New Movement: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo


Zakumi

Zakumi

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2008
Messages
4,841
Likes
374
Points
180
Zakumi

Zakumi

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2008
4,841 374 180
Amani kwenu wazalendo wenzangu:

Baada ya salaam ningependa kusema kuwa uchaguzi uliopita una mapungufu makubwa sana. Mapungufu mengi ni ya masuala ya kikatiba ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu kuanzia uchaguzi wa 1995. Mapungufu hayo hayakujionyesha sana katika vipindi vya uchaguzi vilivyopita kwa sababu wagombea wa chama tawala walikuwa hawana upinzani mkubwa. Hivyo kasoro zote za kikatiba zilifunikwa na umaarufu wa kihistoria wa CCM. Kwa kipindi cha uchaguzi cha 2015, Tanzania itakaribisha wapiga kura wapya wapatao 1.5 miloni au waliozaliwa mwaka 1995 na baadaye.

Hatutajitendea haki wenyewe na kizazi kipya iwapo tutaendelea kutumia katiba iliyo sasa kama mwongozo wa kuendeleza nchi. Hivyo kwa maombi yangu binafsi, wazalendo wa Tanzania tuanze kusukuma mabadiliko ya kikatiba. Ninapoita wazalendo, nina maana wananchi bila kujali itikadi zao vyama vya kisiasa, dini au ukabila.

Bila ya kutaja matatizo ya katiba yetu, ningependa kueleza toka tumepata uhuru katiba ya Tanzania imekuwa ni kitu kisichoeleweka wazi kwa wananchi. Tuliosoma shule wakati somo la siasa linafundishwa mashuleni, tulikuwa tunafundishwa katiba ya CCM na miongozi ya chama hicho. Hivyo basi kuna uwezekano mkubwa hata wanasiasa wetu wengi hawajui umuhimu wa kitabu hicho.

Hivyo ningependa kufungua ukumbi kwa kuwakaribisha wenye mawazo na nia ya kubadilisha katiba kutoa mawazo yao.

Na vilevile kama kutakuwa na watu wanaotaka kuanzisha jumuia ya kufanya mabadiliko ya kikatiba, naomba mjitokeze.
 
Alphonce Kagezi

Alphonce Kagezi

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2015
Messages
261
Likes
97
Points
45
Alphonce Kagezi

Alphonce Kagezi

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2015
261 97 45
Mchakato wa Kikatiba mda fulani umelipa hasara ya billion ya fedha na ukaachwa hewani bila kukamilika,kwa kuwa Selikali ya awamu ya tano kipaumbere chake sio Katiba mpya ,mijadala mazungumzo ya Katiba mpya inaweza kuwepo kwa sehemu mijadala isilete confilct na vipaumbere vya selekali ,inaweza kuendelea taratibu na mda ukifika ikapelekwa bungeni na ikajengewa hoja then Bunge likiona umhimu litashauri Selikali ilete hoja lasmi kuhusu Katiba mpya

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Forum statistics

Threads 1,250,076
Members 481,223
Posts 29,719,979