Neville Meena wa Jukwaa la Wahariri kurejea nchini leo kutoka Afrika Kusini alikokuwa kwa ajili ya matibabu

Unapenda mipasho eee?
Ndiyo maana umeingia kwenye thread.
Thread zingine ni muendelezo wa mipasho tu,watu wamesema "ugonjwa wa kawaida"
Ni suala la kutumia common sense tu,ugonjwa wa mtu ni suala private hawataki kulizungumzia full stop.!
 
Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena leo anarejea nchini kutoka Afrika Kusini alikokuwa anapata matibabu (check up).

Meena alikwenda Afrika Kusini Septemba 20, mwaka huu baada ya kuwa amelazwa Muhimbili kwa siku 12 kutokana na maumivu ya kichwa.

Madaktari wamempima na kumfahamisha kuwa alikuwa na tatizo la kawaida hivyo wamempatia dawa na kumruhusu arejee nyumbani Tanzania kuendelea na kazi.

Tunamshukuru Mungu kwa uponyaji huu na tunawashukuru nyote kwa sala zenu.

Deodatus Balile
Kaimu Mwenyekiti
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)

Nawasubiri wale ' Wazozaji / Wapayukaji ' waliosema kwamba amewekewa ' Sumu ' waje hapa waombe radhi na ikiwezekana ' Watubu ' kwa Mungu wao.
 
Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena leo anarejea nchini kutoka Afrika Kusini alikokuwa anapata matibabu (check up).

Meena alikwenda Afrika Kusini Septemba 20, mwaka huu baada ya kuwa amelazwa Muhimbili kwa siku 12 kutokana na maumivu ya kichwa.

Madaktari wamempima na kumfahamisha kuwa alikuwa na tatizo la kawaida hivyo wamempatia dawa na kumruhusu arejee nyumbani Tanzania kuendelea na kazi.

Tunamshukuru Mungu kwa uponyaji huu na tunawashukuru nyote kwa sala zenu.

Deodatus Balile
Kaimu Mwenyekiti
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)
Hili ni jukwa la siasa. Kuna uhusiano gani kati ya ugonjwa wa Meena na jukwaa hili?? Hapa tunasumbua vichwa kujadili mambo ya siasa za kitaifa na mataifa.

Mod. hamisha thrd hii iende inakotakiwa.
 
yale yale ya kujiteka,ya kukimbia nchi,ya kujifanya umewekewa sumu............................people bwana:D:D:D:D
 
Wapendwa mimi taarifa nilizonazo ndiyo hizo nimezitoa. Sasa kama kuna mtu ana taarifa za ziada na tuhuma hizo zinazotolewa kwa innuendo dhidi yangu ziwekeni wazi.

Lakini nawaambia tukiigeuza Tanzania kuwa nchi ya lawama, mashaka na tuhuma zisizokuwa na uhakika dhidi ya kila awaye, nchi hii mtu atapata shida watu watampita kwa kuogopa kutuhumiwa.

Muda, sala na rasilimali tulizotumia kuokoa maisha ya Meena tangu Tanga, Muhimbili na hatimaye Milpark South Africa kujiridhisha maisha yake yasiwe hatarini leo unasoma tuhuma za aina hii? Inaumiza.

Kwa hakika inanipasa kuazima maneno ya Bwama Wetu Yesu Kristu: " Baba uwasamehe kwani hawajui watendalo."
 
Mkuu Balile pole sana , unapokuwa kiongozi ni lazima uwe na ngozi ngumu kidogo , hatuna ugomvi na wewe hata kidogo , mashaka yetu ni hicho kitu kinachoitwa "tatizo la kawaida" , huku Muhimbili ikishindwa mpaka mtu kupandishwa ndege .
 
Asante kwa taarifa mkuu , ila hilo " TATIZO LA KAWAIDA " ni la kipekee maana Tanzania ilishindikana mpaka South Africa !
Ni kujikweza tu na kutafuna pesa ya wafadhili
Waandishi wengi wana matatizo mazito kuliko la huyo kamanda
Ni stress sugu tu zinamsumbua huyo
 
weee !!! unasema kweli mkuu ?
Siku hizi mpaka figo watu wanabandikwa Muhimbili ,huyo ana stress za kupambana na Magufuli na chuki aliojijazia kifuani bila ya sababu
Waambie wapeleke waandishi wanaosumbuliwa na maradhi makubwa nao kama wana hela ya mchezo
 
Back
Top Bottom