KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,157
Mkuu 'Kalunya', sasa nimekuelewa unachosema, lakini sikubaliani na msimamo wako.Point hivi wa chini maslai duni wanateseka wanakusanya kwa uzalendo Ili nchi iwe na pesa tuwe na maendeleo kwa jumla.Lakini wa juu wanazitafuna haswaa tena bila hata huruma, mabilioni na mabilioni na awachukuliwi hatua.Ripot ya CAG isiyofanyiwa Kazi ni SAwa na wimbo wa KILA jumapili kanisani,kama mamlaka hazichukui hatua kuwawajibisha wezi nini umuhimu wa CAG sasa,si SAwa na muimba kwaya tu kanisa.
Point nyingine watu wengi walikuwa wazalendo Sana wamefanya Kazi kwa uaminifu mkubwa leo hii walishastaafu ni masikini mbwa wanajutia uaminifu wao ikiwemo kuchekwa na jamii, serikali imewatupa na uaminifu wao.
Key points serikali kutochukua hatua za upigaji wa wachache ni kuwavunja moyo walipa kodi.
Ina maana wao pekee ndo wenye shida ya pesa,kuliko hawa wa chini wafanyao Kazi kama watumwa kwa maslai mbuzi,huku wanazikusanya kwa kupigwa jua, mvua,kazini masaa 12 tena bila overtime,posho , hardship allowence,na stahiki zote?
Au na wewe umo kwenye mfumo wa upigaji, maana nchi hii imelaaniwa kwa upigaji na majizi ya awamu ya nne yamerudi kazini.
Kwa hiyo, kwa maoni yako, kwa vile wakubwa 'wanapiga' na hawa wengine wote pamoja na uzalendo wao unataka na wao wageuke wawe wapigaji?
Mantiki ya namna hii uliiona wapi?
Unahimiza kila mtumishi aliye na nafasi, asitekeleze majukumu yake kwa uaminifu, kwa vile wakubwa wanapiga?
Unataka kila mwenye nafasi inayomwezesha kupiga, afanye hivyo, kwa sababu asipofanya hivyo, atastaafu akiwa maskini, na watu kama wewe mtakuwa mkimcheka kwa vile hakutumia nafasi yake kwa manufaa yake mwenyewe?
Haya ni mawazo ya kipuuzi kabisa.
Kama uovu unaofanywa na hawa viongozi juu ya nchi hii unakuumiza kama waTanzania wengine wote, huwezi kuja hapa na kushangilia maovu hayo hata kama ni kwa aina ya kukata tamaa kama unavyoonyesha wewe hapa.
Haya mambo ya uandishi wa kuzungukazunguka, ukionekana kushangilia uovu, kumbe nia yako ni kuumia kwa uovu huo, ni uandishi mbovu.
Sema wazi unachotaka kusema, usizunguke kama kusifu kumbe una maana ya kulaani.
Sasa unamulaumu nini huyo bosi hapo juu ambaye hata baiskeli hana, lakini analinda heshima yake na heshima ya nchi yake.
Wewe ni mmoja wa wapuuzi, na nimekuweka kwenye orodha hiyo hapa JF.
"KALUNYA", ni mpuuzi.
Bure kabisa.