizi la kigaidi la wiki iliyopita, Waziri Mkuu Jacinda Ardern amesema katika muda wa siku 10 atakuwa ametangaza mabadiliko katika sheria ya umilikaji wa bunduki, ambayo amesema anatumai itaifanya hali nchini New Zealand kuwa salama zaidi. Mkutano huo umefuatia kikao cha baraza la mawaziri kilichoongozwa na Bi Ardern, ambapo mawaziri wote wamekubaliana kimsingi kuhusu mageuzi hayo.

Shambulizi la mtu mwenye itikadi kali ya mrengo wa kulia dhidi ya misikiti miwili Ijumaa iliyopita katika mji wa Christchurch liliuwa watu 50 na kuwajeruhi wengine wengi.

Mtazamo kuhusu bunduki wabadilika milele

Katika mkutano huo na waandishi wa habari waziri mkuu Jacinda Ardern alikuwa pamoja na naibu wake Winston Peters, kiongozi wa chama cha New Zealand First ambacho ni mshirika katika serikali. Siku za nyuma chama hicho kilipinga mabadiliko katika sheria ya bunduki, lakini wakati huu kimebadilisha mawazo.

47957164_101.jpg


Ulinzi umeimarishwa mjini Christchurch
Kiongozi wake, Winston Peters amesema shambulizi la Ijumaa iliyopita limebadilisha hali ya mambo milele, na kwa hivyo sheria pia zinapaswa kubadilika. Sheria za New Zealand kuhusu umilikaji binafsi wa bunduki zilikuwa legevu sana, na waziri mkuu Ardern amesema raia wengi wamekuwa wakiitilia shaka.

''Nimeeleza bayana kwamba wa-New Zealand wengi wamekuwa wakiuliza maswali kuhusu upatikanaji wa silaha za kivita mikononi mwa watu nchini. Hata hivyo, jibu kamili nitalitoa baada ya kuyashughulikia maamuzi ya baraza la mawaziri la leo. Bado yapo mambo ya msingi yanayopaswa kutazamwa kwa kina, nataka kufanya hivyo, haraka iwezekanavyo." Amesema Ardern.

DW
 
Back
Top Bottom