New Habari Corp ni dalili nyingine ya mgogoro ndani ya CCM

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,182
307
Nimesoma kwa mshangao mkubwa makala kwenye gazeti la Mtanzania, Mtanzania hili hili ambalo mwaka mmoja uliopita lilikuwa sauti ya CCM sasa ndilo linaishambulia CCM kwa nguvu zote.

Kuna nini kimetokea? Au ndiyo mikakati ya kumvua Kikwete uenyekiti wa chama? Au Wamezisoma alama za nyakati wakaona hawawezi kuenendelea kwa kuendelea kuwa sauti ya chama kinachokufa?
 
Mkuu karibu makala zote za Mtanzania ya leo ni anti-CCM, utadhani unasoma MwanaHalisi
 
Habari cooperation si mali ya Rostam?itabidi tumwulize inakuaje tena anakishambulia chama chetu.
 
Siku watu mtaelimika ndipo Tanzania itabadilika. ukifanya mazuri usemwe kwa mazuri. Ukifanya mabaya ukosolewe, na usipoelewa kakufilie mbali. CCM sio Tanzania, waliikuta. Tanzania ni ya watanzania wote.
 
Kule igunga Mtanzania walitoa makala kuwa ccm kwa miaka yote haijafanya kitu igunga na mwandishi akasahau kuwa igunga kwa muda wa miaka 20 ilikuwa chini ya RA mmiliki wa gazeti hilo.Huu ni mwanzo wa mwisho wa habari corp,raiamwema wako mbioni kuanzisha gazeti la kila siku na redio,watu makini kwa kila nyanja ya habari.Waandishi deiwaka wa RA watazimiwa baharini.
 
RA ana agenda yake ya kumsalimisha swahiba wake na partner wake EL katika hii ya magamba kwa hiyo lazima aweke uhasi katika chama iwatishe watu wanaotaka kufanya haya maamuzi na kummulika zaidi JK ni kumsalimisha EL huitaji kuwa political scientist au jasusi kujua azma hii
 
Kule igunga Mtanzania walitoa makala kuwa ccm kwa miaka yote haijafanya kitu igunga na mwandishi akasahau kuwa igunga kwa muda wa miaka 20 ilikuwa chini ya RA mmiliki wa gazeti hilo.Huu ni mwanzo wa mwisho wa habari corp,raiamwema wako mbioni kuanzisha gazeti la kila siku na redio,watu makini kwa kila nyanja ya habari.Waandishi deiwaka wa RA watazimiwa baharini.

Good idea. Binafsi waeke vyote, ila ntasuuzika nafsi ntapoona tv ya ku counteract umbea na upuuzi wa tbc, channel 10 na tv nyingine ambazo ni makuwadi wa CCM
 
Rostam na timu yake (akina Bashe) walijua igunga inaenda upinzani, akasahau kuwa magamba ni hodari wa uchakachuzi. Sasa anakuja na plan b ambayo anadhani itasaidia kuiangamiza ccm. Uzuri ni kwamba vita ya panzi furaha ya kunguru, maana unapata 'mlo' bila kutoka jasho jingi, khaaa!
 
Mnafurahia huko ccm kukiwaka moto lkn mbona huko cdm sioni plan za ku take advantage ya hii hali?what is the plan?
 
nimesoma kwa mshangao mkubwa makala kwenye gazeti la mtanzania, mtanzania hili hili ambalo mwaka mmoja uliopita lilikuwa sauti ya ccm sasa ndilo linaishambulia ccm kwa nguvu zote.

Kuna nini kimetokea? Au ndiyo mikakati ya kumvua kikwete uenyekiti wa chama? Au wamezisoma alama za nyakati wakaona hawawezi kuenendelea kwa kuendelea kuwa sauti ya chama kinachokufa?

hapo kusema rostam hana ubia tena ccm. Tusubiri tuone mwisho wake ni nini.
 
Nimesoma kwa mshangao mkubwa makala kwenye gazeti la Mtanzania, Mtanzania hili hili ambalo mwaka mmoja uliopita lilikuwa sauti ya CCM sasa ndilo linaishambulia CCM kwa nguvu zote.

Kuna nini kimetokea? Au ndiyo mikakati ya kumvua Kikwete uenyekiti wa chama? Au Wamezisoma alama za nyakati wakaona hawawezi kuenendelea kwa kuendelea kuwa sauti ya chama kinachokufa?

Unafikiri wamefurahi Bosi wao Rostam kuvuliwa gamba?
 
Back
Top Bottom