New TARURA Parking Fee System inaenda kuwa aina mpya wizi na uonevu

Bramo

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
13,160
10,007
Waaungwana Kama heading inavyoonesha hapo juu.

TARURA amekuja na namna nyingine ya kukusanya ushuru wa Maegesho ya Magari, Mfumo huu Mpya ni wa kielektroniki na uko based on Control Number.

Nimefanya Research ndogo na kugundua kuwa Huu utaratibu mpya mbao ni Mzuri umegeuka kuwa ainia ya Wizi na Uonevu Mkubwa.

Watu wengi sana wanalalamika kuwa wala hwakumbuki hata walipo park, lakini wakiingia kwenye Portal ya TARURA inaonesha wanadaiwa, wala haineshi uli park gari wapi.

Huu utaratibu ni wa hovyo sana, maana uko based only on plate numbers za gari, yaani Agent wao akiamua tu anaweza ku register Number za Magari hata akiwa chumbani kwake na Mkewe.

Naziomba Mamlaka husika ziingilie kati na kuwakemea TARURA na huu mfumo wao ambao unatoa room ya wizi, uonevu na Bughuza isiyo ya lazima.

Binafsi nina Magari matano, matatu yana mwezi wa tatu hayatembei, ila yote yanadaiwa na inaonekana ni deni la juzi tu.

Nitoe rai kwa wenye Mgari pitieni hii Portal ya TARURA, maana unaweza kuwa unadaiwa bila kujua mwisho wa siku ukaishia kugombana na Polisi.

=====

UPDATES;

=====

TARURA Watolea ufafanuzi kuhusu malalamiko haya. Zaidi soma;

Thread 'TARURA WAfafanua kuhusu ada ya Maegesho ya Magari kidijitali' TARURA WAfafanua kuhusu ada ya Maegesho ya Magari kidijitali

=====

UPDATES

=====

Waziri Ummy Mwalimu asitisha utaratibu huu kwa muda.

Thread 'Waziri Ummy asitisha kwa muda mfumo wa kieletroniki wa kukusanya ada ya maegesho ya magari unaosimamiwa na TARURA' Waziri Ummy asitisha kwa muda mfumo wa kieletroniki wa kukusanya ada ya maegesho ya magari unaosimamiwa na TARURA
 
Mimi nimeeona wameanza kutuma meseji kwenye simu yangu kuhusu namna ya kulipa parking fees kwa M-PESA *150*00#>Lipa kwa M-Pesa>Malipo ya serikali kisha weka namba ya malipo kukamilisha malipo. Kwa utaratibu huu unaweza kushtuka unadaiwa laki 5 parking fee...
 
Nani ana thibitisha au kuhakikisha hiyo bill unayopewa ni halali? Bora zile receipt ilikua mtu unaona umewekewa kuanzia muda flani hadi unapoondoka unaweza kuthibitisha. Lakini hii ya sasa kubambikiwa rahisi sana.
 
Ni kweli, kiufupi, mimi mtu anidai papo hapo nimlipe, aingize yeye hiyo control number alipe. Vinginevyo aende akadhibitishe mahakamani kwamba hakuwa chumbani kwake akiingiza namba za magari kwa mtindo wa ana ana doo , kajambila pasto, na akabuni tu na za gari lolote akaingiza. Otherwise wawe wanainclude na namba za leseni ya aliepaki.
 
Sina Amani kabisa na huu utaratibu, kwani inakuletea ujumbe unaonesha deni bila maelezo ya eneo na muda husika

Ndugu mteja, ushuru wa maegesho wa chombo T121...
Unatakiwa kulipa kiasi cha Tsh. 2000
kumbukumbu namba yako ya malipo 994571542...
Lipa haraka kuepuka faini.

Kiukweli inakwaza
 
Nilipata control number nilipo jaribu kulipa muamala haukufanikiwa, nikauliza tena kama gari inadaiwa nikapewa jibu kama ujumbe unavyo onekana hapo.... Baada ya siku mbili deni likafika shs. 3000 sijui wanatumia formula gani?
 
Attachments

  • Screenshot_20211007_115207_com.android.mms.jpg
    Screenshot_20211007_115207_com.android.mms.jpg
    36.7 KB · Views: 18
  • Screenshot_20211007_120001.jpg
    Screenshot_20211007_120001.jpg
    37.4 KB · Views: 12
Una gari ya mamilioni ila bahili kulipa mia tano ya parking.

Mkata ushuru anakudai parking fee unamwambia hujakaa hata dakika 2 wakati nusu saa imepita.

Unapita getini unadaiwa jero ya parking/maegesho unadai hujaegesha. Ulitundika?

Unadaiwa jero ya parking unaanza kulia ooh sina hata mia. Unaendeshaje gari bila hela mfukoni?

Yawezekana kuna malalamiko lakini ya kweli yatakuwa machache sana kutokana na uzoefu wangu katika kazi ya kudai ada za maegesho/parking.

Yaani madereva wanajitoa ufahamu kwamba hawaelewi ama hawajui kama kuna tozo hizi. Kabisa, mtu anatokea ndani ya stendi au Soko ila mlangoni anadai kuwa hajaegesha gari.

Wengine wanajitutumua kwamba wao ni watu wa system na baadhi yao wanatoa vitisho.

Hivi kama mtu unasahau ulipaki wapi gari, je unaweza kukumbuka alama za barabarani ili kuepuka ajali?
 
Waaungwana Kama heading inavyoonesha hapo juu.

TARURA amekuja na namna nyingine ya kukusanya ushuru wa Maegesho ya Magari, Mfumo huu Mpya ni wa kielektroniki na uko based on Control Number.

Nimefanya Research ndogo na kugundua kuwa Huu utaratibu mpya mbao ni Mzuri umegeuka kuwa ainia ya Wizi na Uonevu Mkubwa.

Watu wengi sana wanalalamika kuwa wala hwakumbuki hata walipo park, lakini wakiingia kwenye Portal ya TARURA inaonesha wanadaiwa, wala haineshi uli park gari wapi.

Huu utaratibu ni wa hovyo sana, maana uko based only on plate numbers za gari, yaani Agent wao akiamua tu anaweza ku register Number za Magari hata akiwa chumbani kwake na Mkewe.

Naziomba Mamlaka husika ziingilie kati na kuwakemea TARURA na huu mfumo wao ambao unatoa room ya wizi, uonevu na Bughuza isiyo ya lazima.

Binafsi nina Magari matano, matatu yana mwezi wa tatu hayatembei, ila yote yanadaiwa na inaonekana ni deni la juzi tu.

Nitoe rai kwa wenye Mgari pitieni hii Portal ya TARURA, maana unaweza kuwa unadaiwa bila kujua mwisho wa siku ukaishia kugombana na Polisi.

Nimecheki nikakuta nadaiwa Elfu saba. Nimeshangaa nimepark wapi na kwanini nadaiwa kiasi hicho kikubwa? Kulipa ni wajibu. Ila hata kwenye mtandao, lazima waainishe lini na wapi nilipark bila kulipa. Vinginevyo itasumbua sana baadae. Wengi hawana elimu ya nini kinaendelea
 
Una gari ya mamilioni ila bahili kulipa mia tano ya parking.

Mkata ushuru anakudai parking fee unamwambia hujakaa hata dakika 2 wakati nusu saa imepita.

Unapita getini unadaiwa jero ya parking/maegesho unadai hujaegesha.

Unadaiwa jero ya parking unaanza kulia ooh sina hata mia.

Yawezekana kuna malalamiko lakini ya kweli yatakuwa machache sana kutokana na uzoefu wangu katika kazi ya kudai ada za maegesho/parking.

Yaani madereva wanajitoa ufahamu kwamba hawaelewi ama hawajui kama kuna tozo hizi. Kabisa, mtu anatokea ndani ya stendi au Soko ila mlangoni anadai kuwa hajaegesha gari.

Wengine wanajitutumua kwamba wao ni watu wa system na baadhi yao wanatoa vitisho.

Hivi kama mtu unasahau ulipaki wapi gari, je unaweza kukumbuka alama za barabarani ili kuepuka ajali?
Shida sio kulipa. Hupewi risiti halafu unakuta unadaiwa. Mbona mwanzoni tulikuwa tunalipa. Sasa hivi nini kinaendelea?
 
Mimi wiki iliyopita nilipack kisutu mida ya Saa mbili, kwa nusu Saa, baada ya hapo nikaenda Kkoo, mtu wa parking Kkoo ananiuliza umepaki wapi asubuhi hii? Mbona umechajiwa 4,500 kwa siku hii ya Leo ? Na hapo ni Saa Tatu asubuhi
 
Back
Top Bottom