New TARURA Parking Fee System inaenda kuwa aina mpya wizi na uonevu

Huu mwaka wa 2 situmi gari mjini
Gari mjini ni mastress tu....
Poleniiii wenye magari

Ova
 
Waaungwana Kama heading inavyoonesha hapo juu.

TARURA amekuja na namna nyingine ya kukusanya ushuru wa Maegesho ya Magari, Mfumo huu Mpya ni wa kielektroniki na uko based on Control Number.

Nimefanya Research ndogo na kugundua kuwa Huu utaratibu mpya mbao ni Mzuri umegeuka kuwa ainia ya Wizi na Uonevu Mkubwa.

Watu wengi sana wanalalamika kuwa wala hwakumbuki hata walipo park, lakini wakiingia kwenye Portal ya TARURA inaonesha wanadaiwa, wala haineshi uli park gari wapi.

Huu utaratibu ni wa hovyo sana, maana uko based only on plate numbers za gari, yaani Agent wao akiamua tu anaweza ku register Number za Magari hata akiwa chumbani kwake na Mkewe.

Naziomba Mamlaka husika ziingilie kati na kuwakemea TARURA na huu mfumo wao ambao unatoa room ya wizi, uonevu na Bughuza isiyo ya lazima.

Binafsi nina Magari matano, matatu yana mwezi wa tatu hayatembei, ila yote yanadaiwa na inaonekana ni deni la juzi tu.

Nitoe rai kwa wenye Mgari pitieni hii Portal ya TARURA, maana unaweza kuwa unadaiwa bila kujua mwisho wa siku ukaishia kugombana na Polisi.

Kuna tatizo. Hakuna namna ya mdaiwa kujithibitishia (verify) mahali na muda wa parking aliotumia kulinganisha na deni.

Details zaidi zinatakiwa. Au watoe risiti (printout) kwenye maegesho.
 
mkuu we kichwa kigumu sn aisee hakuna mtu anayepinga hio fee watu wanaongelea madeni wanaongelea madeni wanayoyaona kwe system wakati magari yao yako home, deni kubwa kuliko uhalisia, control number kugoma hivyo kushndwa kulipa kwa mda sahihi mpk deni kuongezeka na lingine mbn concerns zao zipo clear tu mzee?mtu kukataa kulipa ushuru wa maegesho ni issue nyingne kabisa haihusiani na hii mada acha kuvuruga watu
Ni hivi, hayo malalamiko sijayakataa, ila kwa uzoefu wangu na kazi hii, hayo madai ya ukubwa wa deni nina mashaka nalo kwa sababu madereva wengi, kwa uzoefu wangu, wakipark gari, hata kama imekaa nusu saa, wanadai ndiyo wamefika, mwingine atasema hajakaa hata dk tano, au anakuambia bado hajashuka yaani kiufupi wanatoa madai ya excuse kwamba wamekaa muda mchache.

Sasa, hoja yangu ni kwamba, ikiwa madereva wengi hawajui ni muda gani wamepark, na madereva hao hao wanadai deni ni kubwa, basi, madai ya ukubwa wa madeni ni batili kwa sababu deni kuwa kubwa au dogo inategemea gari imepaki muda gani. Na hapa uzoefu unanionyesha kuwa madereva hukadiria dakika chache kuliko uhalisia.

Halafu kingine, madereva wengi hawajui maana ya kuegesha. Hapa nina mifano; moja; dereva anakuja parking na kuegesha gari ila hashuki na atakaa hapo hata lisaa, nikienda kudai parking fee, dereva anajibu hawezi kulipa kwa kuwa hajashuka. Pili, gari inatoka getini, dereva anadaiwa parking fee anajibu hawezi kulipa kwa sababu hajaegesha gari.

Sasa, kama dereva kapark, na kabaki kwenye gari akidhania kuwa hatadaiwa, au amepark masaa kadhaa ila akadhani alikaa sekunde, huku mhudumu wa TARURA kamwingiza kwenye Mfumo, huyu dereva ni lazima alalamikie ukubwa wa deni maana japo alipark, hakujua kwamba amepark.
 
Details mfano T000DxV, location Buguruni Malapa, time 1230, parking attendant Rose.
Haiwezekani, basi waseme gari zote nchini kwa mwezi zilipie to parking fee standard ya 25,000...thru TRA payment system. Kwa mwaka discount, lipia miezi 10..park popote.

Huu ubabaishaji utaisha. Watakusanya mpaka waombe pooh! Shida yao makusanyo wala siyo kujenga barabara.

Everyday is Saturday................................:cool:
 
Hata hiyo ya risiti bado mlikuwa/ ni wasumbufu.

Mfano sasa hivi 12:20pm nimetoka kumdai dereva hela, anaanza kumwambia abiria alipe. Abiria anamwambia ni jukumu la dereva. Dereva anadai hana hela. NB: Mimi nipo Mamlaka nyingine siyo TARURA.
Holy Crap
 
Nani ana thibitisha au kuhakikisha hiyo bill unayopewa ni halali? Bora zile receipt ilikua mtu unaona umewekewa kuanzia muda flani hadi unapoondoka unaweza kuthibitisha. Lakini hii ya sasa kubambikiwa rahisi sana.
Wanataka kutuumiza
 
Mimi wiki iliyopita nilipack kisutu mida ya Saa mbili, kwa nusu Saa, baada ya hapo nikaenda Kkoo, mtu wa parking Kkoo ananiuliza umepaki wapi asubuhi hii? Mbona umechajiwa 4,500 kwa siku hii ya Leo ? Na hapo ni Saa Tatu asubuhi

Hizo ni MBINU za waziri wa fedha za kuongeza mapato ya Serikali.a
 
Hizo ni MBINU za waziri wa fedha za kuongeza mapato ya Serikali.a
Mbinu za kishamba, mwendazake, aliwaambia watz tushavuka hatua ya ujinga, tunajua kupambanua mambo na kutafakari.

CCM na ilaumiwe tu na aina viongozi waliowapandikiza.
Ni upuuzi kuiga mfumo wa ulaya huku hauna miundo mbinu ya ulaya, UK mfano, wewe park tu kindezi, fee inakufuata nyumbani kwako. Camera na IT systems zitawasiliana naye. Digitally kweli!

Everyday is Saturday...............................:cool:
 
Nenda shule ukadai pesa yako ya Ada,inaelekea shuleni hujafundishwa chochote wamekuibia,watu Wana complain wizi unaofanyika na si KULIPA,sisi dawasco tu walishawahi kutuletea bili ambayo si yetu,na tulishinda,kupitia watu wajinga Kama wewe wasiopenda kuishughurisha akili vilivyo ndo mnatuletea shida katika nchi hii,na mbaya zaidi utakuta umeshatuzalia watoto wa aina yako tayari,kwa hiyo tuna kazi kubwa
Una uhakika gani kama alipata Elimu Mkuu unaposema akadai Ada..
 
Halafu ni elimu gani mnataka pale mdaiwapo parking fees? Hili nimelikuta mara nyingi sana. Dereva anadaiwa parking fee anajibu embu nieleweshe/nipe elimu. Haya, akishapewa elimu anaanza kutoa excuse ili tu asilipe. Sasa hapa TARURA wanawaagiza mkalipe kwa control number. Sasa elimu gani tena hapa? Kwamba hujui benki? Yaani kama uambiwe 'hii dawa pima kijiko kimoja' halafu unaanza kutaka elimu ya namna ya kukishika kijiko.
Mkuu unakwaza sana watu kwa comment zako ujue!

Mada inayoongelewa hapa siyo unacho comment wewe.

Watu wanalalamika kuandikiwa parking fee za ghushi, yaani watu wengine hawajaondoa magari ndani lakini magari hayo inasomeka yanadaiwa tozo ya maegesho!

Sasa wewe umekazania ukwepaji wa malipo, nani kasema hilo?

Embu nenda na mada husika.
 
True.wanabeti Sana kama matraffic.Nilikuwa na daladala lipo garage mwezi mzima kucheck kwenye system Ina cheti tena cha ruti isiyo yake
 
Parking attendant kama hesabu haitoshi ana bet tu namba yeyeto.Muhimu ukipaki chukua ushahidi wa video.
 
Mkuu unakwaza sana watu kwa comment zako ujue!

Mada inayoongelewa hapa siyo unacho comment wewe.

Watu wanalalamika kuandikiwa parking fee za ghushi, yaani watu wengine hawajaondoa magari ndani lakini magari hayo inasomeka yanadaiwa tozo ya maegesho!

Sasa wewe umekazania ukwepaji wa malipo, nani kasema hilo?

Embu nenda na mada husika.
Kwenye madai ya ukubwa wa madeni, hata kwenye mfumo wa cash yapo.

Siyo kwamba haya madai yameanza wakati huu wa mfumo mpya. Mimi ni mzoefu wa hii kazi.

Sasa wabishi wamekamatika. Kama una analytical skills unaweza ukaelewa ninachomaanisha.
 
Waaungwana Kama heading inavyoonesha hapo juu.

TARURA amekuja na namna nyingine ya kukusanya ushuru wa Maegesho ya Magari, Mfumo huu Mpya ni wa kielektroniki na uko based on Control Number.

Nimefanya Research ndogo na kugundua kuwa Huu utaratibu mpya mbao ni Mzuri umegeuka kuwa ainia ya Wizi na Uonevu Mkubwa.

Watu wengi sana wanalalamika kuwa wala hwakumbuki hata walipo park, lakini wakiingia kwenye Portal ya TARURA inaonesha wanadaiwa, wala haineshi uli park gari wapi.

Huu utaratibu ni wa hovyo sana, maana uko based only on plate numbers za gari, yaani Agent wao akiamua tu anaweza ku register Number za Magari hata akiwa chumbani kwake na Mkewe.

Naziomba Mamlaka husika ziingilie kati na kuwakemea TARURA na huu mfumo wao ambao unatoa room ya wizi, uonevu na Bughuza isiyo ya lazima.

Binafsi nina Magari matano, matatu yana mwezi wa tatu hayatembei, ila yote yanadaiwa na inaonekana ni deni la juzi tu.

Nitoe rai kwa wenye Mgari pitieni hii Portal ya TARURA, maana unaweza kuwa unadaiwa bila kujua mwisho wa siku ukaishia kugombana na Polisi.

=====

UPDATES;

=====

TARURA Watolea ufafanuzi kuhusu malalamiko haya. Zaidi soma;

Thread 'TARURA WAfafanua kuhusu ada ya Maegesho ya Magari kidijitali' TARURA WAfafanua kuhusu ada ya Maegesho ya Magari kidijitali

=====

UPDATES

=====

Waziri Ummy Mwalimu asitisha utaratibu huu kwa muda.

Thread 'Waziri Ummy asitisha kwa muda mfumo wa kieletroniki wa kukusanya ada ya maegesho ya magari unaosimamiwa na TARURA' Waziri Ummy asitisha kwa muda mfumo wa kieletroniki wa kukusanya ada ya maegesho ya magari unaosimamiwa na TARURA

Mkuu uliona mbali sana
 
TARURA wamerudisha mfumo ule ule kama zamani unalipa kwa mtoa risiti,ile ya kulipa online imesimamishwa maana hasara zimekuwa nyingi na malalamiko pia.
 
Back
Top Bottom