New Habari mambo si shwari mshahara bado!

pombe

Member
Feb 2, 2010
12
0
Inasemekana ndani ya kampuni hiyo mambo si shwari kutokana na kwa miezi kadhaa sasakushindwa kuwalipa wafanyakazi mishahara kwa wakati ( tarehe 46) na pia kukabiliwa na migogoro kadhaa ya ki utawala hata kupelekea baadhi ya wafanyakazi kufutwa kazi.

Suala la mshahara linaonekana kuwa sugu sasa na kufikia leo hakuna hata mmoja wa wafanyakazi aliyelipwa. Mmiliki wa kampuni hiyo RA ameamua kuwaacha wadanganyika wataabike na kubaki kuwa ombaomba na wanatusumbua mtaani kwa mizinga.

Mwenye habari zaidi atujuze!
 
Duh! buguruni kama una uhakika hiyoo si dalili nzuri. Kampuni kuanza kushindwa kulipa wafanyakazi ni hatari. Nawapa pole wana Habari wasikate tamaa
 
Kuna fununu kuwa Muungwana kamtosa RA, pigo la mwisho linashushwa Dodoma next week kwenye NEC ambako watuwake watapigwa paranja.

Muhingo kaaga rasmi, Ezekiel Kamwagwa juzi nimemsoma Mwanahali, The African sasa ni weekly, hivyo ni kweli mambo si shwari.

Good news ni kuwa huku Habari Corp. ikitikisika, tangu tarehe 1/02/2010, magazeti yao wameyapa facelift ya nguvu, wamebadili muonekano, layout na design, pia wanapiga full color kurasa zote.
 
Mwenye habari zaidi atujuze!

Pombe, kwakuwa wewe mwenyewe umeanzisha habari ukiwa huna uhakika. Basi haya ni majungu na hayataruhusiwa JF. Topic inafungwa. Usifanye hivi tena hapa, kuja ukiwa na uhakika siku nyingine, hii inatuchafulia jina hapa!
 
Kuna fununu kuwa Muungwana kamtosa RA, pigo la mwisho linashushwa Dodoma next week kwenye NEC ambako watuwake watapigwa paranja.

Muhingo kaaga rasmi, Ezekiel Kamwagwa juzi nimemsoma Mwanahali, The African sasa ni weekly, hivyo ni kweli mambo si shwari.

Good news ni kuwa huku Habari Corp. ikitikisika, tangu tarehe 1/02/2010, magazeti yao wameyapa facelift ya nguvu, wamebadili muonekano, layout na design, pia wanapiga full color kurasa zote.
Pasco,

You have my respect mkuu. Can you give me some hints kwanini topic hii isifungwe? Mwanzisha topic kaianzisha kidaku, haipendezi hata kidogo! Just PM me mkuu
 
Hawa ni wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania na Rai ila mpaka leo hii mshahara haujalipwa na haijulikani kadhia hiyo itaisha lini. Hii imetokana na kampuni kutofanya vizuri kibiashara na tatizo hili limejirudia kwa miezi minne mfululizo sasa.

Kampuni hii kongwe ya habari inaelekea wapi?
 
poleni wahusika,kila kampuni huzaliwa,hukua na hatimaye hufa na mkiwa na bahati inaweza kufufuka,lakini kwa soko la kazi za kampuni hiyo kwa sasa mmh,labda mbadilike.
 
Kaka hiyo ndiyo recession ambayo majuu wanalia nayo.
Kwetu hapa production cost [umeme,karatasi,mishahara,kodi etc ni kubwa matangazo ya biashara yamepungua sana [chanzo kikuu cha mapato]-wateja wao wakuu nao wamepunguza matumizi [mojawapo matangazo]
Tatizo jingine ni electronic media [watu wengi sana wanasubscribe] hivyo kufanya wateja wa magazeti kupungua.
Suluhisho hapa sijui wapate subsidy toka serikalini [lakini hata hivyo ni magazeti gani yapate- ya udaku jee]
suluhisho lingine ni ku merge kampuni za magazeti
Vinginevyo ni vigumu kusurvive
 
Mbali na gharama za uchapishaji kupanda ukweli ni kwamba magazeti ya New habari Corp. hayauziki na hilo wanalijua mdio maana hata sasa Gazeti la The African limeanza kutolewa mara moja kwa wiki badala ya mara sita. Rai ndio kabisaaaa. Ni dhairi kwamba umma umeyakataa magazeti ya New Habari Corp. kutokana na historia ya mwekezaji mkuu katika kampuni hiyo. Hiyo ndio nguvu ya Umma.
 
boss wenu Rostam wa azizi anawaambiaje?za EPA zilishakwisha au ndo anandunduliza za uchaguzi.
 
Fununu, accounts ziko held pending uamuzi wa kumsulubu, atatolewa kafara ya Kagoda kukisafisha chama, mambo yote ni wiki hii mjini Dodoma,
Inatarajiwa ile mtu 4 inayochafua chama, pia itawekwa kando kiuongozi na kubakia kama wanachama waaminifu.
 
Hawa ni wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania na Rai ila mpaka leo hii mshahara haujalipwa na haijulikani kadhia hiyo itaisha lini. Hii imetokana na kampuni kutofanya vizuri kibiashara na tatizo hili limejirudia kwa miezi minne mfululizo sasa.

Kampuni hii kongwe ya habari inaelekea wapi?

Poleni!
Wanaojua kusoma dalili za nyakati, wamesoma, alianza Rose kachomoka, Ezekiel kajisalimisha 'Mwanahalisi' japo ni kuruka majivu. Muhingo ndio tetesi zake zinaendelea.Bado tuu hanjajua kinachoendelea!?.
 
Fununu, accounts ziko held pending uamuzi wa kumsulubu, atatolewa kafara ya Kagoda kukisafisha chama, mambo yote ni wiki hii mjini Dodoma,
Inatarajiwa ile mtu 4 inayochafua chama, pia itawekwa kando kiuongozi na kubakia kama wanachama waaminifu.

Pasco,

Hii Fununu ingefaa ianzishiwe kamba yake mzee........!
 
Fununu, accounts ziko held pending uamuzi wa kumsulubu, atatolewa kafara ya Kagoda kukisafisha chama, mambo yote ni wiki hii mjini Dodoma,
Inatarajiwa ile mtu 4 inayochafua chama, pia itawekwa kando kiuongozi na kubakia kama wanachama waaminifu.

Pagumu hapo.....mazee waweza taja hizo mtu 4.......!
 
NATOA HOJA:

TUWAPITISHIE BAKULI HAWA NI NDUGU ZETU WASIGEUKE OMBA OMBA. Naomba kuunwa mkono ndugu wanajamii. Tusifanye mzaha
 
poleni wahusika,kila kampuni huzaliwa,hukua na hatimaye hufa na mkiwa na bahati inaweza kufufuka,lakini kwa soko la kazi za kampuni hiyo kwa sasa mmh,labda mbadilike.

muwe waangalifu msife, pamoja naye. lakini mkulima akiona shamba halizalishi huliacha. Na mfanyabiashara pia akiona bidhaa fulani haina soko huachana nalo. Ninyi ntalia lia mpaka lini...!!!!??????
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom