New Habari 2006 Ltd washindwa kufikia muafaka na wafanyakazi 51 katika Tume ya Usuluhishi wa migogoro kazini (CMA)

Kamanda Mlo

Member
Feb 9, 2012
10
4
Dar es Salaam

WAFANYAKAZI 51 waliopunguzwa kazi na Kampuni ya New Habari 2006 Ltd wameshindwa kufikia muafaka na mwajiri wao katika Tume ya Usuluhishi wa migogoro kazini (CMA) Kanda ya Dar es Salaam.

Kampuni hiyo ambayo Ofisa Mtendaji wake Mkuu ni Mbunge wa Nzega Mjini na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ilipunguza wafanyakazi zaidi ya 100 Mei 31 mwaka huu katika kile kilichoelezwa kuwa ni kushindwa kujiendesha.

Shauri hilo Namba CMA/DAR ES SALAAM/KIN/504/2019 la Juni 28 mwaka huu lililokuwa likisikilizwa chini ya Msuluhishi wa Tume hiyo, Peter Mahindi, wafanyakazi wanamdai mwajiri wao, jumla ya Sh bilioni 2 ambazo zimetokana na madai ya malimbikizo ya mishahara na fidia kwa kuwaondoa kazini bila kufuata utaratibu wa kisheria.

Kampuni hiyo imeshindwa kueleza bayana kusudio la kuwalipa wafanyakazi hao stahiki zao kwa mujibu wa sheria za kazi.

Katika shauri hilo ambalo New Habari iliwakilishwa na Wakili, Neema Uisso kwa Tume hiyo alisema hawezi kuwalipa wafanyakazi hao mafao yao kama wanavyotaka.

“Sina offer yoyote niliyokuja nayo kutoka kwa mteja wangu”alisema Wakili Neema mbele ya Msuluhishi wa CMA, Peter Mahindi.

Akizungumza katika Ofisi za CMA Dar es Salaam muda mfupi baada ya shauri hilo kumalizika mwishoni mwa wiki, Mwakilishi wa wafanyakazi hao, Khamis Mkotya alisema msingi wa kesi hiyo ni kutokana na mwajili kuwapunguza kazini bila kufuata utaratibu pamoja na kuwalipa stahili zao ikiwamo malimbikizo ya mishahara ya zaidi ya miezi mitano.

“Sheria za kazi zinataka pande zote mbili, yaani mwajiri na mwajiriwa kutimiza wajibu wake, lakini sisi wafanyakazi wa NHL tumeitumikia kampuni hiyo kwa muda mrefu lakini tumeondolewa kazini bila kulipwa malimbikizo ya mishahara pamoja na stahili zingine tangu Januari hadi Mei mwaka huu.

“Katika vikao vya majadiliano vya kupunguza wafanyakazi walitueleza kwamba tungelipwa stahiki zetu zote hadi kufikia tarehe 15 Juni mwaka huu, lakini hadi muda huo ulipofika walishindwa kutekeleza ahadi yao.

“Baada ya hapo tuliwapelekea notisi ya siku saba kupitia kwa mwanasheria wetu ili jambo hili tulimalize mezani jambo ambalo hawakutaka kulifanya”alisema Mkotya.

Akifafanua zaidi Mkotya alisema kwa mara ya kwanza shauri hilo lilipangwa kusikilizwa CMA Julai 22 mwaka huu ambapo Wakili wa mwajiri Neema ambaye awali alijitambulisha kwa wafanyakazi kwamba ni mwanasheria kutoka Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu aliieleza Tume hiyo kuwa mteja wake (New Habari) yupo tayari kulipa stahiki nyingine bila fidia jambo ambalo lilipingwa na wafanyakazi hao kwa maelezo kuwa fidia haiepukiki kulingana na mazingira ya namna walivyoondolewa kazini.

Kutokana na hali hiyo Neema aliomba muda ili akashauriane na mteja wake kuhusu kipengele cha fidia.

Mkotya alisema usuluhishi huo uliendelea Agosti 16 mwaka huu kwa pande zote mbili ambapo msuluhishi alimtaka wakili wa New Habari kueleza hatua waliyofikia, ndipo Neema aliieleza Tume hiyo kwamba hakuja na ‘offer’ yoyote kutoka kwa mwajiri.

Kutokana na maelezo hayo, Mahindi alisema hatua ya kwanza ya usuluhishi wa shauri hilo imeshindikana na kuwauliza wafanyakazi endapo wataendelea mbele au la.

“Kutokana na hali hiyo, tumeamua kusonga mbele katika hatua ya pili ya Arbitration baada ya hii ya kwanza kushindikana.”alisema Mkotya.

Mwisho…..

Madai hayo ni pamoja na wakitaka mwajiri kuwalipa stahiki zao ikiwa ni pamoja na malimbikizo ya mishahara ya zaidi ya miezi mitano, kiinua mgongo pamoja na fidia kutokana na kupunguzwa kazi kinyume cha sheria na taratibu za kazi.

………………………………………………….
Alisema …………………………………………….
“KImsingi hiyo ndiyo sababu iliyotufanya twende kwenye vyombo vya usuluhishi wa kisheria kutafuta haki, hata hivyo kwakuwa mwajiri bado hajawa tayari kulipa stahiki zetu tumeamua kupeleka shauri hilo mbele ili lipate uamuzi wa kisheria.
“………………………………………..
Kampuni hiyo ambayo Mtendaji wake Mkuu ni Naibu Waziri wa Kilimo, Hussen Bashe ilipunguza wafanyakazi Mei 31 mwaka huu huku ikiahidi kwa maandishi kuwalipa stahiki zao ikiwa ni pamoja na malimbikizo ya mishahara,notisi ya mwezi mmoja, likizo kwa wafanyakazi ambao walikuwa bado hawajapata likizo ya mwaka.

Hata hivyo kampuni ya New habari ilishindwa kutekeleza ahadi hiyo badala yake iliamua kuwapa barua za kukatisha mikataba na kuwasimamisha kazi wafanyakazi hao bila kuwalipa chochote kama ilivyoahidi awali.

pic+bashe.jpg
 
Mh Bashe hili ni Dude limekuganda mheshimiwa embu fanya Uwalipe hawa ndugu stahiki zao pambana muheshimiwa hili lisikupe Doa la uongozi wako katika nchi chonde chonde fanya hima. Ikiwa shida ni kwa Rostam Aziz aisee ongea nae vizuri huyo ndugu alipe aisee hawa watu mi nawafahamu vizuri nimekuwa nikifanya nao kazi hapa na pale maisha yao sasa sio vyema yawapate yakuwapata aisee wakati muheshimiwa upo hai na una nguvu ya kuwasaidia embu fanya kuwalipa ndugu yangu. Wanachodai ni haki yao isitoshe wamefanya kazi miezi yote hiyo bila kulipwa na hukukuta hata pen ya ofcn kwako imeibiwa aisee hawa ni watu wema sana hawajakuibia wakavumilia njaa daahhh walipe muheshimiwa njaa mbaya na malalamiko ya binadamu juu yako ni mabaya zaidi maana hata ukeshe msikitini ukiswali swala zako zote hazipokelewi kwa kunyima haki za wanyonge fanya hima 2020 tukutane tena nzega kaka!!
 
Wale wafanyakazi wa BUSINESS PRINTERS LTD wanadai 300M kwa zaidi ya miaka 2 hawajalipwa hadi leo. Mahakama imetoa amri ya kukamata mali lakini wapi.

Zile mashine sijui nani wanatumia pale Business Printers, zingeuzwa wafanyakazi wangesha pata stahiki zao.
Dah wafanyakazi na familia zao wanateseka kweli.
Ee, Mwenyezi Mungu ingilia kati kama ahadi yako ilivyo kwenye Neno lako kitabu kile cha MALAKI 3:5, kwamba WEWE utakuwa shahidi mwepesi kwa anaye mdhulumu mfanyakazi.
 
Dar es Salaam

WAFANYAKAZI 51 waliopunguzwa kazi na Kampuni ya New Habari 2006 Ltd wameshindwa kufikia muafaka na mwajiri wao katika Tume ya Usuluhishi wa migogoro kazini (CMA) Kanda ya Dar es Salaam.

Kampuni hiyo ambayo Ofisa Mtendaji wake Mkuu ni Mbunge wa Nzega Mjini na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ilipunguza wafanyakazi zaidi ya 100 Mei 31 mwaka huu katika kile kilichoelezwa kuwa ni kushindwa kujiendesha.

Shauri hilo Namba CMA/DAR ES SALAAM/KIN/504/2019 la Juni 28 mwaka huu lililokuwa likisikilizwa chini ya Msuluhishi wa Tume hiyo, Peter Mahindi, wafanyakazi wanamdai mwajiri wao, jumla ya Sh bilioni 2 ambazo zimetokana na madai ya malimbikizo ya mishahara na fidia kwa kuwaondoa kazini bila kufuata utaratibu wa kisheria.

Kampuni hiyo imeshindwa kueleza bayana kusudio la kuwalipa wafanyakazi hao stahiki zao kwa mujibu wa sheria za kazi.

Katika shauri hilo ambalo New Habari iliwakilishwa na Wakili, Neema Uisso kwa Tume hiyo alisema hawezi kuwalipa wafanyakazi hao mafao yao kama wanavyotaka.

“Sina offer yoyote niliyokuja nayo kutoka kwa mteja wangu”alisema Wakili Neema mbele ya Msuluhishi wa CMA, Peter Mahindi.

Akizungumza katika Ofisi za CMA Dar es Salaam muda mfupi baada ya shauri hilo kumalizika mwishoni mwa wiki, Mwakilishi wa wafanyakazi hao, Khamis Mkotya alisema msingi wa kesi hiyo ni kutokana na mwajili kuwapunguza kazini bila kufuata utaratibu pamoja na kuwalipa stahili zao ikiwamo malimbikizo ya mishahara ya zaidi ya miezi mitano.

“Sheria za kazi zinataka pande zote mbili, yaani mwajiri na mwajiriwa kutimiza wajibu wake, lakini sisi wafanyakazi wa NHL tumeitumikia kampuni hiyo kwa muda mrefu lakini tumeondolewa kazini bila kulipwa malimbikizo ya mishahara pamoja na stahili zingine tangu Januari hadi Mei mwaka huu.

“Katika vikao vya majadiliano vya kupunguza wafanyakazi walitueleza kwamba tungelipwa stahiki zetu zote hadi kufikia tarehe 15 Juni mwaka huu, lakini hadi muda huo ulipofika walishindwa kutekeleza ahadi yao.

“Baada ya hapo tuliwapelekea notisi ya siku saba kupitia kwa mwanasheria wetu ili jambo hili tulimalize mezani jambo ambalo hawakutaka kulifanya”alisema Mkotya.

Akifafanua zaidi Mkotya alisema kwa mara ya kwanza shauri hilo lilipangwa kusikilizwa CMA Julai 22 mwaka huu ambapo Wakili wa mwajiri Neema ambaye awali alijitambulisha kwa wafanyakazi kwamba ni mwanasheria kutoka Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu aliieleza Tume hiyo kuwa mteja wake (New Habari) yupo tayari kulipa stahiki nyingine bila fidia jambo ambalo lilipingwa na wafanyakazi hao kwa maelezo kuwa fidia haiepukiki kulingana na mazingira ya namna walivyoondolewa kazini.

Kutokana na hali hiyo Neema aliomba muda ili akashauriane na mteja wake kuhusu kipengele cha fidia.

Mkotya alisema usuluhishi huo uliendelea Agosti 16 mwaka huu kwa pande zote mbili ambapo msuluhishi alimtaka wakili wa New Habari kueleza hatua waliyofikia, ndipo Neema aliieleza Tume hiyo kwamba hakuja na ‘offer’ yoyote kutoka kwa mwajiri.

Kutokana na maelezo hayo, Mahindi alisema hatua ya kwanza ya usuluhishi wa shauri hilo imeshindikana na kuwauliza wafanyakazi endapo wataendelea mbele au la.

“Kutokana na hali hiyo, tumeamua kusonga mbele katika hatua ya pili ya Arbitration baada ya hii ya kwanza kushindikana.”alisema Mkotya.

Mwisho…..

Madai hayo ni pamoja na wakitaka mwajiri kuwalipa stahiki zao ikiwa ni pamoja na malimbikizo ya mishahara ya zaidi ya miezi mitano, kiinua mgongo pamoja na fidia kutokana na kupunguzwa kazi kinyume cha sheria na taratibu za kazi.

………………………………………………….
Alisema …………………………………………….
“KImsingi hiyo ndiyo sababu iliyotufanya twende kwenye vyombo vya usuluhishi wa kisheria kutafuta haki, hata hivyo kwakuwa mwajiri bado hajawa tayari kulipa stahiki zetu tumeamua kupeleka shauri hilo mbele ili lipate uamuzi wa kisheria.
“………………………………………..
Kampuni hiyo ambayo Mtendaji wake Mkuu ni Naibu Waziri wa Kilimo, Hussen Bashe ilipunguza wafanyakazi Mei 31 mwaka huu huku ikiahidi kwa maandishi kuwalipa stahiki zao ikiwa ni pamoja na malimbikizo ya mishahara,notisi ya mwezi mmoja, likizo kwa wafanyakazi ambao walikuwa bado hawajapata likizo ya mwaka.

Hata hivyo kampuni ya New habari ilishindwa kutekeleza ahadi hiyo badala yake iliamua kuwapa barua za kukatisha mikataba na kuwasimamisha kazi wafanyakazi hao bila kuwalipa chochote kama ilivyoahidi awali.

View attachment 1185364
[/QUOT
Hawa wateule sidhani kama wanafanyiwa Vetting, pesa za mishahara umekula, pesa za mikopo ya Benki Barclays umekata ktk mishahara kukupeleka umetuachia kesi, pesa za NSSF umekula unakata ktk mishahara lakini hapeleki, ulipaswa uwe gerezani na sio Wizarani, shukuru nchi zetu haki sio mahala pake
 
Back
Top Bottom