New International Airport and Port in Bagamoyo; hivi ni vipaumbele sahihi?

Kujenga bandari bagamoyo sina tatizo nalo. Bandari ya DSM ina kina kifupi meli za mizigo kubwa haziwezi kuingia, wakati huohuo mzigo kwenda/kutoka majirani zetu (land locked) inaongezeka exponentially. To me, it is a big long-run strategic decision.

Kwa kuongeza Dar imejaa, miundombinu yake imekwishaelemewa.

Kuhusiana na uwanja, sidhani kama kuna mpango wa kujenga international airport Bagamoyo kwa sasa. Nijuavyo ni kuwa kuna haja ya kutenga sehemu (reserve) kwa ajili mahitaji ya uwanja mkubwa baadaye. Kwa sasa pajengwe uwanja mdogo tu (to safeguard the reserved land). Sio kitu cha kushandaza kuwa na zaidi ya kiwanya kimoja kwenye mji.

Jiulize, Nairobi kuna viwanja vingapi?
Ninawasilisha.
 
GreatThinkers,
Sie watu wa Mwanza tunamwangalia kwa hasira mbaya, tunapata tabu sana Airport yetu iko kama Shule ya kata. JK ni mtu wa matanuzi tanuzi haangalii wapi pana umuhimu.

wee ngoja yeye anazeeka sie tunakua, ipo siku watajutia maamuzi hao tatanishi.

WATz hebu chunguzeni ni nchi gani ina kiwanja ambacho kipo kama chenu DIA karibu na makazi ya watu. Hakika viwanja vingi vikubwa vimejengwa kwenye fukwe za bahari. hebu angalieni kiwanja cha Entebbe lakini sio kama kile cha Bukoba.

Vile vile bagamoyo ni sehemu nzuri sana kujenga bandari za kisasa na pia uwanja wa ndege ili mueze kujiimarisha uchumi wenu na kuinua uchumi.

jamani tazameni kila kitu katika jicho la kuendeleza nchi yenu kiuchumi.. Nafikiri huo ni mwanzo mzuri.
 
Kujenga bandari bagamoyo sina tatizo nalo. Bandari ya DSM ina kina kifupi meli za mizigo kubwa haziwezi kuingia, wakati huohuo mzigo kwenda/kutoka majirani zetu (land locked) inaongezeka exponentially. To me, it is a big long-run strategic decision.
Kwa kuongeza Dar imejaa, miundombinu yake imekwishaelemewa.
.

Bob, hapo kwenye red: sijui umetoa wapi huo ushuhuda! Kama Bandari ya DSM ina kina kifupi, je, meli zimekuwa zinatia nanga wapi na kivipi? Na kama DSM ina kina kifupi Bagamoyo tusemeje? Kujenga bandari Bagamoyo hakuna tofauti na kujenga nchi KAVU. It will cost an arm and a leg to create a functioning bandari Bagamoyo! Kwa nchi masikini kama hii kwa nini wasiwekeze sehemu ambazo physical location yake kwanza ni strategically important kwa uchumi wa nchi kwa maana ya kuwa inatunganisha kirahisi na nchi jirani hivyo kuengeza ushindani i.e Mombasa. Mfano, Tanga, Mtwara na Zanzibar. Haya maeneo tayari yana kina kirefu na hata kujaa na kupwa kwa maji hakutaathiri sana kina.

Ukiongea na wataalam (walio huru) watakueleza kuwa sio busara kujenga bandari Bagamoyo. Na Tayari kuna nchi wafadhili wameshaonesha kuwa hawataki hata kidogo kuliongelea hili maana wanaona ni usanii. Nadhani Kikwete anategemea nchi za kiarabu kwenye huu ujenzi ila sina hakika baada ya financial crisis hizi nchi bado zinataka kuendeleza hili wazo. Hata hivyo nina wasiwasi sana (pamoja na ufadhili utakaopatikana) kama huu mradi kweli utakamilika! It is a very expensive idea na economically hai-make sense.

Pia wazo la kusema DAR imejaa nadhani ni ulemavu wa kufikiri. Dar haijaja, sanasana Dar inaugua ugonjwa wa planning (or lack of it). Kama kungekuwa na proper public transport system hivi VI-TOYOTA vyetu tungeviacha garage. Pili, kama huduma muhimu zingesambazwa sehemu tofauti za mji watu wasingekuwa na haja ya kwenda city centre (hasa huduma toka serikalini). Tatu, kama serikali ingeacha ngonjera na kuhamia Dodoma tusingesimama kwenye foleni tukisubiri misafara. Nne, kama usafiri wa Reli ungeboroshwa hapa jijini, sisi walalahoi tusingewekeza kwenye vi-Hiace.

La mwisho na muhimu. Kwenye uchumi (hata uchumi wa ki-mamndenyi) unawekeza kwanza eneo lenye return kubwa na kwa urahisi (kihalali) ili utumie hiyo faida kuendeleza mambo mengine. Serikali hata kama ingetumia hii formula ya 'uchumi wa ki-mamndenyi' wangewekeza kwenye Bandari na viwanja vya ndege sehemu ambazo zitaleta faida haraka kwa nchi then use the profit to sort out other "wishful thinking". Jenga bandari Tanga, Mtwara, na imarisha ya Dar (iko connected na Railway - a major bonus kwa kuvutia nchi jirani). then imarisha viwanja vya ndege DAR, Mwanza, KIA na Mbeya. Hizi zote ni strategic locations.

Hapa utatengeza pesa bila shaka na tumia faida kujenga mambo mengine huko Bagamoyo etc etc. Lakini kwa mtindo huu ni sawa na mkulima kula mbegu - tusitegemee mavuno!
 
Watanzania sisi tunaokaa tegeta, goba,bunju tunashukuru kwa ujenzi wa barabara ila si kweli kwamba kunaumuhimu sana wa bandari wala kiwanja cha ndege ila watu wanavutia kwao. inatuingiza katika gharama kama taifa na mbele tutakuja ona na kutambua hakika. poleni watanzania kwetu wote kwa maamuzi haya. kwani kuna miundombinu mingi mibovu inaitaji kurekebishwa.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
@Bob, hapo kwenye red: sijui umetoa wapi huo ushuhuda! Kama Bandari ya DSM ina kina kifupi, je, meli zimekuwa zinatia nanga wapi na kivipi? Na kama DSM ina kina kifupi Bagamoyo tusemeje? Kujenga bandari Bagamoyo hakuna tofauti na kujenga nchi KAVU. It will cost an arm and a leg to create a functioning bandari Bagamoyo! Kwa nchi masikini kama hii kwa nini wasiwekeze sehemu ambazo physical location yake kwanza ni strategically important kwa uchumi wa nchi kwa maana ya kuwa inatunganisha kirahisi na nchi jirani hivyo kuengeza ushindani i.e Mombasa. Mfano, Tanga, Mtwara na Zanzibar. Haya maeneo tayari yana kina kirefu na hata kujaa na kupwa kwa maji hakutaathiri sana kina.

Ukiongea na wataalam (walio huru) watakueleza kuwa sio busara kujenga bandari Bagamoyo. Na Tayari kuna nchi wafadhili wameshaonesha kuwa hawataki hata kidogo kuliongelea hili maana wanaona ni usanii. Nadhani Kikwete anategemea nchi za kiarabu kwenye huu ujenzi ila sina hakika baada ya financial crisis hizi nchi bado zinataka kuendeleza hili wazo. Hata hivyo nina wasiwasi sana (pamoja na ufadhili utakaopatikana) kama huu mradi kweli utakamilika! It is a very expensive idea na economically hai-make sense.

Pia wazo la kusema DAR imejaa nadhani ni ulemavu wa kufikiri. Dar haijaja, sanasana Dar inaugua ugonjwa wa planning (or lack of it). Kama kungekuwa na proper public transport system hivi VI-TOYOTA vyetu tungeviacha garage. Pili, kama huduma muhimu zingesambazwa sehemu tofauti za mji watu wasingekuwa na haja ya kwenda city centre (hasa huduma toka serikalini). Tatu, kama serikali ingeacha ngonjera na kuhamia Dodoma tusingesimama kwenye foleni tukisubiri misafara. Nne, kama usafiri wa Reli ungeboroshwa hapa jijini, sisi walalahoi tusingewekeza kwenye vi-Hiace.

La mwisho na muhimu. Kwenye uchumi (hata uchumi wa ki-mamndenyi) unawekeza kwanza eneo lenye return kubwa na kwa urahisi (kihalali) ili utumie hiyo faida kuendeleza mambo mengine. Serikali hata kama ingetumia hii formula ya 'uchumi wa ki-mamndenyi' wangewekeza kwenye Bandari na viwanja vya ndege sehemu ambazo zitaleta faida haraka kwa nchi then use the profit to sort out other "wishful thinking". Jenga bandari Tanga, Mtwara, na imarisha ya Dar (iko connected na Railway - a major bonus kwa kuvutia nchi jirani). then imarisha viwanja vya ndege DAR, Mwanza, KIA na Mbeya. Hizi zote ni strategic locations. Hapa utatengeza pesa bila shaka na tumia faida kujenga mambo mengine huko Bagamoyo etc etc. Lakini kwa mtindo huu ni sawa na mkulima kula mbegu - tusitegemee mavuno!

Mkubwa umesema vizuri, problem jamaa wanakimbizana na muda wa kumaliza vipindi vya uongozi wao. Itakuwa busara kwenye katiba mpya kukawekwa sheria yenye provision ya kushitaki viongozi kama hawa. Na nyie wabunge mnao elewa masuala mlikuwa wapi hili likapita kwenye bajeti. Nina shaka kama wakina jairo hawako kila wizara.

Mambo mengine muyaone na kuyakomalia jambo la kutapaya raslimali kama hili msilione, hata kuna namna si bure. Tunaomba mtueleze hii imekaa je?
 
Kumbuka, bandari ya Dar Es Salaam ipo karibu kabisa na katikati ya jiji na pia ipo sehemu ambayo kuongezeka ukubwa ni tatizo na pia njia ya meli kufikia bandari ina kina cha maji ambacho hakikidhi kupitisha meli kubwa za kisasa. Tukitaka tusitake bandari mpya ni lazima ijengwe, Jee, mlitaka ikajemgwe Kilimanjaro?

Kuhusu uwanja wa ndege, hali ni hiyo hiyo, uwanja umeshakuwa mdogo kwa matumizi ya kisasa na upelekwe wapi? Bagamoyo ni KM 63 tu kutoka mjini Dar. Ni perfect choice kufanywa kuwa satellite city ya Dar. au mlitaka uwanja upelekwe Karatu?

Nafikiri huna habari pale DSM Int. Airport inajengwa Terminal III na parallel runway, south of the existing runway. "Usafishaji" kwajili ya Terminal III(East of Terminal II) ushafanywa na kwajili ya parallel runway zoezi linaendelea.
Issue ni kwamba kuna three parallel Airport upgrading zinaendelea.

Zanzibar (35km ya prospective Bagamoyo Int. Airport), DSM na hiyo ya prospective Bagamoyo Int. Airport.
 
Pigeni politike lakini bandari ya dar ni ndogo na sio competitive maana mombasa wanapiga bao wakati nyie mnataja majina, congo ni soko kubwa sana kwa bandari ya bongo hakikisheni hampotezi hii business opportunity. Na ndio maana inaunganishwa na sumbawanga ili kuwashika wacongo na kuondosha urasimu wa wazambia kutokea lubumbashi.

Maendeleo sio migodi na kilimo tu kama mnavyotaka tuamini, tanzania itoe service kwa nchi jirani itapiga hatua fasta. ****** mengine mnamuonea tu, barabara ya dar mbeya tunduma iboreshwe zaidi ya hapa manake iko poa mpaka iringa.
 
Kumbuka, bandari ya Dar Es Salaam ipo karibu kabisa na katikati ya jiji na pia ipo sehemu ambayo kuongezeka ukubwa ni tatizo na pia njia ya meli kufikia bandari ina kina cha maji ambacho hakikidhi kupitisha meli kubwa za kisasa. Tukitaka tusitake bandari mpya ni lazima ijengwe, Jee, mlitaka ikajemgwe Kilimanjaro?

Kuhusu uwanja wa ndege, hali ni hiyo hiyo, uwanja umeshakuwa mdogo kwa matumizi ya kisasa na upelekwe wapi? Bagamoyo ni KM 63 tu kutoka mjini Dar. Ni perfect choice kufanywa kuwa satellite city ya Dar. au mlitaka uwanja upelekwe Karatu?
Kwa kuwa miundombinu ya kulekea bara ambako mizigo mingi huelekea ni hafifu, hata kama tutajenga bandari kubwa sana bagamoyo kama outlets zitakuwa mbovu, watu watakimbilia mombasa. Bandari hiyo nayo itajaa na kusababisha usumbufu uleule unaopatikana Dar.

Suala la uwanja wa ndege: je ni lazima ujengwe sasa? Tumeona dar airport ikipanuliwa hivi karibuni, je ni lazima kujenga uwanja mwingine mkubwa just 80 km? Hatuna vipaumbele immediate zaidi ya hilo?

Shule za kata, Reli ya kuelekea bara, dawa hospitalini, mikopo ya elimu ya juu nk. Tusije kujikuta tunajenga uwanja ambao hata ndani ya miaka 10 unakuwa ni white elephant.
 
Pigeni politike lakini bandari ya dar ni ndogo na sio competitive maana mombasa wanapiga bao wakati nyie mnataja majina, congo ni soko kubwa sana kwa bandari ya bongo hakikisheni hampotezi hii business opportunity. Na ndio maana inaunganishwa na sumbawanga ili kuwashika wacongo na kuondosha urasimu wa wazambia kutokea lubumbashi.
Maendeleo sio migodi na kilimo tu kama mnavyotaka tuamini, tanzania itoe service kwa nchi jirani itapiga hatua fasta. ****** mengine mnamuonea tu, barabara ya dar mbeya tunduma iboreshwe zaidi ya hapa manake iko poa mpaka iringa.

Kama mnahujumu ya tanga ili mjustify kujenga hii ya bagamoyo kwenu why mombasa wasipete.

Mkiambiwa mnabiashara za malori ya kwenda congo mnajibu simple sisi wabaangaizaji tu tunamiliki corolla. Watu wakiconclude mnafanya mamuzi ya kuigharimu nchi na wananchi wengine kwa manufaa ya biashara zenu, mnalalama mnatuonewa wivu. Lakini sishangai Jana nimemuona Mtoto wa gaddafi anaitwa hamad (mtanisahihisha) akilalala kuwa anaonewa, eti yeye haja wahi shika nafasi yoyote iwe ya kijeshi au serikali ya baba yake.

Endeleni kusema mnamuonea wakati kuonewa kwa kweli kwaja ku njiani. Hizi familia za madikteta wa afrika zina mambo mengi mno ambayo ni common Kama hili la kulalamika kuonewa).
 
You are stupid,hatuna regional or state government.Hela zote zinazokusanywa mikoani zinaenda Dar !!!!!!!
 
Hivi hapa Logic hipo wapi

Bagamoyo Hipo kati ya Dar es Salaam na Tanga, na Kote kuna Bandari Kubwa, kama waliona ya Dar imebana kwa nini wasingeiendeleza ya Tanga na kuipanua? kuliko kupoteza pesa kwa kufuata matakwa binafsi?
katika mpango wa mji mpya wa kigamboni,bandari wamepewa eneo lote la vijibweni kwa ajili ya upanuzi wa bandari,...tunaye rais selfish and bogus,..kashajua watz hawamkubali hivyo kaamua kuacha legacy kwao,.ironically nyerere hakupendelea kwao na alipendwa tz nzima hadi butiama..oops kidogo nisahau,.EPZ inajengwa bagamoyo na ipo kwenye hatua za mwisho...
hadi ridhiwan kapewa kipaumbele...by the time he leave the office,HAZINA would be shillingless
 
White elephant ni KIA ambapo wahusika hawataki hata kuuzungumzia manake hakufikia malengo yaliyokusudiwa na mnajua kabisa kwa nini ulijengwa hapo.

Bahati mbaya uko kwa untouchables ambao walitumia vibaya convincing power yao sasa leo unakodishwa kwa dola buku kuwanyoshea kidole mnaogopa. Ungejengwa mwanza au mbeya tungepata dola kibao msilazimishe tufikiri the same way.
 
Hivi Mwanza kwa utajiri mlio nao mikoa hiyo, kinawashinda nini kujenga uwanja wa ndege kupitia bajeti zenu za mkoa? mpaka mngoje Serikali kuu iwafanyie kila kitu? wacheni kuwa legelege, wakati wa kufanyiwa kila kitu na Serikali umepitwa na wakati.

Wale wale mnaofikiri kwa kutumia masaburi, na siku serikali ikiruhusu kila mkoa utumie mapato yake ninyi wazaramo mtajuta kuzaliwa maeneo yenu. Ndio mtakapogundua bandari na kiwanja cha ndege hakiwezi kujengwa kwa mapato ya mananasi. ngongongaf kabisa!
 
Ukweli ni kuwa Plan hizi hazina strategies za ukweli katika kulijenga taifa hili kwa dhati,kwani badala ya kutoa vipaumbele kwa bandari zilizopo za Dar,Mtwara na Tanga pamoja na Viwanja vya ndege tulivyonavyo vya Dar,Mwanza,Mbeya na Kilimanjaro. Sasa serikali inaonekana kwenda mrama kwa kubuni vitu ambavyo vitaididimiza nchi kwani Bagamoyo Kunaniii!!!!!!!!!!!!
 
Tatizo lingine Pwani hakuna workforce, they are not hardworkers na <font size="4">HAWAWEZI </font>kazi za shuruba
kwani waarabu wanaweza kazi za shuruba,mbona wameendelea?katika dunia ya leo hatutegemei kazi za shuruba ili uwe na maendeleo.kama workforce ni ndogo basi watu kutoka bara waalikwe kwenda bagamoyo kwa wingi ili kufanya kazi za suluba!
 
nakumbuka kihistoria wajerumani mji wao wa kwanza kuupenda uwe makao makuu ulikuwa ni bagamoyo. lakini kina cha bahari kiliwashinda na ndi sababu ya wao kuhamia dar.ni bora watu wote wa kurasini mpaka kongowe yote kupitia kigamboni liwe sehemu ya bandari serikali ijipange kutanua taratibu kuliko bagamoyo.mipango mizuri inaweza kutengenezwa huku kuliko huko
 
<br />
<br />
mkuu ingekuwa hivyo kahama na shinyanga kungekuwa kama south afrika.. ndio maana kuna tra ndugu..

Nadhani Watanzania wengi mmekosa kuelewa maana ya kuhamishwa madaraka kutoka Serikali kuu kwenda Serikali ndogo.

Lazima kuwe na ubunifu wa vyanzo vya fedha ama kutoka mapato ya manispaa au ubunifu wa kutafuta wawekezaji. Serikali kuiwachia ibebe mizigo yote ni upunguani.

Dhanna ya utawala wa kupangiwa mambo yenu kutokea Serikali kuu ndio inayowarudisha nyuma Watanzania wengi, sasa tufikirie namna ya kujiendeleza wenyewe pale tulipo. Kwa sasa kila kitu ni biashara, sioni kuna sababu ipi ya kutokuwa wabunifu wa kuongeza mapato kwenye manispaa zetu na badala ya kujenga stendi za mabasi tuanze kuwekeza kwenye viwanja vya ndege ambavyo vina faida kubwa kuliko stendi za Taxi na mabasi. Kama hatungoji Serikali kuu katika kujenga stendi za mabasi na taxi kwanini tungoje Serikali kuu katika kuwekeza kwenye stendi za ndege?
 
Mh Zomba kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kujenga bandari mbili Dar es salaam, economically,geographically and strategically it makes no sense at all, ni ujinga unaweza kushangaa sana decision makers wanafikiri nini. Bandari ya Dar es salaam peke yake inatosha sana kwa Tanzania kama uswahili utapungua bandarani. Kama upakuaji na utoaji wa mizigo utafanywa vizuri sidhani kama kutakuwa na tatizo.

Dar es salaam Airport ikiwa upgraded na kuruhusu denge tatu kutua kwa wakati mmoja, hakuna haja ya kujenga uwanja mwingine.

Ni busara kujenga uwanja mzuri Mwanza, Mbeya na Kigoma, na kuboresha bandari ya Tanga. Kuwekeza Dar kupita kiasi ni tatizo, ni hatari na hakuna faida kubwa na manufaa kwa nchi.

kwani bagamoyo ni dar....masaburi yanafanya kazi sasa
 
<br />
<br />

vipi kuhusu bandari ya mtwara na tanga pamoja na zanzibar na je uwanja wa KIA kwa nini hivi visiendelezwe kama kigezo ni kina na ukubwa pamoja na upanuzi wa hicho kiwanja..

Kupanga ni kuchaguwa.
 
Back
Top Bottom