New International Airport and Port in Bagamoyo; hivi ni vipaumbele sahihi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

New International Airport and Port in Bagamoyo; hivi ni vipaumbele sahihi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ibrah, Aug 22, 2011.

1. Ibrah

Ibrah JF-Expert Member

#1
Aug 22, 2011
Joined: Mar 22, 2007
Messages: 2,721
Likes Received: 36
Trophy Points: 145
Nimepitia Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi na nimeshangaa sana pesa nyingi zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Bandari mpya na Uwanja wa ndege wa Kimataifa huko Bagamoyo, kilometa 80 tu kutoka Dar ambako kuna Bandari kuu yetu inayolegalega na Julius Nyerere Int Airport.

Wabunge walipiga sana kelele kuwa Reli ya Kati haijatengewa fedha za kutosha na imetelekezwa, ajabu hawakusema kitu kuhusu haya matumizi ya Ujenzi wa Uwanja wa Ndege na Port mpya Bagamoyo.

Je, twahitaji miradi hiyo Bagamoyo kwa sasa?

2. spencer

spencer JF-Expert Member

#2
Aug 22, 2011
Joined: Nov 25, 2010
Messages: 2,792
Likes Received: 1,337
Trophy Points: 280
GreatThinkers,
Sie watu wa Mwanza tunamwangalia kwa hasira mbaya, tunapata tabu sana Airport yetu iko kama Shule ya kata. JK ni mtu wa matanuzi tanuzi haangalii wapi pana umuhimu.

wee ngoja yeye anazeeka sie tunakua, ipo siku watajutia maamuzi hao tatanishi.

3. Ibrah

Ibrah JF-Expert Member

#3
Aug 22, 2011
Joined: Mar 22, 2007
Messages: 2,721
Likes Received: 36
Trophy Points: 145
Spencer, ile treni na reli yetu ya Mjerumani wameitelekeza, sasa wanadhani kule kwetu mwisho wa Reli sijui hiyo Bandari ya Bagamoyo na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa vitatusaidia vipi kufika Mwanza na Kigoma.

Ingekuwa heri kama pesa za hiyo miradi zingeimarisha Reli yetu ya Kati, na Bandari ya Tanga kuliko Bandari na Uwanja wa Ndege Bagamoyo.

Utitiri wa Viwanja vya Ndege na Bandari ndani ya Kilometa 100 havina faida ya maana kwa nchi yetu, tulipaswa kuimarisha bandari na viwanja vya ndege tulivyonavyo.

4. zomba

zomba JF-Expert Member

#4
Aug 22, 2011
Joined: Nov 27, 2007
Messages: 17,081
Likes Received: 49
Trophy Points: 0
Hivi Mwanza kwa utajiri mlio nao mikoa hiyo, kinawashinda nini kujenga uwanja wa ndege kupitia bajeti zenu za mkoa? mpaka mngoje Serikali kuu iwafanyie kila kitu? wacheni kuwa legelege, wakati wa kufanyiwa kila kitu na Serikali umepitwa na wakati.

5. pangalashaba

pangalashaba JF-Expert Member

#5
Aug 22, 2011
Joined: Jan 10, 2011
Messages: 1,084
Likes Received: 881
Trophy Points: 280
Plus Bagamoyo University.. Huyo ndo ****** zuzu. Mtwara,Tanga,Musoma,Kigoma bandari zipo hoi! Reli ya kati kwishney.... Hv hz ni akili,masaburi au matope? Aaaaaaaarghh....

6. andrewk

andrewk JF-Expert Member

#6
Aug 22, 2011
Joined: Apr 13, 2010
Messages: 3,103
Likes Received: 55
Trophy Points: 145
Huo mradi utakufa kabla jk hajatoka madarakani

7. zomba

zomba JF-Expert Member

#7
Aug 22, 2011
Joined: Nov 27, 2007
Messages: 17,081
Likes Received: 49
Trophy Points: 0
Kumbuka, bandari ya Dar Es Salaam ipo karibu kabisa na katikati ya jiji na pia ipo sehemu ambayo kuongezeka ukubwa ni tatizo na pia njia ya meli kufikia bandari ina kina cha maji ambacho hakikidhi kupitisha meli kubwa za kisasa. Tukitaka tusitake bandari mpya ni lazima ijengwe, Jee, mlitaka ikajemgwe Kilimanjaro?

Kuhusu uwanja wa ndege, hali ni hiyo hiyo, uwanja umeshakuwa mdogo kwa matumizi ya kisasa na upelekwe wapi? Bagamoyo ni KM 63 tu kutoka mjini Dar. Ni perfect choice kufanywa kuwa satellite city ya Dar. au mlitaka uwanja upelekwe Karatu?

8. zomba

zomba JF-Expert Member

#8
Aug 22, 2011
Joined: Nov 27, 2007
Messages: 17,081
Likes Received: 49
Trophy Points: 0
Dua ya kuku, mradi umeshaanza, for your information!

9. ndetichia

ndetichia JF-Expert Member

#9
Aug 22, 2011
Joined: Mar 18, 2011
Messages: 27,641
Likes Received: 236
Trophy Points: 160

mkuu ingekuwa hivyo kahama na shinyanga kungekuwa kama south afrika.. ndio maana kuna tra ndugu..

10. ndetichia

ndetichia JF-Expert Member

#10
Aug 22, 2011
Joined: Mar 18, 2011
Messages: 27,641
Likes Received: 236
Trophy Points: 160

vipi kuhusu bandari ya mtwara na tanga pamoja na zanzibar na je uwanja wa KIA kwa nini hivi visiendelezwe kama kigezo ni kina na ukubwa pamoja na upanuzi wa hicho kiwanja..

11. ndetichia

ndetichia JF-Expert Member

#11
Aug 22, 2011
Joined: Mar 18, 2011
Messages: 27,641
Likes Received: 236
Trophy Points: 160

kudos mkuu pangalashaba..

12. Ibrah

Ibrah JF-Expert Member

#12
Aug 22, 2011
Joined: Mar 22, 2007
Messages: 2,721
Likes Received: 36
Trophy Points: 145
Zomba, Uwanja wa Ndege Dar uko unapanuliwa na mabilioni yameshatumika; sasa kulikuwa na haja gani kupanua Uwanja wa Dar? Bandari ya Dar kutokuwa na huo uwezo wa kupokea meli za Kisasa si kweli, meli za kisasa ni zipi na zina nini kushindwa kutia nanga Dar? Kwa nini tusiimarishe Bandari ya Tanga ambapo kuna Reli ambavyo vingeimarishwa ili vitumike kupokea na kusafirisha mizigo kwenda Bara na nchi jirani?

13. T

Tetere Enjiwa JF-Expert Member

#13
Aug 22, 2011
Joined: Aug 21, 2011
Messages: 217
Likes Received: 1
Trophy Points: 0
Si kuna uliokuwa unajengwe huko mkuranga ambao inasemekena eneo lilishapatikana na wenyeji walishalipwa fidia umefika wapi? kulikua na sababu gani za msingi kupanua huu wa mwalimu Nyerere ambao watu wamehamishwa na kulipwa fidia zilizo jaa dhuluma tupu, ule wa Mbeya hivi sasa unahudumia ndege ngapi kwa mwaka na amini umeisha ndio sababu tunafikiria kujenga mwingine au ndio akili alizo zishangaa mstahiki Meya baada ya kukerwa na mauzauza ya Dar.

14. K

KVM JF-Expert Member

#14
Aug 22, 2011
Joined: Feb 11, 2011
Messages: 1,814
Likes Received: 336
Trophy Points: 180
The priority for this country at the moment is the generation of electricity not new airports or harbours. We need them, but surely they cannot be the ones which should make our leaders spend sleepless nights! The way we dissipate our efforts clearly shows how our leaders are clueless about the country's priorities. We need power immediately, almost at any cost.

Something which I also do not agree with our our leaders is the way they have been demonising generation of power using our water resources. Our politicians are making every Tanzanian believe that hydro-electric projects are a waste of time. I know nothing about power generation but I have reason to believe that in the medium term Tanzania will need to generate power using medium and large scale hydro-electric projects. This can be done by concentrating on rivers which flow into the Kilombero water basin.

I know that Mtera and Kidatu have let us down, but we should also do a research which this is the case. River Ruaha flows into an arid region, Ruaha National Park, Dodoma and parts of Iringa.Most of the river tributaries that feed into Mtera are heavily used for irrigarigating huge paddy fields. Silting could also be another problem although some officials tend to discount it.

Coal is also going to be another major resource in power generation in Tanzania. I beleieve it will overttake all other sources of power in the long run.

15. F

FJM JF-Expert Member

#15
Aug 22, 2011
Joined: Apr 11, 2011
Messages: 8,088
Likes Received: 90
Trophy Points: 145
Hili la bandari naomba nitoe maoni ya kiutalaam zaidi. Bagamoyo hakuna sehemu yenye kina kwa meli kutia nanga. Maji hujaa na kuzama for almost a kilometa! Itabidi waingie gharama kubwa kuchimba na kuhakikisha kuwa kina cha maji kiko kwenye level ya meli kutia nanga. It is a mad business kufikiria kujenga bandari Bagomoyo and I can tell you kuna watu hawana mbavu kwa kutucheka! Kwa nini wasiboreshe Bandari ya Dar es Salaam? Ni cheaper kuboresha bandari ya Dar kuliko kujenga mpya tena sehemu ambayo physical location inahitaji kazi ya ziada!

Kumbuka strategically Bandari na Reli hapa Dar viko karibu, na hivyo hata ungetaka kuuza idea ya nchi jirani kupitishia mizigo Dar idea itaenda vizuri maana watapakuwa makontena na kuweka kwenye meli. Gharama obviously zitakuwa chini kuliko kuwa na Bandari Bagamoyo then walete makontena Dar kwa kusafirisha!

La mwisho, Dar ni commercial city, Dodoma ndio wanatakiwa hawa wanasiasa wahamie huko hivyo ni vizuri kuimarisha miundo mbinu Dar kama kweli tunataka kushindana na Kenya. Mambo ya kujenga vitu vipya ni fikra finyu kwa nchi maskini kama yetu. Tunalishwa na wafadhili lakini bado tunashindwa kupanga!

16. afroPianist

afroPianist Member

#16
Aug 22, 2011
Joined: Nov 3, 2010
Messages: 86
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Anajitengenezea escape paradise and a 'little personal ride'...aaah sweet joys of retirement!

17. mchemsho

mchemsho JF-Expert Member

#17
Aug 22, 2011
Joined: Jun 8, 2011
Messages: 3,158
Likes Received: 143
Trophy Points: 160
Barabara ni mbovu sana so ameaumua ku base kwenye maji na kupasua anga kama kawa

18. zomba

zomba JF-Expert Member

#18
Aug 22, 2011
Joined: Nov 27, 2007
Messages: 17,081
Likes Received: 49
Trophy Points: 0
Angekwenda kujenga kwenye masaburi yenu mngeona ni sawa tu.

19. zomba

zomba JF-Expert Member

#19
Aug 22, 2011
Joined: Nov 27, 2007
Messages: 17,081
Likes Received: 49
Trophy Points: 0
Kama alivyojijengea Nyerere kule Butiama?

20. Msarendo

Msarendo JF-Expert Member

#20
Aug 22, 2011
Joined: Jan 29, 2011
Messages: 9,136
Likes Received: 3,328
Trophy Points: 280
Mkwère anawakumbuka wakwere.

Loading...