Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Watanzania tulikuwa tumepata nafasi pekee ya kumpata kiongozi ambaye anegtupatia katiba ya kisasa sambamba na matakwa ya millenium hii. Unfortunately majambazi wametuharibia bahati yetu hiyo na kuturudisha kwenye ujima. Nashindwa kuwaelewa watu wanaosema President wa watu Slaa akubaliane na ujambazi huo. Ningemshauri anyamze kwa kipindi lakini akumbuke kuwa watanzania wengi wanahitaji uongozi wake kuliko kipindi chochote katika 15 iliyopita; watu wanataka uhuru wao halisi wakilindwa na Katiba yao, siyo huu wa bandia ambapo katiba inawalinda wakubwa tu. Slaa asikubaliane na hiyo dhana potofu kuwa akubali matokeo ya uonevu eti kwa faida ya amani. "Those who sacrifice liberty for security deserve neither!!!"

Kichuguu,

Kwani CCM ilikuwa haijulikani ni majambazi kabla ya kuingia kwenye uchaguzi?? wameanza kuiba kura tangu tunapiga zile za mtu na kivuli!!!!!!

Slaa hatkiwi kwenda IKULU ndio abadili katiba, tunataka katiba ibadilishwe sasa kabla ya mtu yeyote kwenda ikulu! akifika pale atabadilika, kwani ni binadamu tu! katiba inamlinda kiongozi kutotumia hulka za binadamu kuamua! Slaa was never a saint and was not qualified for that.

Kama aliweza kuacha upadre, akaondoka CCM, na kutembea na mke wa mtu inaonyesha kabisa ni BINADAMU KAMILI MWENYE KUHITAJI SHERIA ZA KUMLINDA!!!!!

Tell him to fight for constitutional change starting from today, and see if he will dare to say that!!!
 
This is so Critical na Kama Hawataki Kuzungumzia Mabadiliko ya Katiba, Tuingieni Polini na Kampani za Kuwapata Wanajeshi Wengi na Polisi Kusaini ili Tuwaondoe kwa Nguvu. Hawa CCM Wanaona Hii Katiba Inawalinda Watanzania au Wao na Familia Zao? Matatizo Kwenye Uchaguzi, Rushwa, Freesom of Speech na Kila Jambo Linalomshusu Mtanzania Linazuiwa na Katiba Hii. Sijui Warioba na Wengine Wanajiita Wanasheria Hapo Tanzania Wanakaa Nyumbani Wakifurahia Hii Hali ya Maisha Kweli. Ndio Kitu Kilichowafanya Washindwe Uchaguzi na Mengi Yanakuja.
"Hakuna Katiba Hakuna Nchi"
 
Inasemekana Katika maswali ambayo humuudhi Muheshimiwa Jakaya mrisho kikwete, ni pamoja na Swala la Katiba ya Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania...

Ameshasikika ,marachache akisema kubadili katiba si maendeleo ya nchi huku akijua kuwa Katiba ndiyo inayo Bana maendeleo ya nchi,,

Tazama Zambia, Tazama Rwanda,, Nchi hizi mbili zilikuwa na rushwa na ufisadi wa kutupwa,, lakini Maraisi wake wameamua kujikubali kuwa lazima Wananchi waumie kwa kuwabana na sheria ngumu zinazo leta maendeleo ya nchi ili baada ya maendeleo hayo kupatikana watafurahia maisha

Wananchi wengi tunaishi kwa kukosa besic needs kwa kiwango kile kinachotakiwa,,,

Katiba hii inatakiwa ibadilishe jamaniniiii

kaka usintanie.......we ulijua atabadili au?
 
inasemekana katika maswali ambayo humuudhi muheshimiwa jakaya mrisho kikwete, ni pamoja na swala la katiba ya jamuhuli ya muungano wa tanzania...

Ameshasikika ,marachache akisema kubadili katiba si maendeleo ya nchi huku akijua kuwa katiba ndiyo inayo bana maendeleo ya nchi,,

tazama zambia, tazama rwanda,, nchi hizi mbili zilikuwa na rushwa na ufisadi wa kutupwa,, lakini maraisi wake wameamua kujikubali kuwa lazima wananchi waumie kwa kuwabana na sheria ngumu zinazo leta maendeleo ya nchi ili baada ya maendeleo hayo kupatikana watafurahia maisha

wananchi wengi tunaishi kwa kukosa besic needs kwa kiwango kile kinachotakiwa,,,

katiba hii inatakiwa ibadilishe jamaniniiii

kichwa chako cha thread hakiko sahihi, katika mdahalo siku mbili kabla ya uchaguzi mhe jakaya kikwete akijibu swali hilo alisema kuwa "kuwa katiba imeshafanyiwa mabadiliko mara nyingi tu haja inapojitokeza, na akaendelea kama itakuwepo haja ya kuifanya katiba mabadiliko serikali iko tayari kufanyia hivyo.

Kwa kauli hiyo ni wazi kuwa mlango wa majadiliano ya mabadiliko ya katiba uko wazi. Sipendi negativity ambayo wengi wetu tunayo kiasi cha kushindwa kutumia forum hii kubrain storm solutions za matatizo yanayoikabili tanzania hasa kuhusiana na katiba na tume ya uchaguzi mbovu.

Ni ukweli usiopingika kuwa katiba ya sasa ya inakipendelea chama tawala (ccm); na ni ukweli kwamba cccm kina wanachama kama milioni 3 mpaka 5 nchi nzima. Hivyo viongozi wa ccm wanabasis ya kudai kuwa katiba iliyopo haina tatizo wakitarajiwa kuungwa mkono na idadi hiyo wanachama.

Ni ukweli usiopingika kuwa tokea mfumo wa vyama vingi vya siasa kuanza mwaka 1992, vyama vya upinzani vimejitahidi sana kudai mabadiliko ya katiba kupitia njia mbali mbali ikwemo maandamano ya amani. Lakini kwa bahati mbaya watanzania waliokuwa wakijitokeza katika maandamano hayo ni wachache sana; sijui ni wangapi miongoni mwetu tulikuwa tukijitokeza wakati huo? Na sijui leo hii kama maandamano ya amani ya kudai mabadiliko ya katiba yataitishwa ni wangapi watajitokeza kuweza kupelekea ujumbe kwa watawala kuwa watanzania walio wengi wanataka mabadiliko ya katiba.

Hoja inayokuja hapo ni watanzania wangapi wasiokuwa wanajf wanafahamu kuwa mabadiliko yameshindikana kwa njia ya sanduku la kura kutokana na mapungufu makubwa ya katiba yeti na tume ya uchaguzi; na suluhisho ni kudai mabadiliko kwa njia za amani ama sivyo hadithi itakuwa ile ile mwaka 2015 kama ilivyokuwa 1995, 2000, 2005 na 2010.

Kama kweli tumekasirishwa na wizi wa kura unaolelewa na katiba mbovu na tume ya uchaguzi isiyokuwa huru, kila mmoja wetu anatakiwa kuanza kazi ya kuwaelimisha watanzania popote alipo mapungufu ya katiba tuliyonayo na kuwahamasisha kushiriki katika shughuli mbali mbali za kudai kmabadiliko ya katiba kwa njia za amani kama vile maandamano, makongamano, warsha semina n.k.

Shughuli hii inatakiwa kwenda sambamba kwa sisi tunaotaka mabadiliko ambao tunaona kuwa chadema ndio ngarawa yetu ya kutufikisha kwenye lengo hilo kukijenga chama cha chadema kutoka ngazi ya taifa kwenda ngazi ya mikoa, wilaya, tarafa, kata , vijiji, mitaa hadi kwenye mashina walipo watanzania. Hayo ndio mamabo mawili tunayotakiwa kuyafanya kati ya sasa hadi 2015 badala ya kuendelea kulia kulia pasipo kuchukua hatua zozote muafaka.

Kwa kuwa ccm wanatambua kuwa siasa ni watu, ni wazi katika kipindi cha 2010 -2015 watatumia mbinu mbali mbali kuhakikisha kuwa chadema inapungukiwa na uungwaji mkono wa wananchi. Endapo wapenda mabadiliko atutafanya mambo hayo mawili yaliyotajwa hapo juu, ni wazi kuwa 2015 si ajabu tukashuhudia ccm wakifanikiwa kusambaratisha vuguvugu la mabadiliko, ambapo itachukua muongo au miwili kujenga taena vuguvugu hilo.

Bahati ambayo tunayo ni kuwa penye riziki fitina hazikosi, kama alivyoanza chenge ccm ndio wameshaanza kugo,mbea madaraka na baada ya la uspika watafuata kugombea uwaziri, watagombea uchguzi kwenye chama na mwisho urais wa 2015. Huu ndio wakati tunaotakiwa kuutumia vyema kujijenga kwa wananchi ili ya 2010 yasiweze kujirudia.




 
kichuguu,

kwani ccm ilikuwa haijulikani ni majambazi kabla ya kuingia kwenye uchaguzi?? Wameanza kuiba kura tangu tunapiga zile za mtu na kivuli!!!!!!

Slaa hatkiwi kwenda ikulu ndio abadili katiba, tunataka katiba ibadilishwe sasa kabla ya mtu yeyote kwenda ikulu! Akifika pale atabadilika, kwani ni binadamu tu! Katiba inamlinda kiongozi kutotumia hulka za binadamu kuamua! Slaa was never a saint and was not qualified for that.

kama aliweza kuacha upadre, akaondoka ccm, na kutembea na mke wa mtu inaonyesha kabisa ni binadamu kamili mwenye kuhitaji sheria za kumlinda!!!!!

Tell him to fight for constitutional change starting from today, and see if he will dare to say that!!!

ukiondoa matusi yaliyo in red nakubaliana na wewe 100%. Tuelekeze hasira na machungu yeti katika kudai mabadiliko ya katiba na dr slaa atumie influence yake kushawishi watan zania kuunga mkono harakati hizi.
 
CCM wameibadili katiba mara 2 nikiona. Nahisi upo utaratibu wa kukusanya kura za maoni na zikifikia idadi fulani katiba inakubalika kujadiliwa. Sumaye aliwahi kuzunguka na walichokiita white paper kutafuta ridhaa ya wananchi kuibadili katiba.
Kazi ni wajumbe wa hiyo tume ya kuibadili katiba. Mkiishia na aina fulani ya Makame/NEC ndo kuliwa jumla.
CHADEMA wakicheza vyema waweza kuja na wahite paper na wakakusanya sahihi za watanzania tena wenye vitambulisho vya kupigia kura ikwa ni ushahidi tosha wa ridhaa ya wananchi. Nadhani faulo walocheza safari hii wataijutia tukifanya hivyo. Nonao ndo ponea yetu. Kazi ianze.
 
Hitaji la Tanzania sasa ni KATIBA MPYA na siyo kuweka viraka. Suala la Katiba ni la Watanzania woooote na siyo la madikteta kama Kikwete, Katiba iliyopo iliwezesha majambazi wa CCM wakishirikiana na vyombo vyao viovu kama TISS, NEC, POLISI, JWTZ kuiba na kuchakachua kura na kisha kumtangaza Fisadi JK kuwa rais kwa kujua kuwa Katiba iliyopo inalinda uozo kama huo. Naona sasa ni wakati wa wanaharakati kuongoza vugu vugu la kudai Katiba mpya, suala hili lisiwe la vyama vya siasa kwani itikadi na ushabiki wa vyama unaweza kutumiwa na vyombo viovu kama TISS kuwagawa Watanzania wakakosa umoja wa kufikia lengo hilo.
 
Uelewa wa Wananchi juu ya katiba upoje?
Watanzania wengi wanaielewa katiba iliyopo?
Wanavijua vipengele vilivyo vikwazo kwa maendeleo yao?
kwanza Wananchi waijue katiba(mbovu) ya sasa kisha ndio waelewa umuhimu wa kubadilisha.
Vinginevyo watu watahamasishwa waandamane kudai katiba mpya lakini ukimuuliza ni kipengele gani cha katiba ni kikwazo, Hajui. Yeye amekariri tu katiba ibadilishwe.
 
ukiondoa matusi yaliyo in red nakubaliana na wewe 100%. Tuelekeze hasira na machungu yeti katika kudai mabadiliko ya katiba na dr slaa atumie influence yake kushawishi watan zania kuunga mkono harakati hizi.

Hayo siyo matusi ni kukueleza kuwa binadamu ukimpa mwanya wa kujitawala atautumia tu, kuwa Slaa ni kigeugeu ni hulka za binadamu. Swala la kutembea na wake za watu mimi nimetemeba nao wengi sana kumshinda Slaa!!!! nazungumza ukweli, kwani sio ndio tulivyo??

Leo hii rais anachagua, director wa TAKUKURU, mkaguzi mkuu wa serikali, IGP, Jaji mkuu, makamishna, mwanasheria mkuu!!! hii yote inaashiria hali ya kisultan kama siyo kifalme!!!! wengi sio rahisi kubadili hali hii, na usitegemee mtu aliye kwenye position hii atabadili, never dream that! waulize Kenya na Kibaki wao!!! hata kakobe, pengo au kiognozi yoyote wa dini mpe hii nafasi uone! madaraka matamu ndugu

Yes Slaa can influence and he can initiate to change,na mimi lazima nimuandame maana uwezo anao ameukalia!!!!! I will keep on saying this.
 
We can change the KATIBA if we WANT. It is not for a single individual (whoever it is) to that decide that except the Tanzanian themselves.
 
2005 Sikumpa Kura Yangu JK; 2010 Sikumpa Kura Yangu JK. Kwa Sababu JK Ni Chekibobu. Siwezi Kutoa Kura Yangu Kwa Chekibobu. Bora Nife Tu, Kuliko Kutoa Kura Yangu Kwa Chekibobu. Chekibobu Hastahili Kuwa Rais wa TZ. Ndiyo Maana Tuna Matatizo Mengi Kwa Sababu ya Huyu Chekibobu JK.

Ni kweli kabisa .Hana tofauti na akina Ndama Mtoto wa Ng'ombe , etal

Mfamaji bana....ok bana ngoja nikugongee dole la kijani u made my day kabisaa.....
 
Jambo la msingi kabisa kwa sasa ni wabunge wetu kukaa chini kweli pale Dodoma na kuamka na utatuzi wa udhaifu unaojitokeza katika tume yetu ya uchaguzi.
Ndugu zetu wa Kenya wametuonyesha mwanzo mzuri sana katika harakati hizi ambazo ni muhimu kwetu. Ili kuondoa makundi ya wakosoaji katika jamii kuhitaji maoni ya wakosoaji hao ndio suala la msingi. Kenya wameepusha shari kwa kupitisha rasimu ya katiba mpya ambayo imepigiwa kura na wananchi.
Watanzania wote tuna nafasi japo kwa viwango tofauti katika ujenzi wa njia ya kuelekea katiba iliyojitosheleza na isiyokosolewa na wadau. Watanzania tuchague lipi? Kurekebisha katiba ili tulinde amani na ustawi wetu au kuhifadhi udhaifu ili baadaye tuwe kama Somalia na Congo –DRC?

Inauma sana kuongelea kitu kimoja toka mwana 1999,, hivi hawa watu CCM mbona ni wabishi wa maendeleo ya Tanzania
:A S angry:
 
As long as ccm wako madarakani na wingi wa wabunge basi sahau. hii katiba inawalinda sana ndo maana wanapinga katiba mpya!
 
Kutoa mahubiri marefu juu ya udhaifu wa tume ya uchaguzi kwetu wananchi hakutaleta tofauti yoyote kwani hatuna nafasi ya kusema A na E katika suala la katiba ila pengine kama tunaingia katika suala la rasimu ya katiba ambayo itahitaji maoni ya wananchi.
Jambo la msingi kabisa kwa sasa ni wabunge wetu kukaa chini kweli pale Dodoma na kuamka na utatuzi wa udhaifu unaojitokeza katika tume yetu ya uchaguzi.
Ndugu zetu wa Kenya wametuonyesha mwanzo mzuri sana katika harakati hizi ambazo ni muhimu kwetu. Ili kuondoa makundi ya wakosoaji katika jamii kuhitaji maoni ya wakosoaji hao ndio suala la msingi. Kenya wameepusha shari kwa kupitisha rasimu ya katiba mpya ambayo imepigiwa kura na wananchi.
Watanzania wote tuna nafasi japo kwa viwango tofauti katika ujenzi wa njia ya kuelekea katiba iliyojitosheleza na isiyokosolewa na wadau. Watanzania tuchague lipi? Kurekebisha katiba ili tulinde amani na ustawi wetu au kuhifadhi udhaifu ili baadaye tuwe kama Somalia na Congo –DRC?
Woga wetu sisi utatupeleka pabaya Na ni watanzania wachache tu ndio wanaotunyima maendeleo sisi wenye uchu wa maendeleo,,
FURSA ZA MAENDELEO TUNAZO, CCM WANAZIZUIA KWANINI? (BORA TUANDAMANE KWA AMANI KABISA KUIPINGA KATIBA ILIYOPO"")
 
Tupatieni Katiba Yetu
Kelvin Kachingwe

LUSAKA, Okt 28 (IPS) - Shinikizo linazidi kupanda kwa ajili ya katiba mpya inayoainisha maoni ya wananchi wakati ucheleweshaji wa kuandaa rasimu hiyo bado unaendelea.

Pamoja na kwamba Kongamano la Taifa la Katiba (NCC) liliongezewa muda wa miezi minne kutoka ombi la kwanza la miezi 12, shinikizo inazidi kupanda kwa chombo hicho kukamilisha katika muda uliowekwa ili nchi ipate fursa ya kuendesha uchaguzi mwaka 2011 chini ya katiba mpya.

Zoezi la kuandika rasimu ya katiba mpya ambalo liliwashirikisha wananchi katika mijadala, lilianzishwa na rais aliyefariki Levy Mwanawasa. Lengo lilikuwa kuizuia serikali pekee kupitisha Katiba ya Jamhuri kinyume na demokrasi.

Chombo cha NCC, ambacho kilianzishwa mwaka 2007, kilitakiwa kuandika rasimu ya katiba ambayo ingesubiri maoni ya wananchi katika kipindi cha mwaka mzima.

Lakini ilipofika katikati ya mwaka 2009, NCC iliomba mwaka mmoja zaidi ili kufanikisha zoezi. Rais Rupiah Banda, ambae ana mamlaka ya kukubali ametoa miezi minne tu badala ya 12 iliyoombwa.

Akitangaza kuhusu kuiongezea muda dhamana ya NCC wakati wa uzinduzi rasmi wa bunge mwezi uliopita, Rais Banda amesema anasikitishwa na jinsi mambo yanavyoenda polepole.

Tilyenji Kaunda, mtoto wa rais wa kwanza, Dr Kenneth Kaunda na kiongozi wa chama cha upinzani cha United National Independence, anasema NCC haina budi kumaliza kwa haraka kazi yake katika muda uliowekwa ili uchaguzi mkuu ujao ufanyike chini ya katiba mpya.



"Katika vikao vyake vijavyo, NCC hazima ihakikishe inamaliza kazi kwa sababu wananchi wengi wa Zambia wana shauku kuona katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu ujao," amesema katika mkutano na vyombo vya habari mapema mwezi huu.

Chama cha upinzani cha United Party for National Development (UPND) kinasema kwamba kina wasiwasi kwamba muda ulioongezwa wa mchakato wa katiba mpya ni ishara kwamba nchi haitakuwa na katiba mpya wakati wa uchaguzi mwaka 2011.

"Iwapo tutaendelea kuongeza muda wa NCC, kuna uwezekano wa kutokuwa na katiba mpya mwaka 2011 kwa sababu bado kuna mazoezi mengine kadha ambayo yanatakiwa kufanyika hususan kuendesha kura ya maoni, ndio maana kuongezwa kwa muda sio dalili nzuri kwa taifa," Charles Kakoma, mwenyekiti wa habari na uhamasishaji wa UPND anasema.

Hata hivyo, msemaji wa NCC, Mwangala Zaloumis anasema kuongeza muda ni muhimu kwa sababu mbalimbali ambazo zimeifanya NCC kushindwa kufikiria ripoti za kamati sita kati ya 11 ambazo chombo kilistahili kuzipitia wakati wa kipindi cha mwaka mmoja wa mamlaka hayo.

"Kuongeza muda kulisababishwa na mambo mengi, baadhi ya hayo ni kifo cha Rais Mwanawasa mwaka uliopita, kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa rais na vile vile mabadiliko ya hivi karibuni katika mzunguko wa bajeti. Wakati Bunge linaendesha kikao chake, NCC hairuhusiwi kufanya kazi," Zaloumis amesema.

Profesa Patrick Mvunga, mwanasheria wa katiba, anasema kwamba kuharakisha mchakato wa kutayarisha katiba mpya kwa sababu ya uchaguzi mkuu mwaka 2011 hakutaweza kuleta matokeo mazuri yaliyokusudiwa.

"Ni vizuri kila wakati kufanya kazi nzuri, na kazi nzuri lazima iende na wakati. Iwapo sababu kubwa ya kuwa na katiba ni kwa ajili ya uchaguzi, wale wote wanaotaka katiba ikamilishwe badala yake waiambie NCC wamalize kuzishughulikia sheria zote zinahohusu uchaguzi," Profesa Mvunga anasema.

" Kama ni muhimu hivyo, ingebidi vipitie vifungu vinavyohusiana na uchaguzi na ndio maana sielewi pale watu wanaposema kwamba lazima tuwe na katiba kabla ya uchaguzi mwaka 2011 kwa sababu sio vifungu vyote katika katiba vinahusu uchaguzi, sio mambo yote katika katiba ni uchaguzi."

George Kunda, makamu wa rais nchini alisema mwaka uliopita kwamba NCC itamaliza kazi yake ifikapo Desemba 2009 ili taifa liwe na katiba mpya kabla ya uchaguzi mwaka 2011 lakini aliongeza kwamba mchakato lazima uwe wenye uhalisi na sio wa kuharakisha.

"Hatuwezi kuhujumu mchakato kwa kupendekeza muda usio halisia. Tutamaliza kati kabla ya 2011, lakini tusipendekeze muda ambao hauendani na kazi yenyewe," amesema.

Mwezi Julai 2008, kikundi cha vyama vya vyama hiari, katika barua walioiandikia sekretarieti ya NCC na kunakili kwa Rais, Waziri wa Sheria na Mwanasheria Mkuu, ilidai kwamba kongamano limalize kazi yake ifikapo mwishoni mwa mwezi Julai 2009 na kutoa ripoti ya fedha ya kina kuhusu matumizi ya fedha za umma tangu ilipoanzishwa.

Mashirika yamesema kwamba NCC ilibidi kumaliza kazi yake mara moja ili kutoa fursa kwa zoezi jingine linalohusu ya kupitishwa kwa katiba, hususan Kura za Maoni, liweze kufanyika kabla ya uchaguzi mwaka 2011.

"Zoezi kubwa kama hilo haliwezi kuachiwa lifanye kazi bila kuwa na ratiba maalum…na ili kuonyesha uwajibikaji na uwazi, tunataka ripoti ya fedha kutoka NCC na matumizi yake," ilisomeka sehemu ya barua hiyo iliyoandikwa na baadhi ya wawakilishi kutoka Transparency International Zambia, Citizens Forum, Women in Law Southern Africa na Southern African Centre for Constructive Resolution of Disputes.

Kujibu hoja hiyo, mwenyekiti wa NCC Chifumu Banda alisema kwamba kongamano ni taasisi ya serikali ambayo hukaguliwa na Mkaguzi Mkuu.

"Katibu wa NCC ndie afisa mdhibiti pamoja na mafungu yote yanashughulikiwa na watumishi wa serikali. Matumizi yetu yatawekwa wazi kwa wananchi," amesema.

Lakini Michael Sata, kiongozi mkorofi wa upinzani kutoka chama cha Patriotic Front anapinga kuongezewa muda NCC na anatoa changamoto kwa chombo hicho kuonyesha maendeleo yaliyofikiwa hadi sasa.

"Kila mtu NCC, hawako pale kutayarisha katiba, wako pale kugawana dola milioni 80 zilizotengwa kwa ajili ya kazi hiyo. Watatumia kila sababu kuhakikisha kwamba ‘wanazimaliza' dola milioni 80 kwa ajili ya vikao," Sata amesema.

Situmbeko Musokotwane, waziri wa fedha, katika hotuba yake ya bajeti mwezi uliopita, ametenga fungu jingine la dola milioni 1 kwa ajili ya NCC baada ya rais kuongeza muda wa mamlaka hiyo kwa miezi mingine minne.

Mapema mwaka uliopita, katibu wa NCC Russell Mulele alisema kwamba ingawaje rais ana mamlaka ya kuongeza mamlaka baada ya muda wa miezi 12 kumalizika, watahakikisha kwamba wanakamilisha kazi hiyo katika muda uliowekwa ili uchaguzi mkuu mwaka 2011 ufanyike chini ya katiba mpya.

Banda anasema ana imani kubwa kwamba katiba mpya itakuwa tayari kabla ya uchaguzi mkuu.

"Hatutarudi nyuma kwa sababu tumetoka mbali na tunakaribia ukingoni kukamilisha zoezi la katiba," Banda anasema.

"NCC ina muda maalum ukiondoa siku ambazo Bunge linafanya kikao, siku za mapumziko na siku za mwisho wa wiki, isingekuwa hivyo na maombolezo ya Rais Levy Mwanawasa, tungefika mbali."

Kupitishwa kwa Sheria ya NCC kunatokana na mapendekezo ya wananchi kwa Kamati ya Kupitia Katiba ya Wila Mung'omba kwamba katiba ipitishwe na Bunge, Kongamano la Katiba au chombo kingine chochote kinachoaminika ambacho kitawakilisha mawazo ya wananchi. (END/2009)


Someni kwa Wazambia jamani Wapo juu kutuzidi sisi kwanini tubaki nyuma jamani?
 
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]TATIZO LA TANZANIA NI CCM

Matatizo ya Tanzania ni CCM. Miaka arobaini madarakani, wameharibu kila kitu. Utalaumu nini Tanzania ukose mkono wa CCM?

Kichwa kuuma, husababishwa na mengi. Utakosea sana kununua "HEADACHE" kutuliza maumivu ya kichwa, kumbe macho ndiyo sababu kichwa kuuma. Bila kutibu macho, utajisumbua bure lakini kichwa bado kitaendelea kuuma, na kinaweza kusababisha viungo vingine mwilini kuuma.

CCM ndio chanzo cha matatizo yetu Tanzania. Hakuna marekebisho bila CCM kutoka madarakani. Utaanzia wapi?

Ni kweli kwamba CCM ni chama tu, na watu ndani ya chama hicho ndio waliotunga sera mbovu zilizoipelekea Tanzania kuwa ilivyo. Sambamba na hilo, ndiyo maana tunataka KATIBA ibadilishwe ili Munishi niingie madarakani bila chama.

Ni katiba mpya ndiyo itakayotengeneza mazingara mazuri ya watanzania kuongozwa kujiongoza. Na mtu tayari kufanya yote hayo ni mimi Munishi. Kama kuna wengine siyo kazi yangu kuwatafuta, wajitokeze hapa kwenye ukumbi huu wamwage siasa zao hapa. Mimi siyo mwanasiasa na sitarajii kuwa mmoja. CCM wakitoka madarakani baada ya katiba waliyoiharibu kurekebishwa na kuwa katiba ya wananchi iliyo na mawazo ya wananchi kwa ajili ya wananchi, kila kitu kitakuwa shwari. Uchumi wetu unaweza usiwe kama wa Marekani kwa mwaka mmoja, Lakini utakuwa ukielekea huko. CCM Kiini cha matatizo Tanzania kitakuwa kimetoka.

Huitaji kuwa msomi wa chuo kikuu kujua kwamba CCM ndio chanzo cha kila tatizo Tanzania. Lakini kama wewe ni msomi na hujagundua kwamba CCM ndio chimbuko la matatizo Tanzania, nakupa pole. Nchi masikini duniani haziongozwi na CCM, lakini Tanzania ilitokea kutawaliwa na CCM kwa zaidi ya miaka 45 na watanzania wana kila sababu ya kutaka CCM itoke kwenye maisha yao. Je itamaliza matatizo yao? Ndiyo. Wengine watafaidi matunda ya ukombozi, na kuna wale dhaifu ambao hawataishi kuonja matunda ya ukombozi. Lakini haitukatishi tamaa ya kujikomboa.

Gari ambayo mitambo yake ya kujaza betri moto ni mibovu, inahitaji mitambo mingine na siyo betri mpya. Ukikosea uweke betri mpya na yenyewe itamalizwa nguvu kwani mitambo ya kuijaza nguvu imekufa. Tanzania iliwekwa betri mpya yaani Mwinyi na MKAPA, na zote zimenyonywa moto zikawa hazifai.
Ndiyo maana Tanzania inahitaji mitambo mipya inayozalisha sheria na utengamano. Hii ni KATIBA MPYA itakayoketa uongozi mpya, utakaoleta ENZI MPYA, itakayoleta maisha mapya, yatakayoleta maendeleo, yatakayorekebisha hali ya uchumi wetu, utakaosababisha kila kitu kurekebika na kuwa jinsi ambavyo hakikuwa wakati wa CCM.[/FONT]
[/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Tulitegemea huyu Kikwete ambaye alichaguliwa na Wananchi kwa Asilimia Nyingi sana atafanya Mabadiliko mazuri katika ustawi wa watanzania lakini kilichotolea ni kualibika kwa amani ya mioyo ya Watanzania,, siongelei amani ya Nchi naongelea Amani ya kuto kujua hatma yao miaka ya mbele,[/FONT][/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][/FONT][/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Naomba Watanzania tujiunge kupigania KATIBA MPYA[/FONT][/FONT]
 
Ndugu watanzania tunatakiwa kuomba KATIBA MPYA kwa kutumia Viongozi wetu wa vyama vya siasa. Tunaomba CHADEMA na Asasi zisizokuwa za kiraia zituongoze kwa hilo.

Ndugu Watanzania tukishinikiza SERIKALI kuitisha mkutano wa KATIBA MPYA ndo tutaweza kupata TUME HURU YA UCHAGUZI, TAKUKURU HURU (Siyo hii ya sasa inayosafisha MAFISADI -RICHMOND NA RADA).

CCM na Kikwete hawako tayari kufanya hivyo ila kwa shinikizo kubwa kutoka kwa wananchi kwa kuandamana na kuwazomea kama tulivyofanya kwa baadhi ya Mawaziri wakati furani.
Tusiposhinikiza KATIBA mpya MAFISADI wa CCM wataendelea kutafuna nchi na kwa sasa wengine wanataka usipika.

Kwa People Power ................. Inawezekana
 
Back
Top Bottom