New Mount Meru Hotel | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

New Mount Meru Hotel

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by ndezi, Dec 2, 2010.

 1. n

  ndezi Member

  #1
  Dec 2, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani kwa wakaazi wa Arusha na vitongoji vyake watakuwa wameshaona kwenye mabango mbalimbali barabarani ama kupitia redio ama magazeti ya kuwa iliyokuwa inaitwa novotel mount meru hotel inafunguliwa tena upya ikijulikana kama New Mount Meru Hotel.

  Kikubwa nachotaka kuwafikishia watanzania wenzangu ni kuwa nimestaajabika sana ile maana kamili ya uwekezaji kuendelea kutupwa kapuni. Huwezi amini moderator na watanzania kwa ujumla, Hotel hii hadi maua na mchanga vyote vimetoka South Africa ambapo ndipo ilipo kampuni iliyopewa jukumu la kuindesha hotel hii ijulikanayo kama Zabulan.

  Nachokiona hapa ni kuwa wasauzi afrika wao wanathamini vyao hata kama wako nje ya kwao, itakumbukwa watu walishapiga kelele kuhusu bidhaa zipatikanazo shoprite ya kuwa hadi nyanya na vitunguu hata mchicha vinatoka hukohuko SA, sasa ambacho watu watajionea hapa ni kuwa mchanga, maua, mbolea, signboards, tisheti, viatu, sabuni, vitambaa, computer, curtains na vyooote vinatoka sauzi afrika, hivi ina maana hapa hatuna hivyo vitu; vingine itasemekana labda viwango na jee hata mbolea na mchanga??

  Kali zaidi ni kuwa Senior staffs woote ni ndani ya sauzi afrika ama asia au kwa watani wa jadi, ina maana hapa hatuna mameneja wazuri wakuendesha hotel? hatuna mashefu wazuri hapa tz?

  Ikumbukwe walisema katika ajira wataweka mbele wazawa...hii imefia wapi??

  Kama uwekezaji ndo hivi jamani bora tufie na tai shingoni.

  Kali nyingine ni kuwa Raisi wetu yuleyule aliyeifunguaga Snow Crest Hotel then kesho yake ikaja kuvunjwa ukuta ndio anakuja tarehe 17Dec kuifungua hii ambayo ilikuwa mali ya watanzania then mkapa na magufuli wakaiuza na sasa watanzania hawana hata percent moja hapa, hilo moja pili ni kuwa wafanyakazi woote ni wametoka kenya ama sauzi afrika ma bara asia na pia waliopewa tenda za ku-supply vyakula ni wakenya tupu na vyote vinatoka hukuhuko kenya kuanzia kuku, maharage hadi matunda, jamani rais hana washauri wakamfungua kwenye hili na jee watanzania tutakuwa wapole hadi lini watu wanakuja kupora malighafi zetu na kukimbia??

  Ama ndio kichwa cha mwendawazimu??

  TUAMKE WATANZANIA NA TULIANGALIE HILI SWALA LA MOUNT MERU KWA JICHO LATATU.

  NGUVU YA UMAA IFANYE KAZI JAMANI............
   
 2. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #2
  Dec 2, 2010
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Na bado....
   
 3. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #3
  Dec 2, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  CCM na serikali yake. Na bado .
   
 4. Mtumpole

  Mtumpole JF-Expert Member

  #4
  Dec 2, 2010
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Mbona wabongo wengi mnapenda kulalama sana! Fanyeni kazi mpaka mwaka 2015 tena.
   
 5. k

  kibenya JF-Expert Member

  #5
  Dec 2, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  mbunge wenu awape majibu ya kuridhisha yawezekana wanakwepa kodi
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Dec 2, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu Ndezi (nice name though)... wewe leo ukienda Sauzi ukakuta mijitu yenyewe mivivu, majungu, kulalama, mafisadi, vibaka, wasengenyaji na aliyekupa hizo nyuzi ni msauzi mwenyewe utafanyaje?

  Si utaanza kutafuta unaowaamini?? Ndivyo hospital ilivyofanya hao makaburu

  Hayo ya maua na majani, sina la kusema kwasbabu ni mijitu yetu ya borders (airport bandari na mpakani) ndiyo imeruhusu

  MITANZANIA NDIVYO TULIVYO
   
 7. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #7
  Dec 2, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,053
  Likes Received: 3,964
  Trophy Points: 280
  nathani useme ukweli hiyo Hotel iliiuzwa kwanza kwa Mtanzania chini ya Blue Jewel Co akawa hana hela ya kuifufua ndo akaingia ubia na the Southern African Enterprise Development Fund (SAEDF) ambao kwa sasa wanamiliki 40% kufanya kampuni Hotel Management Company Ltd (HODI)! Tuache majungu Wabongo kama Hotel mlipewa ila ndo mambo ya ufisadi aliyeuziwa hakuwa na uwezo wa kuikarabati kama makubaliano yalivyohitaji mfanywe nini? na wa kulaumiwa ni nani? halafu suala la mchanga kuletwa toka SA kuna vitu kama "organic humus soil" na "compost" ambavyo vyote hutumiwa kupanda maua na majani sidhani kama kuna kampuni hapa Tanzania inayoshughulika na kutengeneza bidhaa hizi! nathani hilo linahitaji maarifa zaidi ya kulalamika! uwezo wa wafanyakazi pia nathani kuna Watanzania pia wameajiriwa kutokana na uwezo wao... sasa huwezi kumlazimisha mwekezaji hata awe Mtanzania kuweka Watanzania woote kazini bado tuna upungufu wa skilled individuals with experience nathani over time hayo mambo yataisha tuwe na subira!
   
 8. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #8
  Dec 2, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145

  Hiyo hotel serikali ilimuuzia muwekazi mzalendo, Bwana Sunda, ambaye aliendelea kumtumia meneja yuleyule aliyekuwa akiindesha kabla ya kuuzwa, huyo ni mkenya, Fred Maina. Baadae Sunda alizidiwa na madeni katika biashara zake na kwakuwa hana elimu (hajakanyaga hata darasa moja) alishauriwa na mmoja wa aliyekuwa naibu gavana wa BOT kuwa watafute wawekezaji watakaonunua nusu ya shares za Sunda.

  Sunda hakujua ule mchezo, muwekazaji alikuja kutoka South-Africa, ni taasisi yenye makao makuu yake USA. Sunda aliingia mikataba ya kijinga kabisa na kilichotokea mwishowe alilazimika kuuza shares karibu zote. Alifanyiwa ufisadi wa kimafia, siri zingine ni za ndani mno na zinawahusisha watu wengi wakubwa, lakini kikubwa alihujumiwa.

  Upande wa pili wa stori, turudi kwenye uuzwaji wa ile hotel, kwa kweli serikali iliiuza kwa bei ya kutupa, ulikuwa ni ujinga kuiacha hoteli kama ile iende kiholela kama vile, mkumbo huo pia ulizipata hotel kama Embassy na Kilimanjaro ambapo wakubwa walitiuibia kwa kutunganya na sera yao ya privatization.

  Kuhusu bidhaa zinazotumika kwenye hotel hiyo kutoka S.Africa na Kenya, hivi wewe ndugu yangu ungebahatika kupata diliu kwenye Taifa lenye viongozi vilaza kama TZ usingefanya kama hao wa-south, serikali imefumba macho, jamaa wanakamua tu kama kawa!
   
 9. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #9
  Dec 2, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Mameneja wa kibongo vikao tuu vya kupeana taarifa za kazi vinavyofanyika ndani ya masaa ya kazi wanataka walipwe allowance!!!! Sekta binafsi haiendeshwi hiyvo
   
 10. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #10
  Dec 2, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Tumeyataka wenyewe. Na huo ndio ushindi wa CCM, chama cha waTanzania wasiopenda ukombozi.
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Dec 2, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  majungu yamezidi watanzania... Dah
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Dec 2, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  nASIKITIKA KUSEMA KWAMBA HII POINT HAINA MASHIKO... SI KILA KITU KINAANZIA KWENYE SIASA...

  UWAJIBIKAJI NI KILA SEHEMU
   
 13. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #13
  Dec 2, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Muhimu ni "Impact" kwa uchumi wetu ukilinganisha kabla ya kuuzwa na baada ya kufunguliwa upya. Kwamba Serikali ililipwa ngapi siyo "Relevant" tena hata kama ingetolewa bure ili kukuza ajira nalo ni sawa tuu
   
 14. N

  Newvision JF-Expert Member

  #14
  Dec 2, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  "Humus soil" ni kitu gani mzee ni kitu rahisi ni mboji ya kawaida tu hakuna cha ajabu.Ila kusema kweli uwajibikaji wetu ni mbovu kila tunapopewa majukumu na tukishindwa maneno yako kibao mdomoni na hili linatupa changamoto hata sisi wenyewe wana JF katika maeneo yetu ya kazi tunawajibikaje??? Toka Rais wetu mpaka serkali yake si wawajibikaji nasema hivyo kwa sababu gani vitu vyote vya kisheria vilishawekwa vitabuni lakini havitekelezwi na wasomi wapo na wana Degree mpaka PhD! We are too lazy to be accepted as hard workers hata kama sasa tuna wasomi wengi kuliko zamani. Mtu anakuja ofcni saa3/4 anaondoka saa 6 na bosi anamwona sasa hii hatuendi hivi.
   
 15. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #15
  Dec 2, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,053
  Likes Received: 3,964
  Trophy Points: 280
  Hapo ndo unapopigwa bao wenzio wana makampuni ya kuuza aina hiyo ya mchanga....angalia hapa kukusaidia kuwa watu hawapigi kelele they mean business http://www.humusproducts.com/ na gardening ni profession
   
Loading...