New Mount Meru Hotel

ndezi

Member
Nov 25, 2010
6
0
Nadhani kwa wakaazi wa Arusha na vitongoji vyake watakuwa wameshaona kwenye mabango mbalimbali barabarani ama kupitia redio ama magazeti ya kuwa iliyokuwa inaitwa novotel mount meru hotel inafunguliwa tena upya ikijulikana kama New Mount Meru Hotel.

Kikubwa nachotaka kuwafikishia watanzania wenzangu ni kuwa nimestaajabika sana ile maana kamili ya uwekezaji kuendelea kutupwa kapuni. Huwezi amini moderator na watanzania kwa ujumla, Hotel hii hadi maua na mchanga vyote vimetoka South Africa ambapo ndipo ilipo kampuni iliyopewa jukumu la kuindesha hotel hii ijulikanayo kama Zabulan.

Nachokiona hapa ni kuwa wasauzi afrika wao wanathamini vyao hata kama wako nje ya kwao, itakumbukwa watu walishapiga kelele kuhusu bidhaa zipatikanazo shoprite ya kuwa hadi nyanya na vitunguu hata mchicha vinatoka hukohuko SA, sasa ambacho watu watajionea hapa ni kuwa mchanga, maua, mbolea, signboards, tisheti, viatu, sabuni, vitambaa, computer, curtains na vyooote vinatoka sauzi afrika, hivi ina maana hapa hatuna hivyo vitu; vingine itasemekana labda viwango na jee hata mbolea na mchanga??

Kali zaidi ni kuwa Senior staffs woote ni ndani ya sauzi afrika ama asia au kwa watani wa jadi, ina maana hapa hatuna mameneja wazuri wakuendesha hotel? hatuna mashefu wazuri hapa tz?

Ikumbukwe walisema katika ajira wataweka mbele wazawa...hii imefia wapi??

Kama uwekezaji ndo hivi jamani bora tufie na tai shingoni.

Kali nyingine ni kuwa Raisi wetu yuleyule aliyeifunguaga Snow Crest Hotel then kesho yake ikaja kuvunjwa ukuta ndio anakuja tarehe 17Dec kuifungua hii ambayo ilikuwa mali ya watanzania then mkapa na magufuli wakaiuza na sasa watanzania hawana hata percent moja hapa, hilo moja pili ni kuwa wafanyakazi woote ni wametoka kenya ama sauzi afrika ma bara asia na pia waliopewa tenda za ku-supply vyakula ni wakenya tupu na vyote vinatoka hukuhuko kenya kuanzia kuku, maharage hadi matunda, jamani rais hana washauri wakamfungua kwenye hili na jee watanzania tutakuwa wapole hadi lini watu wanakuja kupora malighafi zetu na kukimbia??

Ama ndio kichwa cha mwendawazimu??

TUAMKE WATANZANIA NA TULIANGALIE HILI SWALA LA MOUNT MERU KWA JICHO LATATU.

NGUVU YA UMAA IFANYE KAZI JAMANI............
 
nimepita hapo jtatu hii na kuyaona haya.....ila bado haijachangamka sana......

staff karibu wote ni kutoka nje ya tz....kaka nguvu ya umma ifanye kazi ganitena juu ya hii hotel? unadhani watu wanakuelewa hapa?....
 
Tatizo lilipo ni kuwa, wakubwa waliopo na wanaosikia haya malalamiko wanashare, ni ngumu kwa mwananchi wa kawaida kubadilisha haya zaidi ya kupiga kelele. Mfumo mchafu uliojaa hauruhusu:(
 
Najuta kusoma hii sred imenipa uchungu sana,nakumbuka iliyokuwa mount meru ya kwanza ilivyokuwa na wazawa wengi na wengi walinufaika kupitia ajira zao,new mount meru is becoming the worsiest one huh!
 
Wabongo hawaaminiki,kila kitu kuchakachua yawezekana waliogopa kuwapa tender kwa kuogopa uchakachuzi.unaweza kumuagizia mbongo udongo akakuletea tope la tindigani.tupunguze kuchakachua kwani madhara yake ndo haya!
 
Back
Top Bottom