Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Mi nafikiri Hawa jamaa wanalijua hilo la katiba mpya lipo midomoni mwa Watanzania sasa, Na ndio maana wamemuweka Speaker mwenye kiburi cha kuzqliwa yule Anne Makinda,, Ili mtu yeyote akianzisha suala la Katiba aliziue na kuwaambia wabunge kuacha kabisa mjadala wa Katiba,,, Hii ndio maana yao..
 
Tazameni Katiba Inavyo sema jamani Tusiwe Waoga Tukaze boot,,

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, Sura ya 2 ya Sheria za Tanzania imeweka ‘Malengo Muhimu na Misingi ya Mwelekeo wa Shughuli za Serikali’ kuwa ni pamoja na mambo yafuatayo:[1]
  • Kwamba “wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi….”;
  • Kwamba “lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi”; na
  • Kwamba “Serikali itawajibika kwa wananchi….”
  • ….”
kwa mtindo huo Wananchi tunahaki ya kuiwajibisha na kuwapa kazi ya kufanya,, kwasababu wao wapo kwaajiri yetu sisi na kututumikia sisi
 
Tunataka Katiba mpyaaaaaa,, Ng'hili naombA UWAPE VIDONGE WASIO TAKA KATIBA IBADILISHWE,, tunataka katiba mpyJmNI
 
Wachakachue matokeo ............. shauri yao.

Sijui Membe/Rostam/Pinda/Maguguli/Prof.Tibaijuka/Masai waziri mkuu.....haituhusu.

Sijui Anna Makinda Spika............inanghu???

Sijui Sheikh yahaya kasema upupu.....to hell!!

What we need is and only this:

Katiba Mpya!!!!
 
asanteni wadau kwa hoja. its high time tuje na well researched and reasoned papaer that expalains in a simple lg kwanini tunahitaji katiba mpya.
sababu zaweza kua
1.katika iliyopo haikutungwa na wananchi wa tanzania bali kamati ya watu 11 ikiongozwa na pius msekwa asiye mwanasheria wala hana mafunzo yoyote ya haki za biandamu.
2.inatambua tz kama nchi ya kijamaa na wakati huu sio ukweli!
3.inampa raisi madaraka makubwa sanaaaaaaaaaaa,eg.kuanzaisha na kufunga ofisi yoyote.
endeleeni na nyingine.
baada ya paper CHADEMA,VYAMA VYA KILAIA,TAASISI YA HAKI ZA BIANDAMU,NA WAPENDA MAENDELEO AKA WANAHARAKATI WOTEEEEEEEEEEE TUPANGE KUSAINISHA WATU MILION KUMI(IZIDI WAPIGA KULA) NA TUILAZIMISHE SERIKAKI YA CCM,
 
siongelei amani ya Nchi naongelea Amani ya kuto kujua hatma yao miaka ya mbele,

Naomba Watanzania tujiunge kupigania KATIBA MPYA
 
Kwanini unataka katiba mpya? ?

Huwezi kuvua nguo yote kama inakustiri maungo. Badala yake unarekebisha kwa kuweka kiraka palipo chanika
 
hilo la mabadiliko ya katiba ndiyo jibu la matatizo yetu ya uchaguzi. Hongera kwa wazo hilo la kuanzisha vuguvugu ili kesho kama tunarudia kumchagua dr. Slaa, tunajua tuko salama vinginevyo tutakuwa tunafanya biashara ya kubeba maji kwa gunia

na kifungu cha kwanza kubadilishwa iwe "kushiriki upigaji kura ni lazima kwa kila mtanzania ,mtanzania yoyote asieshiriki katika kupiga kura ni kosa na adhabu ya kufungo ama faini ya tshs:500,000.00."

tukiachia watu wachache watuchagulie kuna siku tutapata hitler na ndio tumenoa.....wengi wasio piga kura ni watu wenye uwezo wa kuchagua lakini hawaoni umuhimu wa kuchagua kwani wengi wanamawazo ya kwamba aah nikenda nisende ccm itachaguliwa
 
Wazalendo:

Kuhusiana na mabadiliko ya katiba kuna njia nyingi tu za kubadili katiba. Njia ya kwanza ni kutumia wabunge. Njia ya pili kufungua kesi mahakamani kuonyesha kuwa katiba ya sasa inavunja haki zako za kiraia na kibinadamu. Tanzania imetia saini mikataba mingi ya kimataifa kuhusiana na haki za binadamu.

Kwa mfano: Universal Declaration of Human Rights Article 21 inasema:

(1) Everyone has the right to take part in the government of his country, directly or through freely chosen representatives.
(2) Everyone has the right of equal access to public service in his country.
(3) The will of the people shall be the basis of the authority of government; this will shall be expressed in periodic and genuine elections which shall be by universal and equal suffrage and shall be held by secret vote or by equivalent free voting procedures.

Article hii inaonyesha kabisa kuzuia mtu asiye mwanachama kugombea nafasi ya uongozi ni makosa.
 
Wana jamii wenzangu....
Kilio cha samaki.....kweli tunakubali kuendeshwa na ububu na ukiziwi wa watu wachache hawa???
1.tulilie katiba ibadilishwe....kampeni nchi nzima tuianzishe kweli na kwa haki nguvu zote kudai haki yetu

2.tupunguze na kulaani matumizi yasiyo ya lazima ya pesa zetu walipa kodi..wabunge viti maalumu hawana maana sana...mzigo mkubwa sana sana kwa taifa na walipa kodi.(inaniuma sana walivyojazana hawana cha maana wanachokifanya..wabakie wabunge wa majimbo tuu)

3.anasa na magari ya kifahari....hatutaki kabisa.

4.80% ya waziri wakuu wastaafu ifutwe..walipwe mara moja yaishe...mzigo unazidi kuwa mkubwa sana.....wako 7 sasa ukiacha marais wastaafu bara na visiwani...inatosha sasa.

5.mishahara ya wabunge na ma posho mara 2 kila kamati wanalipana mara mbili mbili....mzigo kwa walipa kodi.(ubunge uwe ni kazi ya hiari na kujitolea walipwe posho za kujikimu au mishahara ya kawaida yenye kukatwa kodi)...

6.hakuna kurundikiana vyeo vingi mtu mmoja...mkuu mkoa,mbunge,mjumbe wa bodi etc.

7.............wenzangu tujiandae kwa hayo na mengine..taifa lina mzigo mkubwa sana kwa sasa na usio wa lazima kabisa.....pamoja tutaweza na kushinda...
 
katiba ni dira ama ramani inayotumiwa na nchi kuongoza watu wake kwa kufuata sheria,taratibu,mwongozo, kanuni zilizowekwa. nasikitika kusema kuwa tanzania imekoswa muongozo sahihi (katiba) hivyo nchi kuendeshwa na kundi dogo kulingana na wanavyo taka. kundi hili hutawala wanavyo taka bila hofu kwa kujua makusudi nchi ina mapungufu makubwa, wasafiri (wananchi) waliomo hawana ramani wala dira hawajui waendako, pamoja na hayo bado walio na dhamana ya kuongoza hawataki kushtuka kwamba abiria sasa wanafahamu kuwa wamepotezwa njia na wanaitaji mambo mawili; kwanza, dira au ramani sahihi ioneshayo waendako itolewe na isahihishwe maana tulishapotea; pili, safari ifuate mwongozo huo.

katiba ndio nguzo pekee itakayo saidia kutufikisha huko tunapo pafikiria kama sio sisi basi watoto wetu, nchi yoyote inapo kosa katiba madhubuti basi inakuwa vulnarable, tanzania tunaendelea kunyemelea hatari nyingi kama bado hatuta washurutisha viongozi wetu kufanya mabadiliko haraka ya katiba tena tusichelewe zaidi maana, viongozi wetu watatupa wakati mgumu sana kuirudisha nchi katika dira sahihi endapo hatutaungana kupinga udhalimu, wanaoutenda kwa wananchi ambao wengi wao bado hawajui wanapelekwa kwenye hatari ya kufa huku wakiimba nyimbo za viburudisho na mipasho. kweli inatia huruma na hasira kwa mtu aliye kwisha soma alama za nyakati.

ukweli tanzania haina amani tanzania haina utulivu, iko wapi amani kwa mtu mwenye njaa? ipo wapi amani kwa mwananchi aliyekosa mahali pa kupumzika? upo wapi utulivu kwa mtu aliyekosa tiba? je mwenye kiu ana furaha? la hasha! hivi ni vilio vya wanyonge walio kata tamaa wanasubiri shujaa kutoa sauti ya matumaini angalau kwamaba wataishi kwa masaa mengine yajayo kabla ushindi haujatangazwa.
 
Ndugu zangu,

Wakati tukiendelea kufatilia "mtanange" wa kisiasa wa Tanzania, naomba tujadili swala ambalo limetokea kuwavutia wengi: katiba mpya.

Swala la katiba mpya limekuwa ndio gumzo hivi sasa. Hata viongozi wa vyama vya siasa wamesikika wakitoa kauli kuwa katiba mpya ndio ufumbuzi wa matatizo ya nchi yetu.

Hata hivyo, kinachonishtua ni kwamba swala hili limetawala mazungumzo ya kisiasa nchini baada ya uchaguzi, ambao umekirudisha Chama Cha Mapindizi madarakani. Imeelezwa (na viongozi wa kisiasa na wanaharakati) kuwa mfumo uliopo unafanya zoezi la kukitoa chama hicho madarakani kuwa ni "ndoto za alinacha".

hoja zilizotolewa zinaweza kuwa na uzito, lakini zinaacha maswali yanayohitaji kujibiwa:
1. Je, tatizo la katiba ni jipya Tanzania? Kama si jipya nini kilifanywa na wanaolitambua tatizo hili, katika miaka 5 iliyopita, ili kulitatua? Itakumbukwa kuwa kipindi hiki Bunge liliweza kufanya mambo makubwa kama kumshinikiza waziri mkuu kujiudhuru baada ya hoja nzito za ufisadi ambazo zililetwa na wabunge ambao wangeweza kuleta hoja ya katiba kwa minajili hiyohiyo.
2. Wakati wagombea wanachukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali hawakuliona hili? kwa nini walikubali kushiriki uchaguzi ambao hauwapi nafasi sawa? Na kwanini walitoa kauli kuwa wanaingia kwenye uchaguzi kushinda? - kauli hizi zinakinzana na kauli za sasa kuwa mazingira hayawaruhusu kushinda.

Karibuni tujadili.
 
Kuwa na katiba mpya is a long process. Rejea the case of Kenya. Binafsi nisingeunga mkono vyama kususia uchaguzi eti kwa sababu katiba haijakaa vizuri. Huwezi ukaleta mabadiliko ukiwa nje ya system. Mfano mzuri ni hivi sasa, chadema wameongeza wabunge na sauti ya wanyonge imeendelea kusikika zaidi. Kwa kufanya hivyo, umuhimu wa kuwa na katiba mpya utaongezeka.
 
Kudai Katiba mpya ni muhimu hasa kutokana na vyama kujifunza kasoro nyingi zilizojitokeza katika uchaguzi, ambazo zimetokana na ubovu wa katiba. Ikumbukwe kuwa kipindi hiki kuwa tofauti na chaguzi zilizopita, kutokana na mwamko mkubwa wa watu hasa vijana, na wasomi wengi. Elimu ya uchaguzi inaendelea kuenea kwa watu, mazingira yanaonyesha miaka 5 ijayo itakuwa na tofauti kubwa tofauti na sasa. Bila katiba mpya amani ya nchi yetu hatarini. Ni hatari kutokana na udhaifu unaoonyeshwa na tume ya uchaguzi, mahakama, nk.
 
Tuna safari ndefu watanzania Wenzangu ya mabadiliko ktk nchi hii. Unapoona tabaka lililoko madaraka inajinufaisha yenyewe kwa rasilimali zetu na kupeana madaraka kwa kutegemea uswahiba usifiki kitu kingine zaidi ya KATIBA gandamizi tulilonalo. Katiba ndiyo matokeo ya yote hayo yanayoendelea rais kuwa na madaraka kupindukia na kufanya atakalo.

Ni wakati wetu kuanza kudai katiba mpya,inasemekana Tanzania ni nchi pekee katika EAST Africa iliyobaki na katiba iliyotungwa na wakoloni ambayo iliandaliwa kwa mujibu wa kuilinda chama kimoja tu cha siasa.

Tunahitaji katiba mpya kuliko kitu kingine chochote.
 
Back
Top Bottom