New Movement: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo


Zakumi

Zakumi

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2008
Messages
4,820
Likes
336
Points
180
Zakumi

Zakumi

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2008
4,820 336 180
Amani kwenu wazalendo wenzangu:

Baada ya salaam ningependa kusema kuwa uchaguzi uliopita una mapungufu makubwa sana. Mapungufu mengi ni ya masuala ya kikatiba ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu kuanzia uchaguzi wa 1995. Mapungufu hayo hayakujionyesha sana katika vipindi vya uchaguzi vilivyopita kwa sababu wagombea wa chama tawala walikuwa hawana upinzani mkubwa. Hivyo kasoro zote za kikatiba zilifunikwa na umaarufu wa kihistoria wa CCM. Kwa kipindi cha uchaguzi cha 2015, Tanzania itakaribisha wapiga kura wapya wapatao 1.5 miloni au waliozaliwa mwaka 1995 na baadaye.

Hatutajitendea haki wenyewe na kizazi kipya iwapo tutaendelea kutumia katiba iliyo sasa kama mwongozo wa kuendeleza nchi. Hivyo kwa maombi yangu binafsi, wazalendo wa Tanzania tuanze kusukuma mabadiliko ya kikatiba. Ninapoita wazalendo, nina maana wananchi bila kujali itikadi zao vyama vya kisiasa, dini au ukabila.

Bila ya kutaja matatizo ya katiba yetu, ningependa kueleza toka tumepata uhuru katiba ya Tanzania imekuwa ni kitu kisichoeleweka wazi kwa wananchi. Tuliosoma shule wakati somo la siasa linafundishwa mashuleni, tulikuwa tunafundishwa katiba ya CCM na miongozi ya chama hicho. Hivyo basi kuna uwezekano mkubwa hata wanasiasa wetu wengi hawajui umuhimu wa kitabu hicho.

Hivyo ningependa kufungua ukumbi kwa kuwakaribisha wenye mawazo na nia ya kubadilisha katiba kutoa mawazo yao.

Na vilevile kama kutakuwa na watu wanaotaka kuanzisha jumuia ya kufanya mabadiliko ya kikatiba, naomba mjitokeze.
 
technically

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Messages
7,268
Likes
17,792
Points
280
technically

technically

JF-Expert Member
Joined Jul 3, 2016
7,268 17,792 280
Duuh,una elimu Gani kama unaipima katiba katka kipengele kimoja cha cha uchaguzi huru na haki tuu?VP uwepo wa serikali tatu,nguvu ya wananchi kuwajibisha viongozi,kupunguzwa kwa madaraka ya mkuu wa nchi,nk
Na ndipo ilipo tageti ya wanasiasa wa upinzani wao wanafikiria wakipata katiba itawapeleka Ikulu ..

sawa katiba ina vitu vingi lakini hatuwezi kuficha ukweli inaangaliwa kwa umakini kwenye mgawanyo wa madaraka na uchaguzi

hatuwezi kuepuka ilo.
 
mnengene

mnengene

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2011
Messages
1,180
Likes
747
Points
280
mnengene

mnengene

JF-Expert Member
Joined Nov 21, 2011
1,180 747 280
Na ndipo ilipo tageti ya wanasiasa wa upinzani wao wanafikiria wakipata katiba itawapeleka Ikulu ..

sawa katiba ina vitu vingi lakini hatuwezi kuficha ukweli inaangaliwa kwa umakini kwenye mgawanyo wa madaraka na uchaguzi

hatuwezi kuepuka ilo.
Acha ulimbukeni wewe Katiba nzuri ya nchi ni nyenzo muhimu Sana ya kuendesha nchi Kwa utaratibu unaofaa.
Ndio tatizo la wanasiasa wapumbavu na wapuudhi kama wewe, katiba ni Mali ya wananchi wote na sio wanasiasa tu kwamba eti wanasiasa wa upinzani wataenda ikulu.
Una akili fupi Sana we kima utafikiria na wewe upo kwenye list ya dudu baya.
Katiba tuliyonayo ni ya hovyo sana na imepitwa na wakati.
Ukitaka kujua hilo rejea rasimu ya tume ya warioba.
Wewe lazima utakuwa huna marinda
 
B

Buffet

Senior Member
Joined
Aug 11, 2018
Messages
142
Likes
243
Points
60
B

Buffet

Senior Member
Joined Aug 11, 2018
142 243 60
Tufike sehemu tuwe wakweli kwa serikali za kiafrika hata tuwe na katiba nzuri kiasi gani sio suluhisho la matatizo yetu hasa kuna watu wanasema .

Tukipata katiba tutaweza kuwa na uchaguzi ulio huru thubutu hakuna kitu kama hicho na hakitakaa kitoke

Matatizo ya uchaguzi ni busara za vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi na utashi wa viongozi waliopo madarakani

Kama mnabisha angalia uchaguzi wa mwaka 2017 nchini kenya Mpaka kijana mmoja mzalendo wa tume ya uchaguzi IEBC alikatwa kiganja ili tu Uhuru Kenyatta aendelee kuwa madarakani

Kenya ndio nchi yenye katiba bora kuliko nchi zote barani africa lakini kilichotokea mwaka 2017 ilikuwa ni ubakaji wa democrasia waziwazi.

angalia Marekani mwaka 2016 Trump alizidiwa popular votes million 3 lakini mpaka sasa eti yupo ikulu sijui anawakilisha wananchi wapi upuuzi mtupu.

tufike sehemu tuwe wakweli hata kama tungetengeneza katiba ya namna gani kama hakuna utashi wa watawala na watu wa usalama kama police na jeshi hawajaamua kuwa wazalendo na kuacha kutumikishwa na wao kuwa na wagombea hasa africa tutaendelea kupiga kelele mpaka kiama ..

Hivi unategemea mtu kama Magufuli akupe katiba mpya halafu akuruhusu kwenda IKULU?
nani kasema anataka katiba mpya ili ituletee maji na barabara??kuna mtu kasema anahtaji katiba mpya ili iboreshe huduma za kijamii??ni wapi ulisikia mtu anadai katiba mpya ili itujengee viwanda??? constitution is the body which governs the state,tunahtaji katiba ambayo itaweka mifumo na misingi ili rais atakayepatikana awe kichaa au timamu misingi ndyo im'shape
 
J

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Messages
14,399
Likes
8,792
Points
280
J

JokaKuu

Platinum Member
Joined Jul 31, 2006
14,399 8,792 280
..Ghana wana demokrasia madhubuti.

..Wanabadilisha serekali bila matatizo.

..Tujitahidi tuwakaribie na hata kuwazidi.

..Ninaamini Mwalimu aliposema tunahitaji siasa safi ili tuendelee, ktk mazingira ya sasa hivi siasa safi zinategemea katiba bora na utawala wa demokrasia.

..Tukiondokana na mikwaruzano ya demokrasia tutapata muda mwingi zaidi wa kujielekeza kwenye maendeleo.
 
WILE

WILE

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2009
Messages
3,110
Likes
2,058
Points
280
WILE

WILE

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2009
3,110 2,058 280
Na swali moja tu. Alichofanya Jecha alifuata katiba au hakufuata katiba? Baada ya hapo urudi uniambie umuhimu wa kubadilisha katiba kwenye Jamii ambayo haifuati wala kuitetea hiyo katiba inapovunjwa.
 
Mathias Raymond Nyakapala

Mathias Raymond Nyakapala

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Messages
1,823
Likes
1,104
Points
280
Age
30
Mathias Raymond Nyakapala

Mathias Raymond Nyakapala

JF-Expert Member
Joined Mar 1, 2017
1,823 1,104 280
Haki haiombwi ni lazima......HUDAIWA
 
Nadu

Nadu

Senior Member
Joined
Jul 19, 2018
Messages
154
Likes
110
Points
60
Nadu

Nadu

Senior Member
Joined Jul 19, 2018
154 110 60
Hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu.hata hiyo iliyopo imeamriwa kutoka juu.
Mamlaka zinatoka kwa Mungu lakini applications za mamlaka zaweza kuingiliwa na mashetani. Mfano ni Nebuchadnezzar, Hitler na IDD Amin Dada

Hata iliyoko yaweza kuingiliwa
 
C

Chesty

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2009
Messages
3,532
Likes
970
Points
280
C

Chesty

JF-Expert Member
Joined Aug 30, 2009
3,532 970 280
Mamlaka zinatoka kwa Mungu lakini applications za mamlaka zaweza kuingiliwa na mashetani. Mfano ni Nebuchadnezzar, Hitler na IDD Amin Dada

Hata iliyoko yaweza kuingiliwa
Hili andiko wengi huwa wanalichukulia literally. Ile mamlaka ya utawala ni Mungu ameiweka na anakuwa anaweka vipawa kwa watu fulani ili waongoze nchi kwa mafanikio.

Kinachotokea ni kuwa watu wengi wanaotaka kutawala wanakwenda kwa waganga na wasoma nyota ambao wamewezeshwa na shetani kutambua vipawa vilivyomo ndani ya watu (nyota).

Ndipo mganga anapoyatuma mashetani kuiba vipawa na kuwawekea watu wanaowaendea. Hayo yanahusisha mikataba ya kuua watu, watoto na mambo yanayofanana na hayo.

Kimsingi watawala hao wanakuwa wanatembelea nyota za watu. Ndio maana ya andiko linalosema shetani ni mwizi, anaiba vitu vya rohoni.
 
K

Kiwete

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2010
Messages
686
Likes
614
Points
180
K

Kiwete

JF-Expert Member
Joined Dec 18, 2010
686 614 180
Mkuu,labda uongezee hapa:
-Nyie ni akina nani na mko wapi(if you dont mind)!
-Bila shaka ni inputs nyingi zinahitajika, mngeacha milango wazi kwa wengine kuleta hizo inputs.
Hilo swali usijibuuuu
 

Forum statistics

Threads 1,238,884
Members 476,223
Posts 29,335,553