Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Mi mwenyewe niko mpakani hiyo asilimia 60 unayoisema umeipata wapi? Tz ni nchi huru ya kidemokrasia yenye Katiba na utawala,ukitaka kujitenga nenda kawaulize Bokoharam waambie wakupe eneo huko!!

Mbona kwa Boko haram ni mbali saana......hapahapa jirani Kenya.anagalia hiyo 60% nilivyoipata...Wadigo wapo Kenya na TZ...WAKURYA wako kote....Wamasai kote....Wasomali kote....Wajaluo kote....Wahaya....kote upande wa Uganda...Wachagga....usiseme nusu ya Mombasa ni wachagga .
 
Sasa nimeelewa ni mtu gani naongea nae nilikua nahangaika bure sasa nimeshakujua muhaini mkubwa wewe!na usanii wako!huna nafasi katika taifa hili na huna tofauti na Idd Amin aliyepokea malipo ya uzandiki,unafiki na upoyoyo wake,watu jamii ya Idd Amin wanaotamani kugawa watu kwa misingi ya kabila na maeneo hawapaswi kusikilizwa hata kidogo tokaaaaaaaa����
 
Huu mchakato upo na tuna kamati ya vijana wapiganaji tunakutana tena next Monday then tutaandaa press conference kuwaeleza waandishi wa habari nia yetu na jinsi tutakavyoifanikisha.

Ni wazo chanya....lakini bado nina wasiwasi kama mtakubaliwa.Hebu angalia walioteuliwa kutoa elimu kwenye TV pamoja na kushiriki kwenye Bunge la katiba,mafunzo yao ni kwamba katiba imesheheni vitu vingi na imetaja makundi yote...ki vipi....hawatuelezi na itafanyaje kazi hawatuelezi.
Mukikubaliwa munaweza kuondoa huu mpasuko uliopo sasa hivi.
 
Teh te he teh mnajifanya wajanja eti mnataka kuwatumia waandishi wa habari kupitishia urojo wenu thubutu media sio kichwa cha mwendawazimu mmekosea njia!!! Na mtakua mmetumwa nyie sio bure!!!! Ha ha ha siku ya kufa nyani miti yote inateleza mwisho wenu umefika!!!mtawapata makanjanja tu na watakula hela zenu mpaka mfe!!!
 
Ha ha ha ha rudi kwenye lugha ya nyumbani tu maana naona unachanganya madesa!Tanzania imejengwa kwenye misingi imara,usilolijua wewe ni nafasi yako katika kuendelea kufanikisha mafanikio yaliyopo!jipange sawasawa kupokea mabadiliko ya nchi yako,usipaniki na kukata tamaa!

If the country was built on the sound foundations, why do you demand a new constitution?
 
hacha kulilia mabadiliko huku umelala nyumbani jitokeze

Naamini wewe hujalala nyumbani na wala hujalala kwenye suala nyeti la mustakabali wa taifa letu. Sasa hebu jitokeze simama imara mbele ya watu jiandikishe ili uwe miongoni mwa Watanzania watakao ipa nchi yao viongozi wa kuiongoza 2015 hadi 2020 na Katiba Mpya. Mungu Ibariki Taznzania kwenye matukio haya mawili nyeti na muhimu kwa taifa letu.
 
Katiba mpyaa iwee na kipengelee kinacho sema. Raisi ahukumiwe kama aja timizaa asilimia kadhaa ya vitu alivo ahidi kwa wananchi
 
Kwa kweli wenzetu waliofanikiwa kushinikiza kuwepo kwa katiba muafaka wako na nafuu kubwa. Wao kama wananchi wayatakayo yanakuwa na serikali zao zinawajibika kwao. Ununda uliokuwapo unaelekea kuwa historia.

Kwa wenzetu katiba zinawalazimisha Polisi kuwa walinzi wa umma. Polisi anawajibika kulinda waandamanaji. Polisi anakuwa vetted na wananchi. Asiye faa anatupwa pembeni.

Mahakama zao zawajibika kwa wananchi -- hizi zetu zinazoongelea dhamana (si kesi) wakati uko ndani kwa siku lukuki zinatia mashaka. Tukimbilie wapi siye? Haiyumkiniki ni katika kudai katiba mpya yenye kutuweka sote sawa mbele za haki.

Yawezekana hawajafika wanako tarajia kufika lakini wako na nafuu na wanapiga hatua mbele. Tujifunze kwa wenzetu. Maana mazingira yao na yetu hayako na tofauti kubwa hali wenzetu angalau wana sauti za kusemea. Sisi Je?

Source: Dismissal of 127 officers hits traffic police hard
 
Katiba mpya ni nzuri ikiwa KILA UPANDE hautaiangalia katiba kwa maslahi yake KICHAMA. Bali maslahi ya NCHI na WATANZANIA na VIZAZI vijavyo.

Kama kuna MAPUNGUFU humo ndani yajadiliwe, YAREKEBISHWE na Katiba IPATIKANE. Maana katiba hii si ya MAGUFULI, LOWASSA, CCM ama CHADEMA ni ya Watanzania WOTE wanaotaka KUJIKWAMUA kutokana na UMASKINI na KUSAIDIWA KUFIKIRI.

Ili hatimaye WAFIKIRI wao wenyewe ni nini wanachokihitaji na ni wapi!
Bila Katiba mpya maendeleo Tanzania itakuwa ni NDOTO.
Maana Tanzania ni kubwa mno.
Na huwezi kutimiza mahitaji ya maendeleo ya nchi toka Dar.
Ni lazima yawakaribie wananchi!
 
Katika hii verdict iliyotolewa na Mahakama ya juu huko Kenya kutengua ushindi wa Uhuru kufuatia magumashi kwenye uchaguzi tofauti na maoni ya wengi ambao wanahimiza mahakama hasa yetu ambayo imekua ikilalamikiwa kupendelea upande mmoja kufata nyayo

Mimi naona katiba mpya ndio itakua mkombozi maana utamwona kila mara yule supreme judge ana defends katiba.

Nawasilisha
 
Tunahitaji katiba mpya iseme nini ambacho hakijasemwa katika katiba iliyopo?

Kama ni uhuru wa mahakama katiba iliyopo sasa imeweka wazi kabisa mahakama zitakuwa huru..

Tume ya uchaguzi? Katiba iliyopo sasa imeweka wazi kabisa kwamba tume ya uchaguzi itakuwa huru..

Sidhani kama tatizo ni katiba..

Sijasahau pia tulikwenda katika bunge la katiba badala ya kupigania mambo ya muhimu tukaenda kugombania madaraka(serikali tatu)
 
Katiba mpya haiwezi kupatikana kama ccm hawajaamua...na Kenya katiba mpya imewezekana baada ya damu kumwagika damu na Tanzania bila kung'ata meno hakuna katiba mpya...hivi ccm Ni wapumbavu kiasi gani waruhusu katiba itakayomnyang'anya mwwnyekiti wao uwezo kuchagua mwekiti tume ya uchaguzi?hivi ccm Ni wwndawazimu kwa kiasi gani jadi waruhusu katiba mpya itakayozuia matokeo kupingwa mahakamani?hivi ccm Ni wendawazimu kiasi gani hadi waruhusu katiba mpya itakayo mdhibiti msajili WA vyama vya siasa?hivi ccm Ni wapuuzi kiasi gani waruhusu katiba itakayomzuia rais asijichagulie jaji mkuu? Hayo Ni maswali mepesi mnapaswa kujiuliza ukiona Kuna uwezekano basi katiba tutapata bila shida...bila ngumi katiba hakuna..na tusitegemee uhuru WA mahakama kwa majaji watakaoteuliwa na mwwnyekiti WA ccm
 
Tunahitaji katiba mpya iseme nini ambacho hakijasemwa katika katiba iliyopo?

Kama ni uhuru wa mahakama katiba iliyopo sasa imeweka wazi kabisa mahakama zitakuwa huru..

Tume ya uchaguzi? Katiba iliyopo sasa imeweka wazi kabisa kwamba tume ya uchaguzi itakuwa huru..

Sidhani kama tatizo ni katiba..

Sijasahau pia tulikwenda katika bunge la katiba badala ya kupigania mambo ya muhimu tukaenda kugombania madaraka(serikali tatu)

Umesahau madaraka ya kimungu ya Raisi katiaba ya sasa rais ndio alfa na omega

Leo tumepata pombe anavunja iatakavyo siku tunampata mbaya zaid ndio utajua
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom