NEW CABINET 2020: Ninaomba iwe desturi kwa Waziri wa Utalii kuakisi shughuli za ofisi yake kwa mavazi anapokuwa anakula kiapo cha utii kwa Jamhuri

Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania;

Ninaomba sasa iwe desturi kwa Waziri wa Maliasili na Utalii kuakisi shughuli za ofisi yake kwa mavazi ya asili anapokuwa anakula kiapo cha utii kwa Jamuhuri.

Waziri wa zamani wa utalii (Dr. Khamis Kigwangalla) akila kiapo akiwa hajavaa nguo za utamaduni wa mtanzania zaidi ya suti za mabeberu.

View attachment 1636325

Katika uvaaji wa mavazi ya asili, tunachovaa ni zaidi ya vitambaa tu vilivyoshonwa pamoja ili kutulinda miili yetu, bali nguo za asili ni ishara ya utambulisho wetu na pamoja tamaduni.

Kwa hivyo haishangazi kwamba kwa karne nyingi, jamii zimetumia mavazi kama njia ya kuwasilisha hadhi, tamaduni/mila na kusherehekea hafla muhimu na kuonyesha umoja ukiachilia mbali mambo mengi zaidi.

Mavazi ya asili huonyesha hisia ya ufahari katika jamii ya mtu na nchi na vile vile kuonyesha heshima kwa taifa lako. Haijalishi unatoka dini, ukanda ama kabila gani, kuvaa nguo za kitamaduni sio jambo baya ikiwa una sababu nzuri na maalum za kufanya hivyo.

Kuvaa nguo za kitamaduni sio jambo mbaya hata kidogo. Ninadhani inaweza kuwa ni jambo la kushangaza kwa mtu kuvaa nguo za kitamaduni wakati wote, angalau mtu aishi katika muonekano wa nyakati za kisasa kwa kuvaa suti na tai kwa kipindi fulani cha muda.

Waziri wa zamani wa utalii (Lazaro Nyalandu) akila kiapo akiwa hajavaa nguo za utamaduni wa mtanzania zaidi ya suti za mabeberu.
View attachment 1636333

Hata hivyo, watu wanapaswa kujaribu kuzivaa nguo za asili angalau mara moja moja. Ikiwa mtu ataamua kuvaa nguo za kitamaduni kutoka kwa utamaduni ambao hautokani na asili yake au yeye binafsi hautambui (Mjaluo kuvaa mavazi ya Kimaasai) basi ninapendekeza aombe maoni kutoka kwa mtu au watu ambao wanajua vizuri kuhusiana na vazi la kabila/tamaduni hiyo husika.

Nguo za jadi zinaonyesha utamaduni wa taifa. Nguo nyingi za kitamaduni zina vielelezo na vitu ambavyo vinavutia kutoka kwa wabunifu wengi hapa nchini Tanzania.

Kwa hivyo, mimi binafsi ninaamini, kuvaa mavazi ya kitamaduni katika hafla maalum (kama vile uapisho wa Waziri wa Utalii) ni njia nzuri sana ya mtu kujisikia yupo nyumbani.

NCHINI SWAZILAND - 12 MAY 2019: Newly sworn in Mayiwane MP, Eric Sifiso Matsebula was not to be left out as he quickly participated in Parliament business 20 minutes after taking his oath. Matsebula replaces David Shongwe who died last year.

View attachment 1636326

Before taking his oath, Matsebula who was in traditional wear was escorted into the House of Assembly by Mbabane West MP Johanne Shongwe and Ludzeludze MP Nonhlanhla Dlamini.

SOMA PIA>>> Kwanini mitaa ambamo kuna Balozi za nchi tano zenye nguvu duniani isiitwe majina ya vivutio vya utalii vya Tanzania?

NDUGU YANGU USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Imekaa njema hii
 
Back
Top Bottom