New Dar Master Plan to render millions homeless

Mliojenga Maeneo yasiopimwa, na Maeneo yaliokatazwa, better read this 👇👇



SOURCE: GUARDIAN ON SUNDAY


Naona sasa kuwa watanzania ni vilaza inaonekana Dhahiri-dar ina watu milioni 4.5 unataka kubomoa makazi ya watu milioni 3.9 -GOoDLUCK WITH THAT
 
Hiyo ni simply impractical na haiwezekani, angalia Tabata almost wanasema itakuwa ya wafanyakazi tena taasisi chache na lundo la wafanyakazi wengine waishi wapi??

Pili plan hii inanikumbusha walioenda kuplan Kigamboni master plan ilikuwa nzuri kweli ila tuna hela za kulipa fidia Dar nzima ili tuipange upya au tunataka kuanzisha mgogoro mwingine kama wa Kigamboni??

Plan ni nzuri ila haitekelezeki labda ingekuwa inatekelezwa in peace meal
Mkuu usemacho ni ukweli mtupu. Nafurahi kupata comment kutoka wataalam wa ardhi kama wewe
 
Pamoja na dhamira njema ya kufanya yote haya,gharama hii ataibeba Magufuli na CCM yake mwaka 2020 huku mijini.

Msimtishe hakuna cha gharama wa nini kwani hata sasa CCM haina kitu mijini hivyo ndio fursa kubwa kwao kunyoosha maana hawana cha kupoteza 2020
 
Mlikua mnapiga kelele CCM mbaya mkasahau mnakaa kwenye maeneo hatarishi ngoja wawanyooshe kwanza
 
@MKILINDI ingelikuwa vizuri kutengeneza master plan kuweka satelight city nzuri nje ya mji ili shughuli nyingi na maofisi ya Serikali yaamie huko!!
Serikali ihamishie ofisi zake nyingi na wizara zake Dodoma, kama plan ya awali, kupunguza msongamano ktkt ya jiji!!
Kuliko kuwatia umasikini watu ambao hawana makosa kujenga bila plan maana haikuwepo, wala hawakuambiwa!!
Wengine walipewa vibali kwa makosa!!
 
Kuna tatizo la kimfumo hapo lazima liangaliwe. Serikali ya Jamhuri ya Muungano mipaka yake kwenye kupanga miji ikoje. Mamlaka za serikali za mitaa hazimiliki ardhi, lakini madiwani ndiyo wenye kumiliki miji, jee vikao vyao havina mamlaka ya kisheria ya kuhalalisha ujenzi unaoitwa "Uvamizi" na Serikali ya JMT? Serikali za mitaa zenyewe haziwezi kushitakiwa na hao wanaoitwa wavamizi leo, wakati zenyewe ndizo zilitoa "vibali vya ujenzi" kwenye maeneo hayo?

Mkuu, Halmashauri zinatoa building permits kwa maeneo yaliyopimwa tu, ila tatizo property tax inachajiwa hadi kwenye squaters kwa hiyo malalamiko bado yako pale pale.

Kwa ujumla hata mimi sioni jambo hili likotekelezeka kwa sababu mwenye makosa ni wizara ya ardhi
 
Propaganda Tupu Tu Hizo!! Walikuwa Wapi Miaka YOTE Hiyo!! Wkt BUGURUNI MNYAMANI Likiwa Ni Shamba Tu!!! Je, Walikuwa Wapi MANZESE, MBURAHATI, KIGOGO, MABIBO, KIBANGU, MBAGALA, KONGOWE, CHAMAZI, MBANDE, TEGETA, BUNJU, KIMARA, MBEZI, KIBAMBA, KILUVYA N.k. WATANZANIA Wakijenga!!!?? Hebu Niambie Unaanza Vp Kuiplan Mbagala Au G /mboto Ya Leo!!!!!?? NDIO Maana NASEMA Ni Propaganda Tupu Tu Hizo!!! HAIWEZEKANI!!! Labda Hao Wa Mabondeni Na Maeneo Ya Wazi Au Wale Waliouziwa Maeneo Ya WATU Wengine!!! Hata Mabondeni BADO WATENDAJI Wa SERIKALI Ndio Wawe Wa KWANZA Kula Kibano!! Maana Watu WANAJENGA WAO Wanawatazama Tu, Hata Kuweka Mabango Ya Makatazo Walau Ya Kuzuga Kama Ya Tanroads Kule Mandela Road!! Eti "USIPAKI KTK ENEO HILI LA HIFADHI YA BARABARA "Lkn Malori Yamejaa KIBAO, TENA Hadi Mbele Ya Ofisi Zao Wenyewe!! Tehe! Tehe! Tehe!! Hiyo Ndio Bongo Bhana!!! NDIO Maana Bonde La Msimbazi Miaka 80- 90 LILIKUWA Tupu KABISA!! Lkn CCM Wakavamia Na Kujenga MAJENGO Ya MRADI WAO Waliouita SUKITA!! Muda Mfupi Tu Mwanzoni Mwa Miaka Ya 90, RAIA WAKAANZA Kujenga Kidogo Kidogo, Baada Ya KUONA Kumbe Sio MAENEO HATARISHI TENA, Baada Ya KUJENGA Na Kuanzishwa Kwa MRADI KUFUGA Wanyama Aina Mbali Mbali!!! HATIMAYE Bonde Lote La Msimbazi Likajengwa Kuanzia Pale Pale Jirani Na SUKITA, Magereji, Magodauni, Mayadi, Maofisi, Viwanda Na Makazi!! Leo Tabata Matumbi Na Buguruni Zimeungana, Kigogo Na Buguruni Na Sharifu Shamba, Na Magomeni Na Mburahati!! Hatimaye Mabonde Yooote YALIOPO Dar Yamejaa Ama MAKAZI, VIWANDA, MAGODAUNI, MAYADI, MAGEREJI N.k!!!! SWALI Je "HAO " Wanaojiita MIPANGO MIJI, WIZARA YA ARDHI, MANISPAA NA JIJI Walikuwa LIKIZO!!!!??? HATA Leo WAMEREJEA KAZINI!!!!???
 
Manzese yote mburahati yote ipigwe chini haiwexekani watu wamejenga mbele ya nyumba za wwnzao wamejenga vyoo nyumba zimebanana kama njiti za kiberiti
 
Kwanza nawapongeza JF kwa kuja na jukwaa zuri lililoboreshwa. Pili, kila mtu angetamani kuona maisha ya dar yanaboreka tunaondokana na makazi holela na foleni zisizo na mwisho. Ila serikali ijitathimini kwa hili ukiangalia asilimia kubwa ya mji haujapimwa na hata pale wakipima viwanja vinauzwa ghali balaa kiasi kwamba mtu wa kawaida kupata kiwanja kilichopimwa kwa dar ni ngumu. Mfano kiwanja kinauzwa kwa chini kabisa ni Tshs. 8,000/= kwa mita moja ya mraba.
Mimi naona tatizo ni pale serikali inapoingizwa mkenge na wafanyabiashara na yenyewe inaitikia na kuanza kufanya biashara ya kuuza viwanja kwa lengo la kupata faida.
Tatu, mji wa dar na nchi yote sidhani kama tunapanga miji yetu kwa kulenga miaka mingi ijayo kuanzia sasa ukizingatia ukuaji wa shughuli za kiuchumi na ongezeko la watu. Laiti kama tungekuwa na mipango ya miji kwa kipindi kirefu na tukaisimamia sidhani kama tungekuwa tunasumbuka na bomoabomoa leo hii. Sawa labda tuwasingizie waliojenga mabondeni na sehemu zisizoruhusiwa lakini wakati wanajenga serikali ilikuwepo inaangalia watu mpaka wanaanza kuishi pahala pale ndipo wanaonekana wamevamia. Dar hapahapa bado kuna mapori, naishauri serikali ijipange kupanua mji zaidi, shughuli za kiserikali zipelekwe na pembezoni mwa miji na waongeze kasi ya upimaji wa mji na pia bei ya viwanja wapunguze ili makusudi watu wengi zaidi hasa wa tabaka la chini wamiliki viwanja vilivyopimwa.
Na mwisho namalizia kwa kuuliza; hivi serikali inajua wanaobomolewa nyumba zao wanaenda kuishi wapi?
 
Kama hizi habari ni za kweli basi hata huyo Kingozi aliejilipua kutoa hizi taarifa anastahili kupimwa Ubongo wake. Haiingii akilini Dar kuvamiwa na kujengwa kwa kiwango hiki bila mamlaka husika kufahamu, kuona, kukubali hata kama ni kwa kutoa Vibali au kwa kupuuzia.

Kwa ufupi hili janga la kujitakia kwa kuanzia hapo Wizara ya Ardhi waanze kwa kumsweka ndani huyu alietoa taarifa pia wote waliofanya kazi baada ya City Master Plan ya Mwaka 1999 kuisha muda wake kwa makosa yafuatayo
1. Kulipwa Mishahara na Posho bila kufanya kazi (Wizi wa Pesa za umma)
2. Kushindwa/kukataa kwa makusudi kutimiza wajibu na majukumu yao (Kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu)
3. Kuhuhudhuria Semina, Warsha, Makongamano ya Mipango Miji bila kufanyia kazi Elimu husika (Professional negligence)
4. Kutoa Vibali hewa katika maeneo ambayo walikuwa wanafahamu hayajafayiwa Plan ( Matumizi mabaya ya madaraka ya Umma)
5. Kutoa taarifa za kuvunja nyumba za Wakazi wa Dar zaidi ya 3.6 Milioni kukosa makazi (Kutishia kuua kwa maneno)
6. Kutoa ushauri na taarifa za uongo kwa Viongozi na Umma wa Tanzania kwa kpindi chote tangu 1999 hadi leo hii ( Matumizi ya Takwimu za uongo)
 
Duuh..?! sasa, kama huu mji 80% haujapangwa walitaka wakazi wote wa Dar tubanane kariakoo na posta huko kulikopimwa?! Au walitaka watu wabaki vijijini hadi pale wao watakapopima?! maana hata nyumba za kupanga zilizopimwa dar nazo hazipatikani. Hivi walitaka wakazi wa Dar waishi mawinguni hadi watakapopima ndio watu washuke ardhini baada ya kupimwa?! Kwahili sioni ni namna gani itawezekana.
 
mber: 296267"]Tanzania hatuna wataalamu tunao wachumia tumbo tu ambao kila kitu kinachofavour upande wao hata kama ni kwa muda mfupi wao hukipitisha mara moja. Hebu angalia ambavyo tumepoteza old DAr city image kwa kubomoa majengo ya zamani na kujenga majengo mapya, marefu naarufu kama sky scrapers. Badala ya kuanzi sha miji mipya inayozunguka old city maarufu kama satelite cities, tumegangania kubadili image ya mji wetu na kuaribu kabisa miundo mbinu yake. Wanaojiita maprof, ma dr hamna kitu kabisa. Nchi za wenzetu old city ni chanzo cha mapato ya serikali yakitumika kama sehemu ya utalii, sisi tunafuta kabisa.[/QUOTE]
Old city ni muhimu kwa historia nawapongeza jiji la Tanga kwa kuhifadhi majengo na mazingira ya mji wa kale
 
Sio shida kwenda na brand new Master plan.Hiyo ilikuwa ni ndoto yangu kwa miaka mingi sana huko nyuma tangu nilipokuwa mtoto.Nilipotembea nchi za watu na nilipokuwa narudi Home bongo, nilikuwa nashindwa kuelewa n ikwa nini inashindikana kuiweka miji yetu katika mpango mzuri.Sio siri miji yetu inatia aibu kwa kukosa miundombinu muhimu kama ya barabara nzuri na bora hadi kwenye mitaa,mifumo ya maji safi na maji taka hasa ukizingatia karne hii vyoo vya shimo vimepitwa na wakati na pia vinaharibu mazingira,mpangilio mzuri wa majengo na anwani za makazi bado ni tatizo pia.Kwa ujumla, tujiandae kisaikolojia kwa mpango huu mzuri ambao serilkali inakuja nao ,ila ije pia na mpango mzuri wa kutufidia kwa makosa yao waliyo yafanya utafikiri hakukuwa na wizara ya ardhi tangu alipong'atuka Mwalimu.Walikaa kimya hata kutoa elimu ya mipango ya ardhi kwa njia ya vyombo vya habari ilikuwa shida,na wananchi wakajizoelea kwamba utaratibu ndio huo,mashamba yakageuzwa viwanja na matokeo yake ndo haya tunayotarajia muda mfupi ujao.Ushauri wangu kwa Serikali ni huu,waje na plani itakayo kidhi mahitaji ya miaka 100 hadi 150 ijayo ingawa sina uhakika kama dunia itaendelea kuwepo.
Msiwe na presha,kwani Utumbuaji wa majipu siku zote huja na maumivu.
 
Haya ni maneno nikitu kisichowezekana habadani labda huwe ni mpango wa miaka 10
 
Hiyo ni simply impractical na haiwezekani, angalia Tabata almost wanasema itakuwa ya wafanyakazi tena taasisi chache na lundo la wafanyakazi wengine waishi wapi??

Pili plan hii inanikumbusha walioenda kuplan Kigamboni master plan ilikuwa nzuri kweli ila tuna hela za kulipa fidia Dar nzima ili tuipange upya au tunataka kuanzisha mgogoro mwingine kama wa Kigamboni??

Plan ni nzuri ila haitekelezeki labda ingekuwa inatekelezwa in peace meal


Serikali iliyochoka ndiyo ilivyo! Plan za mifukoni na makabatini inawezaje kusaidia Mji?
Ebu angalia hayo ya Kigamboni. 2008-2015 miaka Sita na ushe unawagandisha watu na maisha yao! Walielezwa toka awali anachaneni na udalali wa ardhi na badala yake Serikali ihangaike na Miundo Mbinu kama Barabara,Maji safi na Taka na Umeme hata kama nikopa pesa.
Mwisho wa Siku Mji utakua wenyewe kama Kariako ilivyo sasa . Lakini Mdudu aliyepo ni kuwa Ndani ya Serikali na Wizara kuna majipu ya miaka nenda rudi na sasa yameshakuwa Donda Ndugu.

Nini maana na mankiti ya Soko huru?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom