New Age: Dini mpya ya ulimwengu

Tunaamini vipi ulichokiandika wewe.? Nini Tofauti ya wanao sema mambo hayo ni mazuri na wewe unaesema ni mabaya.? Unawezaje kututhibitishia kwamba wewe upo sahihi na ulichokiandika.? Una Evidence yoyote au confessions zozote zilizo wazi toka kwa victims waliofanya mambo hayo na wakapatwa mabaya.?? Please let us know..
 
Kwa kifupi, New Age ni nini? Ni mkusanyiko wa dini zote; matendo mbalimbali ya kidini, ambayolengo lake ni kumfanya mwanadamu awe mungu. Ni mwavuli ambao chini yake dini zote zinaweza kujificha, ingawaje mafundisho yanaweza kuwa kinyume kabisa dini tulizozizoea kwa mana uislam& ukristo.

Yako mafundisho na dini ambazo asili yake ni ubudha, imani za siri za kishetani, na hata baadhi ya dini ambazo zina mafundisho ya msingi ya Kikristo, kwa mfano kanisa la Moon na Mashahidi wa Yehova hawa walipigwa marufuku Urusi, Wana wa Mungu au kile kinachoitwa ‘Sayansi ya Kikristo’ Church of Scientology pamoja na madhehebu ya kiislamu yanayoamini kwenye meditation.

Ziko falsafa: Ukonfyushasi wa Kichina (Chinese Confucianism), imani za siri (occult) na mafundisho ya unajimu, mashamani, ma-guru, Krishna, n.k. Makundi haya na mengineyo yanatengeneza namna ya kundi moja ambalo kiini chake hasa ni ushetani. Nguvu zingine zote za kichawi na imani za siri zinatokea hapa.

Pamoja na hayo, ni watu wachache sana waliomo ndani ya New Age wanaofahamu juu ya ukweli huu. Ndiyo sababu kuna Watu wengi walio kwenye kundi hili bila wao kujijua wanapotea.

Kwa kuwa, kwa nje kundi hili linaonekana ni la kiutu na ni chanya, hiki ni kishawishi kwa Watu na malengo yake yaliundwa kwa ajili hasa ya Watu wasio wanachama, ili kwamba wazimwe nguvu zao; na waweze kupelekwa mbali na Mungu . Baadhi ya mambo yanayofanyika ni yoga, kutoka katika mwili (astral projection), kuelea (levitating), namna zote za uchawi na upigani bao. Mambo haya ni vishawishi.
Mambo yote ya Meditation ni Ushetani wa kusalimu amri pamoja na akili ili kuruhusu kitu usicho kijua kichukue ufahamu wako.

Wanaanza kwa kufundisha kwamba Wakristo au waislamu wanatakiwa kuwa wavumilivu kwa makundi mengine, kwa mfano, kwa ajili ya maslahi ya wanadamu na amani ya dunia. Maneno yanayohusiana na upendo yanaweza kuwadanganya kirahisi Watu wengi.

Wako watu wengi wanaojifanya ni watumishi wa Mungu na wanaokuja kuhubiri na kutoa mawaiza kumbe ni wasanii tuu kajamaba8 washauza nafsi. Lakini pia wako watu kutoka kundi la New Age, wanaojiita guru, ambao nao wanakuja. Na kama mtasikiliza mafundisho yao na kutenda yale watakayowafundisha basi mungu atageuzia uso wake mbali na ww na jina lako litafutwa kwenye kitabu. .

Nisisitize tena kwamba, matendo na mafundisho haya ya kundi la New Age yanaweza kuharibu maisha yenu, lakini baya zaidi ni kuwa, yanaweza kuharibu roho yako pamoja na familia yako.

Binafsi nimeshashuhudia Wakristo na waislamu waliorudi nyuma na kumwacha Mungu aliye hai.kwa mfano wapo watu hapa jf wenye falsafa za ki new age ambao wana hadaa watu na meditation au astral prjection nakushauri usiingie humo madhara yake ni makubwa utaalika mapepo wachafu ndani ya nafsi yako au roho yako na kuharibu maisha yako kwa ujumla. Ndugu zangu msipende miujiza najua mnadanganywa kwenye meditation kuna miujiza hamna kitu ni majini tuu na mapepo yanachezea ufahamu wenu.

Ziko njia nyingi na matendo mengi ambayo Watu huingizwa humo. Kwa mfano, yoga, na hasa hatha-yoga, ambayo inajumuisha mazoezi ya viungo na kupumua. Wako binadamu wengi wa Marekani na nchi za magharibi ambao wanajihusisha na jambo hili.

Yoga ni nini? Ni mfumo wa vitendo vya kidini kwa ajili ya mtu kurudi tena baada ya kufa (reincarnation). Neno linasema kwamba Na kama vile watu walivyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu (Ebr. 9:27). Hakuna mtu anayeweza kurudi tena duniani kwa njia nyingine baada ya kufa hawezi kurudi kama mti au myama au mdudu. Yoga asili yake ni Uhindu, na ni mfumo wa vitendo vya dini nyingi. Vitendo hivi vinaaminika kuwa vinavunja nira kwenye maisha yako, ambazo, kwa imani zao, zitaanzisha mchakato wa “kuzaliwa tena baada ya kufa”. Kwa hiyo, kupitia yoga, tunafungulia mlango kwa mapepo ya Kihindu.

Wanaotetea falsafa ya Reicarnation ni wale wanaohusisha De Ja Vu na Maisha ya Zamani

Watu walegevu au wapuuzi wanasema kuwa hawaamini juu ya mambo haya bali kwamba hatha-yoga ni mazoezi tu mazuri kwa ajili ya mwili. Kwa kusema hivyo, tayari wameshaamini uongo wa ibilisi.

Iweje Shetani atakuruhusu ujenge mwili wako, na kujisikia vizuri? Inamana anakuoenda Sana? maana anajua kuwa Watu kama hao hawawezi kuona kilicho nyuma katika ulimwengu wa roho. Ni nini basi kitatokea? Matokeo yote ya kimwili na kiroho yanajengwa juu ya nguvu iitwayo Shiva. Hili ni pepo la Kihindu, ambalo wanalifungulia mlango.

Katika upande wa chini wa uti wa mgongo wetu, kuna nafasi wanayoiita “nguvu ya nyoka” au Kundalini kwa wanaofanya Mambo haya wanajua Unapofanya mazoezi ya yoga, unakuwa kimsingi unasujudu kwa huyu Shiva; ile nguvu ya nyoka inaamshwa kwenye mwili wako. Inapokuwa kubwa, watu wanapata na uwezo fulani usiokuwa wa kibinadamu.

Mambo haya hayatoki kwa Mungu aliye hai. Asili yake ni kwenye ulimwengu wa giza wa kipepo. Kwa hiyo, kumbuka kuwa mambo yote tunayofanya kimwili wakati wa yoga yana asili ya ulimwengu wa giza wa kipepo; haijalishi tunafikia ngazi gani. Hata hatua za kwanza kabisa zinakuwa zinaelekea kwenye vifungo hivyo – tuwe tunakubaliana au hatukubaliani.

Namna ya pili ambayo ni kishawishi kwa Watu, hata walio makanisani au Miskitini na imeenea sana nchi za magharibi pamoja na hapa jamii forum kuna mafundisho yake ni “kutoka nje ya mwili” (astral projection). Hii ni aina ya mazoezi ambayo yanaweze kufanya roho ya mtu ikatengana na mwili. Kwa uamuzi wako mwenyewe, unaweza kupeleka roho yako kwenye mahali au wakati wowote, kwa mfano ukarudi nyuma ya wakati kwenye maisha yaliyopita (time travel) ukaenda kwenye anga au kokote kwingineko.

Mara nyingi hili linawezekana, lakini ambacho watu wa namna hii hawatambui ni kuwa, roho zao zinakuwa haziingii kwenye ufalme wa Mungu bali wa mapepo.

Kwa njia hii, unafungulia mlango kwa viumbe wengine wa kiroho wasioonekana. Shetani ameweka tayari mtego wake kwa ajili yako pale. Watu wanapoanza kufanya mambo haya, kwa mara ya kwanza wanakuwa na hisia nzuri za kunyanyuliwa. Hisia hizi zinatoka kwenye asili ya dhambi.

Kuna hatari kubwa hapa. Kwa kitambo kidogo unakuwa unaweza kuitawala hali hiyo, lakini baada ya kufikia mahali fulani, unaanza kupoteza udhibiti wa mwili wako na unakuwa ni uwanja wa mapepo kufanya kila watakacho. Wengi walipoteza hata uwezo wao wa kurudi.

Res ipsa loquitur,
Badison.

View attachment 1015716

Sent using Jamii Forums mobile app

Mungu aliye hai yupi? Yeye alitokea wapi, kwani kuna wengine waliokufa?

Ni dini gani inakupeleka kwa huyu Mungu aliye hai wakati yeye mwenyewe hakuna dini aliyoshusha kutoka ili tuiabudu.

Ni hukumu gani atatupa sisi tuliokengeuka na kukataa kanisa na misikiti. Wanasema tutachomwa moto milele, kuna moto gani unaweza kuchoma roho?

Unasema hii dini mpya asili yake ni shetani inatupeleka mbali na Mungu, kwani hujui kuwa siku nyingi tuko mbali na mungu shetani ndiye mtawala wa hii dunia? Jehova na kina Alah washaiacha siku nyingi hii dunia wako huko kwenye solar system ingine na shughuli zao.

Kwanini huyu Mungu aliyetuumba atupe akili ndogo kiasi kwamba tushindwe kujua chanzo chake yeye au mwanzo wake maana kwa akili alizotupa tunajua hakuna kiti kisicho na mwanzo wala mwisho, je mwisho wake yeye ukifika sisi viumbe alivyotuumba tutakuwaje ?
 
Tunaamini vipi ulichokiandika wewe.? Nini Tofauti ya wanao sema mambo hayo ni mazuri na wewe unaesema ni mabaya.? Unawezaje kututhibitishia kwamba wewe upo sahihi na ulichokiandika.? Una Evidence yoyote au confessions zozote zilizo wazi toka kwa victims waliofanya mambo hayo na wakapatwa mabaya.?? Please let us know..
Upo sahihi Kabisa. Naweza nikakuthibitishia. But kuwa na Subira Kidogo but endelea pitia pitia imani za waamini masanamu kama Buthist au Wahindi utaelewa nilicho kiandika. Nasubiri maoni ya New agers ili ni update uzi with proof.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu aliye hai yupi? Yeye alitokea wapi, kwani kuna wengine waliokufa?

Ni dini gani inakupeleka kwa huyu Mungu aliye hai wakati yeye mwenyewe hakuna dini aliyoshusha kutoka ili tuiabudu.

Ni hukumu gani atatupa sisi tuliokengeuka na kukataa kanisa na misikiti. Wanasema tutachomwa moto milele, kuna moto gani unaweza kuchoma roho?

Unasema hii dini mpya asili yake ni shetani inatupeleka mbali na Mungu, kwani hujui kuwa siku nyingi tuko mbali na mungu shetani ndiye mtawala wa hii dunia? Jehova na kina Alah washaiacha siku nyingi hii dunia wako huko kwenye solar system ingine na shughuli zao.

Kwanini huyu Mungu aliyetuumba atupe akili ndogo kiasi kwamba tushindwe kujua chanzo chake yeye au mwanzo wake maana kwa akili alizotupa tunajua hakuna kiti kisicho na mwanzo wala mwisho, je mwisho wake yeye ukifika sisi viumbe alivyotuumba tutakuwaje ?
Hoja yako ni ya Msingi Sana kiasi kwamba Imenibidi nirudie kuisoma mara kadhaa. Misingi ya kuwa binadamu ni ufahamu. New age Movement ni kiini macho cha kuhadaa walimwengu. Kuna kizuizi kilichowekwa na Muumbaji kinachotufanya sisi wanadamu tusiweze kuwaona majini/mashetani lakini wao wanatuona. Sisi wanadamu kwa mujibu wa kanuni za ulimwengu hatupaswi kushirikiana na viumbe hivo. Ili tuweze kushirikiana nao lazima tuwape nafasi kwa hiari yetu watuvae ufahamu wetu kwa njia ufahamu. Dhana ya binadamu siku zote ni kuvuka mipaka na kuasi, matokeo ya kuasi sheria hizo ndo kufungua njia au ku chanel viumbe hao. Kuhusiana na Mungu aliye hai sio kama unavyofikiri bali ni cosmic laws ambazo sisi kama binadamu tuliokuwa hai tumewekewa tuzifuate. Tukizishika sheria hizo hakuna kitu kitakachoweza kutudhuru. Sasa hizo sheria baadhi wanaziita mungu, wengine wanaita energy. Kama binadamu ukiishi kwa kufuata sheria hizo utakuwa na AMANI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binaadam ni mwoga wa kujijua na kitendo cha kutaka kuvunja minyororo ya mapokeo na ku kuikumbatia hatima yake ni vitu vinavyo mshtua sana, na hasa kutokujua uwezo tulionao ndo tumefikia kuziweka nguvu zetu kwa watu na vitabu

Na labda hao watu ‘mitume’ wanashangaa tulivyo ziacha nguvu tulizonazo

Hii misemo ‘tuumbe mtu kwa mfano wetu ‘ ama kwa mweye imani anaweza kuuamrisha mlima na ukahama ‘ ni misemo ya kutuonyesha nguvu tulizo nazo ‘but we scared to face our own nature ‘

Hii ni ‘Enlighten age’ mkuu wanaoweza kujua na kufunuliwa wanatawala mazingira haya na wanakamilisha msemo ‘ binaadam ni mtawala wa ulimwengu ‘ na any fate ipo mikononi kwetu

Sorry kwa uandishi wangu

Be blessed
 
Mkuu fafanua kidogo bssi tunawezaje kutawala haya mazingira
 
Hoja yako ni ya Msingi Sana kiasi kwamba Imenibidi nirudie kuisoma mara kadhaa. Misingi ya kuwa binadamu ni ufahamu. New age Movement ni kiini macho cha kuhadaa walimwengu. Kuna kizuizi kilichowekwa na Muumbaji kinachotufanya sisi wanadamu tusiweze kuwaona majini/mashetani lakini wao wanatuona. Sisi wanadamu kwa mujibu wa kanuni za ulimwengu hatupaswi kushirikiana na viumbe hivo. Ili tuweze kushirikiana nao lazima tuwape nafasi kwa hiari yetu watuvae ufahamu wetu kwa njia ufahamu. Dhana ya binadamu siku zote ni kuvuka mipaka na kuasi, matokeo ya kuasi sheria hizo ndo kufungua njia au ku chanel viumbe hao. Kuhusiana na Mungu aliye hai sio kama unavyofikiri bali ni cosmic laws ambazo sisi kama binadamu tuliokuwa hai tumewekewa tuzifuate. Tukizishika sheria hizo hakuna kitu kitakachoweza kutudhuru. Sasa hizo sheria baadhi wanaziita mungu, wengine wanaita energy. Kama binadamu ukiishi kwa kufuata sheria hizo utakuwa na AMANI.

Sent using Jamii Forums mobile app
Big up chief,umajibu hoja kwa nondo kali.
Great thinker

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii umeongea hapo yote ni upuuzi mtupu, wewe una hakika gani ni ushetani, kwanza nikuulizie nani amewahi kutana na shetani hapa duniani na hasa miaka ya karibuni achana na story vitabu vya kale,
Na mbona huwa mnatetea Mungu sana, c muache Mungu afanye makuu anayoyaweza
Kwani hio mambo zote zinatokea duniani yeye haoni!??? Watu wenye dini mingi sana huwa mna matatizo ya akili kabisa
Mmejaa na maono ya ajabu kabisa, hivi mnadhani ukristo na Uislamu ndio dini pekee hapa duniani na huwa mnajiona mko sahihi sana,
Kwa taarifa yako kuna dini zaidi ya 200 na zote wanajiona wako sahihi

Ni kweli huu ni upuuzi. Lakini nitaandaa topic ingine maalum ya lucid dreams au ndoto ili watu wajifunze ukweli na uongo ujitenge kwa mana topic ya meditation ushaelewa na imekugusa. Thats very nice.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni woga tu.

Adui mkubwa ktk dini ni Shetani,kusema ukweli ni rahisi muungano wa nchi na nchi kutokea lakini sio muungano wa dini na dini

Aidha ni rahisi maridhiano ya kisiasa kufanyika lakini maridhiano ya kidini ni jambo ambalo sio rahisi kutokea

Sio rahisi kwa sababu kwa kufanya hivyo,watakuwa wametenda dhambi na na kufanya maridhiano na Shetani

Kila dini inaona wenzao kama ndio wafuasi wa Shetani,

Ukweli ni kwamba hakuna kiumbe anayeitwa Shetani au Ibilisi bali kuna nature ya binadamu. Binadamu anaweza kuwa Shetani au Mungu. Hizo zote mbili ni sifa za binadamu. Lower self and higher self.

Hakuna mahali panaitwa motoni au mbinguni,hizo ni hali za akili ya binadamu. Binadamu anaweza kuishi motoni kwa hali yake ya akili au kuishi peponi kwa hali yake ya akili,yaani moto au pepo unaziumba wewe mwenyewe akilini,ukiishi maisha ya kujiumiza uko motoni na ukiishi maisha ya furaha yanayopatana na kanuni 16 za maumbile basi uko peponi.

Mazoezi kama Astral projection, Levitation ni nguvu za ziada

Roho ya mwanadamu ambayo inaishi ndani ya mwili wote inao uwezo wa kuacha mwili bila ya kufa,na hii hutokea pale ambapo roho inapokuwa imagain energy kubwa ya cosmic energy ( nguvu kuu),na hapo kwa mara ya kwanza binadamu huweza kujigundua kwamba yeye sio mwili huu,bali anaishi ktk mwili huu.

Levitation ni nguvu mojawapo ya nguvu za ziada,watu maarufu ktk Biblia kama Yesu,Philipo,Eliya,Paulo walielea angani au walitoka nje ya mwili.

The greatest trick the Devil ever pulled was convincing the world he didn't exist.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
The greatest trick the Devil ever pulled was convincing the world he didn't exist.

Sent using Jamii Forums mobile app
He doesn't exit, show me where is he living, coz I have been trying to meet him, it's neither pastors or mosque leaders wamewahi kujua anapokaa, ni propaganda tuu,
Nipeleke kwa shetani hata leo, natamani sana kuonana naye

My Favorite Poem of All Time. "IF I WERE THE DEVIL"

If I were the Prince of Darkness, I would want to engulf the whole earth in darkness.

I'd have a third of its real estate and four-fifths of its population, but I would not be happy until I had seized the ripest apple on the tree.

So I should set about however necessary, to take over the United States.

I would begin with a campaign of whispers.
With the wisdom of a serpent, I would whispers to you as I whispered to Eve, "Do as you please."

To the young I would whisper "The Bible is a myth." I would convince them that "man created God," instead of the other way around. I would confide that "what is bad is good and what is good is square."

In the ears of the young married I would whisper that work is debasing, that cocktail parties are good for you. I would caution them not to be "extreme" in religion, in patriotism, in moral conduct.

And the old I would teach to pray — to say after me — "Our father which art in Washington."
Then I'd get organized.

I'd educate authors in how to make lurid literature exciting so that anything else would appear dull and uninteresting.

I'd threaten TV with dirtier movies, and vice-versa.

I'd infiltrate unions and urge more loafing, less work. Idle hands usually work for me.

I'd peddle narcotics to whom I could, I'd sell alcohol to ladies and gentlemen of distinction, I'd tranquilize the rest with pills.

If I were the Devil, I would encourage schools to refine young intellects, but neglect to discipline emotions; let those run wild.

I'd designate an atheist to front for me before the highest courts and I'd get preachers to say, "She's right."

With flattery and promises of power I would get the courts to vote against God and in favor of pornography.

Thus I would evict God from the courthouse, then from the schoolhouse, then from the Houses of Congress.

Then in his own churches I'd substitute psychology for religion and deify science.
If I were Satan I'd make the symbol of Easter an egg And the symbol of Christmas a bottle.

If I were the Devil I'd take from those who have and give to those who wanted until I had killed the incentive of the ambitious. Then my police state would force everybody back to work.

Then I would separate families, putting children in uniform, women in coal mines and objectors in slave-labor camps.

And if i were the devil i will convice people i do not Exist.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona unaleta vingereza tuu hapa, weka kwa lugha pendwa ya Mheshimiwa tukuelewe
Au ndio unataka tujue unajuana na Mungu sana, maana hio ndio lugha wakoloni walitumia kubadilisha dini za mababu zetu, na kutupatia hizo dini zao zenye kutaja shetani na moto huko kwa Mr God, bila ya uthibitisho wa kuwa Mungu au shetani wako wapi,!?? Kwa miaka elfu kadhaa sasa.
By the way, c nimekuambia unipeleke huko kwa shetani, mbona unaleta vingereza vingi mzee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaanza kwa kufundisha kwamba Wakristo au waislamu wanatakiwa kuwa wavumilivu kwa makundi mengine, kwa mfano, kwa ajili ya maslahi ya wanadamu na amani ya dunia. Maneno yanayohusiana na upendo yanaweza kuwadanganya kirahisi Watu wengi.
Kwamba watu wakipigana kuuana na kuchukiana ndio inavyotakiwa ...sijakuelewa kabisa hapa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom