Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

I wish hawajamaa wangekuwa wanasikia haya! SIJUI UGUMU UNATOKA WAPI?
 
I wish hawajamaa wangekuwa wanasikia haya! SIJUI UGUMU UNATOKA WAPI?

Henge kwa ujumla katiba ya sasa inawatete mafisadi,inakataza rais akisha apishwa huwezi kwenda mahali popote kupinga,tume ya uchaguzi nec inafanya inavyotaka. Siku tutakayopata katiba mizigo hii yote itatua
 
Kuwa na katiba mpya is a long process. Rejea the case of Kenya. Binafsi nisingeunga mkono vyama kususia uchaguzi eti kwa sababu katiba haijakaa vizuri. Huwezi ukaleta mabadiliko ukiwa nje ya system. Mfano mzuri ni hivi sasa, chadema wameongeza wabunge na sauti ya wanyonge imeendelea kusikika zaidi. Kwa kufanya hivyo, umuhimu wa kuwa na katiba mpya utaongezeka.

Kiongozi Gosbertgoodluck,
Kususia uchaguzi na kumsusia Rais kipi kina nguvu kubwa?

Kumbuka kuwa wangesusia uchaguzi, hizi asilimia 58 za registered voters ambao hawajajitokeza kupiga kura zingehesabiwa kuwa ni za kwao plus zile zilizoharibika.
Ukisusia uchaguzi unaweza kuweka bayana zaidi tatizo lililopo na unaonekana hauko kimaslahi. Ukiingia kwenye uchaguzi na kuzikubali kanuni zote, halafu baada ya uchaguzi unazidenounce hizo kanuni, unaonekana uko kimaslahi.

Pia tukumbuke kuwa huu si uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi. Somo hili lilitakiwa kuwa limeshasomwa tangu awali na kutafutiwa ufumbuzi.
 
Kudai Katiba mpya ni muhimu hasa kutokana na vyama kujifunza kasoro nyingi zilizojitokeza katika uchaguzi, ambazo zimetokana na ubovu wa katiba. Ikumbukwe kuwa kipindi hiki kuwa tofauti na chaguzi zilizopita, kutokana na mwamko mkubwa wa watu hasa vijana, na wasomi wengi. Elimu ya uchaguzi inaendelea kuenea kwa watu, mazingira yanaonyesha miaka 5 ijayo itakuwa na tofauti kubwa tofauti na sasa. Bila katiba mpya amani ya nchi yetu hatarini. Ni hatari kutokana na udhaifu unaoonyeshwa na tume ya uchaguzi, mahakama, nk.

Kiongozi,
Uko sahihi kabisa kwenye hili.
Swali: Je, unaafikiana na hatua zinazofuatwa katika kuchochea mjadala wa katiba mpya?
 
Katiba yetu ilikuwa nzuri sana miaka ya 70' ambapo mfumo wa demokrasia ulikuwa still low na hata watu walikuwa hawana upeo wa kuhoji na kuweka wazi msimamo wao... lakini imezeeka na haifai kuendelea kutumika kwa sababu bado inafunga na inakinzana na mapinduzi ya demokrasia nchini Tanzania bado ipo kwenye miaka ya 70'.Kitu ambacho tunakihitaji sasa kutokana na wale tuliowaamini na kuwakabidhi madaraka wametumia nyadhifa zao vibaya...mfano katiba yetu hairuhusu uchunguzi wa matokeo baada ya NEC kuyatangaza,ibara ya 41 ibara ndogo ya 7,..jamani hii si njia ya kuuziba mdomo ukuaji wa demokrasia nchini?
Mimi naunga mkono katiba ibadilishwe thats 1 man down out of 44milion...so wanajamii tunaunga au tunapinga?
 
Katika nchi yetu muda umefika wa kuleta katiba mpya, hii ni baada ya ile iliyopo kutoridhisha wananchi. Kwa mabadiliko makubwa ya mfumo wa kisiasa na yale mengi tuliyojifunza kupitia chaguzi zetu tulizo fanya hakuna haja ya maandamano., watu wenye utashi wa kusoma nyakati wanatakiwa kujua kuwa huu ni muda muafaka wa katiba mpya.
Tumeona wenzetu Kenya wamepigana na wengine wamepoteza maisha kuleta mabadiliko haya yaliyopo sasa. Pia tumejifunza kutoka kwa wenzetu wanzanzibar baada ya kutoelewana kwa muda mrefu wameamua kurekebisha katiba ili kuendana na wakati. Katika Tanzania tumeona kuwa katiba imekuwa ni kikwazo kikubwa sana katika kuleta Dermokrasia ya kweli kitu ambacho kinaashilia Tanzania isiyosalama. Vyama mbali mbali vimeendelea kushiriki katika uchaguzi licha ya kujua kabisa kuwa kwa mfumo wa katiba tulionao ni kwamba wanashindwa kabla ya hata uchaguzi kufanyika.
Katiba safi ni msingi wa kuleta Demokrasia ya kweli, Katiba mpya ndio suluhu ya hali ya kisiasa tuliyonayo. Na ni ukweli uliowazi kuwa Kikwete atakumbukwa katika historia ya Tanzania endapo tu ataleta mabadiliko makubwa ya kikatiba ambayo yataepusha machafuko na kuleta Ustawi thabiti wa Demokrasia ya kweli. Hili linawezekana.
 
Wakuu kilio cha mabadiliko ya katiba kilianza miaka mingi iliyopita kabla ya mfumo wa siasa ya vyama vingi haujaruhusiwa rasmi.Mwaka huu 2010 chama kikuu cha upinzani CHADEMA kimeshika bango na inavyoonekana mabadiliko ya katiba ni ajenda kuu ya chama hicho.

Binafsi naona yapo makosa kulilia katiba mpya ilihali wananchi wengi hawajui mapungufu ya katiba ya sasa.Ningekuwa kiongozi wa CHADEMA ningeanza kuwaelimisha watanzania wa kawaida mapungufu ya katiba kabla ya kuanza mchakato wa kuomba mabadiliko ya katiba ndani ya bunge.

Wapiga kura wengi including walioichagua CHADEMA hawajui mapungufu ya katiba.Sijafanya utafiti lakini ni jambo lililo wazi wapiga kura wengi walikuwa wakililia huduma bora za afya,elimu bora,uboreshaji wa miundombinu,ajira kwa vijana na nk.CHADEMA wasipotoa elimu ya kutosha kwa wananchi wengi suala la mabadiliko ya katiba linaweza kuzimwa na CCM na likabaki bila mashiko.

Nianze kwa kuangalia baadhi ya maeneo ambayo ningependa katiba yetu iyaangalie.

Ningependa kuona katiba yetu inafanyiwa marekebisho yafuatayo.
[1] Madaraka ya rais wa JMT yanapunguzwa sana.Teuzi za mawaziri,Majaji,Wakuuu wa vyombo vya dola ulinzi na usalama,Mabalozi,Mwanasheria mkuu,Mkurugenzi wa Mashitaka na Makatibu wakuu wanathibitishwa na bunge.Ningependa nafasi kumi za rais kuteua wabunge zinafutwa mara moja.

[2]Jaji mkuu atokane na majaji wa mahakama ya rufaa na achaguliwe na majaji wa mahakama ya rufaa kama spika anavyochaguliwa na wabunge.

[3]Ofisi ya mkurugenzi wa mashitaka iwe huru zaidi,mamlaka ya nidhamu ya mkurugenzi wa mashitaka iwe ni bunge.

[4] Tume ya uchaguzi iwe huru[vyama vya siasa vishirikishwe kuunda tume].Mwenyekiti wa tume akishateuliwa na rais na kuthibitishwa na bunge asiwepo wa kumwandoa isipokuwa mahakama kwa makosa yaliyohainishwa wazi.Wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya wilaya wawe waajiriwa wa tume si wa haliamshauri kama ilivyo sasa.

[5] Wabunge wasiruhusiwe kuudumu zaidi ya vipindi vitatu.wastaafu serekalini wasiruhusiwe kugombea nafasi za ubunge wanapostaafu labda kama watajiondoa kwenye ajira kabla ya kufikisha umri wa miaka sitini.

[6] Nafasi za Wakuu wa mikoa na wilaya zifutwe mara moja.

[7] Kiwepo kipengele ambacho wapiga kura wanaweza kumwondoa mbunge wao wasiporidhika na utendaji wake badala ya kusubiri miaka mitano ipite.Wapika kura asilimia 50 wakisaini hati maalumu na kutoa sababu za msingi eg ahadi hewa.

[8] Rais lazima achaguliwe na wapiga kura waliojiandikisha kwa zaidi ya asilimia 50.

[9] TAKUKURU na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serekali wawajibike bungeni moja kwa moja bila kupitia kwa mawaziri eg utawala bota na wizara ya fedha.
 
Ningependa nafasi kumi za rais kuteua wabunge zinafutwa mara moja.

kaka, wananchi wetu wanaweza kuchagua wabunge mbumbumbu hawajafika hata darasa la saba itampa rais tabu kupata mawaziri.

Na kuna watu watendaji wazuri lakini sio wanasiasa rais anaweza kumteua mfano CEO fulani awe waziri wa Fedha kama anafaa na ubunge anapewa.
Mimi naona hizo nafasi bado za umuhimu.
 
Hapa siasa za bongo zinaendeshwa na pesa, tuna wasomi wangapi na vyuo vikuu vingapi vinatema wataalam wangapi kila mwaka? Kama una hela ya kuonga itabidi ukae nje tu, ndio maana vyama vya upinzani vina wasomi ambao mmoja anaweza akawa na uwezo wa wana ccm zaidi ya kumi.
Kingine, ccm bado ina wataalam lakini haitaki kuwatumia, matokeo yake inatumia wanajeshi wastaafu zamani walikuwa ni PEO (Political education officers)
 
Ningependa nafasi kumi za rais kuteua wabunge zinafutwa mara moja.

kaka, wananchi wetu wanaweza kuchagua wabunge mbumbumbu hawajafika hata darasa la saba itampa rais tabu kupata mawaziri.

Na kuna watu watendaji wazuri lakini sio wanasiasa rais anaweza kumteua mfano CEO fulani awe waziri wa Fedha kama anafaa na ubunge anapewa.
Mimi naona hizo nafasi bado za umuhimu.

Mkuu ningependa tuwe na mawaziri wasiokuwa wabunge.Mbunge akiteuliwa waziri anaacha mara moja kuwa mbunge.Mbunge anatakiwa kuwa mwakilishi wa wananchi waliomchagua.Ningefurahi Tanzania ingefuata mfumo wa Marekani.
 
Ningependa nafasi kumi za rais kuteua wabunge zinafutwa mara moja.

kaka, wananchi wetu wanaweza kuchagua wabunge mbumbumbu hawajafika hata darasa la saba itampa rais tabu kupata mawaziri.

Na kuna watu watendaji wazuri lakini sio wanasiasa rais anaweza kumteua mfano CEO fulani awe waziri wa Fedha kama anafaa na ubunge anapewa.
Mimi naona hizo nafasi bado za umuhimu.

Pia katiba iseme kuwa Mawaziri wasitokane na wabunge, kwani kitendo cha mkuchagua mbunge kuwa waziri atashindwa kuwahudumia wananchi waliomchagua inavyopasa badala yake atakuwa busy kufanya kazi za serikali
 
[9] TAKUKURU na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serekali wawajibike bungeni moja kwa moja bila kupitia kwa mawaziri eg utawala bota na wizara ya fedha.

Nakuunga mkono hapo namba 9
 
:angry: Boooshiiiittt yaani kweli Kunguru hafugiki na makazi ya mende ni ******,, yaani hawa CCM wanachakachua hadi madai ya msingi ya Wananchi,, hawa jamaa mi nasema we ngoja tu,, mi nitawashitaki kwa njia yeyote ile,, maana makosa wanafanya Kwasababu mahakama ni yao hawafungwiii,,, Katiba hwataki kubadilishaaa

yaani hawa CCM wanaona Watanzania wata faiiiidiii kukubali kubadili KATIBA yetu sasa mimi nasema we ngoja tu..

Hawa watu wamezidi kuzoea kuchakachua vitu hadi madai ya Katiba nayo "" yaani Bomba langi lilinasa hiyo Wakisema Katiba ikirekebishwa na kuwa na Favour nzuri kwa Tanzania Watanzania watafaidika na wao wataumia, kwa mtindo huo hawataki kubadili katiba"" Watachakachua madai haya mpaka tukomeeee
 
Akizungumza juzi jijini Mwanza katika ziara yake ya siku moja Waziri huyo Mkuu wa Kenya alisema katiba ni hitaji la wananchi na iwapo wameanza kudai basi hakuna budi kuangaliwa kwa vile katiba ndiyo huchochea ustawi wa nchi.

"Tanzania haitakwepa kuwa na mabadiliko ya katiba iwapo wananchi watataka" alisema.

Raila alibainisha kuwa katiba nyingi za Afrika ikiwepo ya Kenya ambayo ilibadilishwa hivi karibuni zilipitwa na wakati kwa sababu ni za zamani na nyingi zimerithi mapokeo ya kikoloni.

Hata hivyo baadhi ya nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ikiwemo Kenya zimefanya mabadiliko ya katiba na nyingine ziko kwenye mchakato kubadilisha.
 
You people need to know that there is no way Kenya can dictate or even suggest what we ought to do. Hawa watu wanataka tuanze chezea katiba tuweke na provision on ownership of land nini! Not being paranoid but you have to agree that Kenya does not act in the interests of Tanzania so Raila can Shut the F..up. Kwanini wasianze na Uganda ambako Ikulu ni nymba ya familia ya Museveni.
 
Back
Top Bottom