NEW CABINET 2020: Ninaomba iwe desturi kwa Waziri wa Utalii kuakisi shughuli za ofisi yake kwa mavazi anapokuwa anakula kiapo cha utii kwa Jamhuri

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
11,637
2,000
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania;

Ninaomba sasa iwe desturi kwa Waziri wa Maliasili na Utalii kuakisi shughuli za ofisi yake kwa mavazi ya asili anapokuwa anakula kiapo cha utii kwa Jamuhuri.

Waziri wa zamani wa utalii (Dr. Khamis Kigwangalla) akila kiapo akiwa hajavaa nguo za utamaduni wa mtanzania zaidi ya suti za mabeberu.

unnamed.jpg


Katika uvaaji wa mavazi ya asili, tunachovaa ni zaidi ya vitambaa tu vilivyoshonwa pamoja ili kutulinda miili yetu, bali nguo za asili ni ishara ya utambulisho wetu na pamoja tamaduni.

Kwa hivyo haishangazi kwamba kwa karne nyingi, jamii zimetumia mavazi kama njia ya kuwasilisha hadhi, tamaduni/mila na kusherehekea hafla muhimu na kuonyesha umoja ukiachilia mbali mambo mengi zaidi.

Mavazi ya asili huonyesha hisia ya ufahari katika jamii ya mtu na nchi na vile vile kuonyesha heshima kwa taifa lako. Haijalishi unatoka dini, ukanda ama kabila gani, kuvaa nguo za kitamaduni sio jambo baya ikiwa una sababu nzuri na maalum za kufanya hivyo.

Kuvaa nguo za kitamaduni sio jambo mbaya hata kidogo. Ninadhani inaweza kuwa ni jambo la kushangaza kwa mtu kuvaa nguo za kitamaduni wakati wote, angalau mtu aishi katika muonekano wa nyakati za kisasa kwa kuvaa suti na tai kwa kipindi fulani cha muda.

Waziri wa zamani wa utalii (Lazaro Nyalandu) akila kiapo akiwa hajavaa nguo za utamaduni wa mtanzania zaidi ya suti za mabeberu.
w4.jpg


Hata hivyo, watu wanapaswa kujaribu kuzivaa nguo za asili angalau mara moja moja. Ikiwa mtu ataamua kuvaa nguo za kitamaduni kutoka kwa utamaduni ambao hautokani na asili yake au yeye binafsi hautambui (Mjaluo kuvaa mavazi ya Kimaasai) basi ninapendekeza aombe maoni kutoka kwa mtu au watu ambao wanajua vizuri kuhusiana na vazi la kabila/tamaduni hiyo husika.

Nguo za jadi zinaonyesha utamaduni wa taifa. Nguo nyingi za kitamaduni zina vielelezo na vitu ambavyo vinavutia kutoka kwa wabunifu wengi hapa nchini Tanzania.

Kwa hivyo, mimi binafsi ninaamini, kuvaa mavazi ya kitamaduni katika hafla maalum (kama vile uapisho wa Waziri wa Utalii) ni njia nzuri sana ya mtu kujisikia yupo nyumbani.

NCHINI SWAZILAND - 12 MAY 2019: Newly sworn in Mayiwane MP, Eric Sifiso Matsebula was not to be left out as he quickly participated in Parliament business 20 minutes after taking his oath. Matsebula replaces David Shongwe who died last year.

mkhu-new-mp2.jpg


Before taking his oath, Matsebula who was in traditional wear was escorted into the House of Assembly by Mbabane West MP Johanne Shongwe and Ludzeludze MP Nonhlanhla Dlamini.

SOMA PIA>>> Kwanini mitaa ambamo kuna Balozi za nchi tano zenye nguvu duniani isiitwe majina ya vivutio vya utalii vya Tanzania?

NDUGU YANGU USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 

Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
6,476
2,000
1. Waziri Mkuu. Kassim Majaliwa
2. Fedha.... Mpango Philip
3. Nje...... Palamagamba Kabudi
4. Ulinzi..... Makame Mbarawa
5. Kilimo......Hussein Bashe
6. Mifugo.... Luhaga Mpina
7. Viwanda/Biashara.... Charles Kimei
8. Maji.... Kitila Mkumbo
9. Uwekezaji.... ?????????
10. Madini.... Dotto Biteko
11. Umeme .... Merdard Kalemani
12. Afya....Ummy Mwalimu
13. Elimu.... Joyce Ndalichako
14. Tamisemi .....Suleiman Jafo
15. Ujenzi.....?????????
16. Mambo ya ndani.......??????
17. Mazingira.......??????
18. Utalii..........????????
19. Michezo.......??????
20. ????
 

1gb

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
1,792
2,000
Sio huyo tu,waziri wa ulinzi nae avae Gwanda,Amiri Jeshi mkuu nae Avae Gwanda.
Rais wa wanyonge nae avae ma lapulapu ku tanabaisha nchi maskini Tanzania.
Waziri wa Madini nae atinge kila aina madini na vito vya thamani.
Haki sawa kwa wote,
Sio maliasiri avae ngozi afu wa mazingira avae thuti.
 

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
11,637
2,000
Waziri wa Madini nae atinge kila aina madini na vito vya thamani.
Haki sawa kwa wote,
Sio maliasiri avae ngozi afu wa mazingira avae thuti.
Ninadhani Waziri wa Utalii anapaswa kupewa kipaumbele zaidi katika suala la mavazi kuliko hao wengine mkuu
 

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
11,637
2,000
1. Waziri Mkuu. Kassim Majaliwa
2. Fedha.... Mpango Philip
3. Nje...... Palamagamba Kabudi
4. Ulinzi..... Makame Mbarawa
5. Kilimo......Hussein Bashe
6. Mifugo.... Luhaga Mpina
7. Viwanda/Biashara.... Charles Kimei
8. Maji.... Kitila Mkumbo
9. Uwekezaji.... ?????????
10. Madini.... Dotto Biteko
Time will tell mkuu...
 

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
11,637
2,000
1. Waziri Mkuu. Kassim Majaliwa
2. Fedha.... Mpango Philip
3. Nje...... Palamagamba Kabudi
4. Ulinzi..... Makame Mbarawa
5. Kilimo......Hussein Bashe
6. Mifugo.... Luhaga Mpina
7. Viwanda/Biashara.... Charles Kimei
8. Maji.... Kitila Mkumbo
9. Uwekezaji.... ?????????
10. Madini.... Dotto Biteko
11. Umeme .... Merdard Kalemani
12. Afya....Ummy Mwalimu
13. Elimu.... Joyce Ndalichako
14. Tamisemi .....Suleiman Jafo
15. Ujenzi.....?????????
16. Mambo ya ndani.......??????
17. Mazingira.......??????
18. Utalii..........????????
19. Michezo.......??????
20. ????
Mzee baba hii team umeipata wapi mkuu? Au na wewe upo kitengo?
 

Mwalimu Ntuntu

JF-Expert Member
Jun 3, 2016
279
250
Mzee baba hii team umeipata wapi mkuu? Au na wewe upo kitengo?
1. Waziri Mkuu. Kassim Majaliwa
2. Fedha.... Mpango Philip
3. Nje...... Palamagamba Kabudi
4. Ulinzi..... Makame Mbarawa
5. Kilimo......Hussein Bashe
6. Mifugo.... Luhaga Mpina
7. Viwanda/Biashara.... Charles Kimei
8. Maji.... Kitila Mkumbo
9. Uwekezaji.... ?????????
10. Madini.... Dotto Biteko
11. Umeme .... Merdard Kalemani
12. Afya....Ummy Mwalimu
13. Elimu.... Joyce Ndalichako
14. Tamisemi .....Suleiman Jafo
15. Ujenzi.....?????????
16. Mambo ya ndani.......??????
17. Mazingira.......??????
18. Utalii..........????????
19. Michezo.......??????
20. ????
20. Paul Makonda (Waziri asiye na Wizara Maalum)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom