New movies 2015- mabwepande and the wrath of the pliers | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

New movies 2015- mabwepande and the wrath of the pliers

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Richard, Jul 16, 2012.

 1. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: infobox vevent, width: 22"]
  [TR]
  [TH="align: left"]Directed by -
  [/TH]
  [TD="class: description"]Hon: Mizengo Pinda
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TH="align: left"]Produced by - Hemed Msangi, Alhaji Suleiman Kova
  [/TH]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TH="align: left"]Written by -
  [/TH]
  [TD]Bwana Deo
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TH="align: left"]Starring - Hemed Msangi, Suleiman Kova, Dr Ulimboka


  Guest starring - Rev Gwajima,
  [/TH]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TH="align: left"]Editing by
  [/TH]
  [TD]- Habari leo and Daily News
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TH="align: left"]Release date(s)
  [/TH]
  [TD]2015
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TH="align: left"]Running time
  [/TH]
  [TD]96 minutes
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TH="align: left"]Country
  [/TH]
  [TD]United Republic of Tanzania
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TH="align: left"]Language English, Swahili-


  [​IMG]

  Movie ikiwa bado inatayarishwa.


  Casting:

  Mama Kijo Bisimba, Dr Mpoki, Judge of Kisutu Magistrate Court and his team, Gangster Joshua aka Mkenya, Members of Police Force and special agents (mawakala).


  Location: Dar-es-Salaam, Dodoma and South Africa.
  [/TH]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Duuu nimeipenda sana hii!
   
 3. m

  mwanza_kwetu JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2012
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 684
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Good innovation- Liwalo na Liwe movies
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  UKITAKA KUJUA ATHARI ZA SINEMA ZA KIHINDI KURATIBIWA NA UONGOZI WA KI-CHINA BASI KAMUULIZE ALHAJI AFANDE SELE PALE 'MAMBO YA NDANI' NA JINSI GANI ALIVYOLITIA KOVU LA KUDUMU JESHI LA POLISI

  Kwa akili tu ya kawaida, busara zinatuamrisha ya kwamba pindi tunapoinuia kutengeneza sinema ama yaa Kihindi, Kimang'ati au hata ya Kichina, ni vema tukawapa nafasi watu wenye ufahamu mzuri na tamaduni za mahali husika wakatusaidia kuratibu mambo.

  Ajabu na kweli ni kwamba katika jaribio la kumchukua uhai Dk Ulimboka, majina ambayo yatokea kutajwatajwa yametokea kuwa ni wa upande fulani tu. Madai ya Uhalifu huo ni wao, Uchunguzi ni wao, Usemaji ni wao, na hata Uratibu mzima bado ni wao tu.

  Hakika hili kidogo linatatiza kwa kuwa jeshi letu la polisi sote tunajua halina dini lakini kwa mwenendo huu wa mara Abeid wa Ikulu, Ahmed Msangi wa Kanda Maalum, Selemani Kova kubwa lao, Saed Mwema ambaye ndiye Back-stopper hapo -- mmmmmmhhhh!!!

  Japo ni jambo ambalo halisemwi wazi wazi na wengi LAKINI mmmhhhhh!!! Kwa nini na kwani kuna nini??? Siku zote Matokeo ya mambo kama haya, pengine ni ajali tu imetokea hadi hapo, mwisho wa siku huleta taswira kama vile ya Picha ya KIHINDI kuratibiwa vile na WACHINA.

  Mtu akiangalia ki-undani,
  pale kwenye ONYESHO LA PILI, jinsi gani ka-Gwajima (Mkristo) na Joshua (nalo jina la kikristo ila mbebaji wa jina hilo HATUNA UHAKIKA na dini yake mpaka atakapotuthibitishia kwa kinywa chake mwenyewe) wanavyovutwa kwa nguvu zote kuwa sehemu ya mchezo katika filamu hii - yote yanayojitokeza ni VITUKO VYA KARNE katika historia ya mambo ya kipolisi duniani kote.

  Kwa watazamaji wapya wa picha hii ya '
  KOVA KATIKA MABAWA YA MABADILIKO YA NGUVU YA UMMA NCHINI TANZANIA', kwa kukumbushia tu, ONYESHO LA KWANZA ilianzia pale Leaders' Club na kuishia Mabwepande Tegeta na walioonekana mwishoni mwa picha ile ni Mama Kijo Bishimba, Mzee Mwanakijiji, Mjeruhiwa Dk Ulimboka pamoja na wanakijiji katika yale mandhari asili ya MabwePande.

  Sababu ya kusema hivyo ni kwamba Alhaji Afande Sele (Kanda Maalum Jijini Dar), kwa kosa moja tu la kutokufahamu desturi na taratibu za madhehebu ya ki-Kristo ki-ajali kabisa kajikuta AMEUNGUZA PICHA ZIMA kwa kudai kwamba mgeni wake Joshua Muyungi alienda na AKATUBU katika kanisa la Nabii Mkuu na Askofu Gwajima juu ya uhusika wake kwenye jaribio la kumua Dr Ulimboka. Hii ndio maana kila wanapojaribu kuunganisha picha hizo mbili hali inaendelea tu kuwa kama mafuta ya taa na maji kwenye maabara zetu za kibongo hizi.

  Ukweli wa mambo ni kwamba mbali na Kanisa Katoliki ambako watu hujichagulia kwenda kwa Padre na kutubu dhambi zao, madhehebu mengine yote ya ki-Kristo hayana utaratibu huo. Lakini kwa kuwa Alhaji alikua anatafuta MNOGO WA PICHA YENYEWE ndio hapo maini yakaingia nyongo.

  Kama bado tu mtu hajashtuka kitu hdi hapo, hivi watu bado tu hamjiulizi kwa nini
  ONYESHO LA TATU (linalotegemewa kuwa ndefu sana mpaka hadhira kujikuta wachapa tu usingizi badala ya kuendelea kufwatilia picha) la filamu ilivyoanza kwaa usiri mkubwa katika mahakama ya Kisutu na kwamba wahusika wote huko wakawa ni WATU WA KUFIKIRIKA tu huku wengine wakidaiwa kuwasili tu kutoka katika taifa la KUSADIKIKA ('nimewasili na bado ninaendelea kuwazoea').

  Mpaka hapa wala mtu hahitaji kutngaziwa kwamba kwele Alhaj Afande Kova kalitia kovu chombo hiki, tulichopata kukiamini na kukithamini sana miaka hiyo, kwa namna ambayo itachukua miaka kuturudisha imani sisi Umma wa Tanzania.

  Sasa kilichobaki pengine ni wahusika wkuu wa filamu hii warudi tena mezani ili waje na ubunifu mwingine maana huu wa sasa ndio kama hivo umekwishagonga mwamba.
   
 5. D

  Deofm JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hapo mwisho nadhani walitaka kuwategeshea wananchi wenye hasira wampige huyo muuaji wa kutengeneza, akishakufa picha iishie hapo, lakini kwa vile watu wamekuwa wajanja inabidi turudi studio tubuni episode nyingine
   
 6. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Enyi wana-JF wenzangu,

  Ni nani kati yetu hapa anayeweza kututabiria ONYESHO LA NNE litakavyokua katika filamu hii mara baada ya kutathmini onyesho zilizotangulia, je?

  1. Kuna uwezekano filamu ikaishia hapa hapa?

  2. Kuna uwezekano filamu ikaanza upya?

  3. Yawezekana Staringi Dr Ulimboka akaibuka upya na kuipa nguvu zaidi picha hii?

  4. Kuna uwezekano steringi Dr Ulimboka akanunuliwa kwa kupewa KIFUTA DAMU (Mganga Mkuu wa Serikali Wizarani) na picha zima kupata taswira mpya?

  5. Yawezekana, kwa mara ya kwanza katika historia ya ulimwengu wa filamu duniani, huyu Steringi Dr Ulimboka wakamkolimba huko huko ili kinachodaiwa mezani hivi sasa ndicho kibakie ukweli na ukweli mtupu wa mambo (Afande Kova et al 2012)?
   
 7. M

  MTENGE Member

  #7
  Jul 16, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika onyesho la nne, watatafutwa watu wengine ambao watabebeshwa huu mzigo wa nani mhusika, maana ili picha iishe salama lazima watafute mtu watakayemtwisha mzigo walioubeba maana unawaelemea nisawa na kubeba gunia la mavi usipolemewa litakunukia, Inavyoonekana mkuu wa kaya amewapa muda wafanye haraka kumsafisha
   
 8. E

  Etairo JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 244
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimependa uchambuzi wako isipikuwa kuunganisha zoezi hili na imani za watu (udini) umechemka pa kubwa. Akitenda mkristo ingekuwa sawa kwa sababu tu ya ukiristo wake? Kuna taasisi ngapi kubwa na nyeti zinaongozwa na wakiristo tu bila hata harufu ya muislam? BOT, JWTZ,. Jadili mada bila kuegemea upande wowote-pima kwa matendo yao siyo imani waliyonayo.
   
 9. Mpitagwa

  Mpitagwa JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,298
  Likes Received: 213
  Trophy Points: 160
  kwa kweli hapa mimi ni mkristu lakini siungi mkono mtazamo wa udini hapa. Mbona DEO ni mkristu na yule anonymus wa Ikulu who knows his religion. Halafu watanzania hatuko wadini kivile sana sana tunazidhalilisha dini. Kumpendelea mtu mnayesali au kuswali pamoja hiyo siyo dini kwani dini zote msingi wao mkuu ni haki. Na ambacho alifanya Nyerere na sasa kikwete kwa kuzaja majina yanayoashilia dini moja siyo udini kwani mwisho wa siku wenye dini wenyewe wanaishi maisha ya choka mbaya. Mfano sasa angalia kilwa, mtwara lindi na hata hapa Dar ambapo waislam ni wengi zipo wapi huduma zilizoboreshwa kwa JK kuondoa akina John na kuwaweka akina Juma kwenye vyeo mbalimbali? Poleni washika dini kwa kudhalilsha na wanasiasa. wanawatumia vibaya. Ingekuwa ni udini, kipindi hiki kilwa kungejengwa hospital, shule, vyuo vipya ili jamii za kiislam zifaidi zaid. Lakini wapi.
   
 10. kiagata

  kiagata Senior Member

  #10
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ukisikia Tii,basi ujue kitu kimegonga mwamba.
  Unaweza kudanganya watu wote wakati fulani,lakini huwezi kudanganya watu wote wakati wote.
  Hapa ndipo tunapata picha huenda hata zile habari za...''ALIKUWA ANAPAMBANA NA ASKARI TUKAMSHINDA''labda kweli/siyokweli. TIME WILL TELL
   
 11. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #11
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  jamani tujifunze kutofautisha "msitu wa pande" na mabwe pande- tunaharibu radha.
   
 12. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #12
  Jul 17, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Hapa jana kulikuwa na THREAD inayosema kuwa SERIKALI kwa kupitia Afande Sele Kova anajipanga kufyatua kibao kingine cha Movie ambacho kitakuwa na Wahusika wakuu watatu (MAJAMBAZI WAWILI na RAIA WA CHINA MMOJA)

  Na kutokana na maelezo kuwa movie hii itakuwa kali kwani hata gari jeusi limeandaliwa na movie itachezwa kuanzia maeneo ya msituni.(Haijajulikana kama watatumia mabwe Pande au msitu upi)

  Bila shaka movie ijayo itakuwa nzuri zaidi ya ile iliyopita kwani ina wahusika wazoefu. (Majambazi = wataigiza sehemu ya kuteka nyara na kuua; Mchina sehemu ya kuruka Kung-Fu na kutesa kwa kunyonga shingo)

  Jiandaeni Watanzania kwa picha kali inayokuja na maandalizi yameshaanza.
  MIZAMBWA
  NABII MTARAJIWA!!!
   
 13. KeiEd

  KeiEd Senior Member

  #13
  Jul 17, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 127
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nionavyo mimi hii sio movie bali ni series kwani kutakuwepo na seasons nyingi zilizosheheni episodes nyingi zisizokuwa na mtiririko wa matukio, hapa ninamaanisha kuwa matokeo yanaweza kuwa nanaenda mbele na nyuma kulingana na upepo wa audience
   
 14. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #14
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  ah i thought location of the movie would be mabwepande ama?
   
Loading...