Neville Meena amehamia rasmi Gazeti la Tanzania Daima na kupewa nafasi ya Mhariri Mtendaji

hapa ni kama vile unalipigia debe gazeti la tanzania daima na unalipaka matope mwananchi. akina meena wameondoka hawakukimbia na wamefuata green pasture. sasa tanzania daima ihakikishe kuwa donge nono linadumu au sivyo na wao watakimbiwa pia.
Nimenote like u
 
TanzaniaDaima=Mbowe= Chadema= Chaga = Meena
Mawazo ya ukabila ya kijinga kabisa haya. Kwa jinsi hiyo utajikuta unaishia na fomula hiyohiyo mpaka kwenye dini, jinsia rangi nk. Ukimaliza hapo utahamia kwa wake zao. Hayo ni mawazo ya kwenda mbele hatua moja na kurudi nyuma hatua 3 Mtu mwenye kuchambua mambo kwa mtindo wako ni wa kuepukwa kama ukoma! Watu wanaangalia uwezo na utendaji wewe unaturudisha kwenye ukabila. Una sifa kama za Meena akaenda kuomba kazi kwa Mbowe ukaikosa kwakuwa wewe sio mchaga? Mtakalia hayo hayo ya ukabila wakati wenzenu wanasonga mbele!
 
Jambo moja ambalo wengi wenu mtakuwa hamjalijua ni kwamba Kuhamia Tanzania daima kwa Meena ni mwendelezo wa mkakati wa Team Lowassa kuhakikisha ana kila Mhariri katika Kila Media Outlet.

Meena, Kibanda, Balile na Manyerere Jackton ndio ambao walipaswa kuanzisha Gazeti la Jamhuri mwanzoni kabisa wakati Gazeti lilianza huku baadae Kibanda akitakiwa pia kuanzisha Gazeti jingine liitwalo TUENDAKO. Magazeti yote haya mawili yana mkono wa Lowassa katika kujiandaa kwa 2015. Tuendako halijaweza kusimama lakini Jamhuri lilianza chini ya Manyerere na Deo Balile baada ya Meena na Kibanda kuamua kubaki katika magazeti yao ya awali wakati huo yaani Mwananchi kwa Meena na Tanzania Daima kwa Kibanda.

Mkakati ulisonga mbele kwa Kibanda kupeewa Mtanzania ikiwa ni baada ya TUENDAKO kusuasua huku ikitafuta namna ya kuyashika magazeti megine yenye ushawishi. Hatimaye wamelipata Tanzania Daim na amekabidhiwa Meena huku jitihada zikindelea kuyakamata Nipashe, Raia Mwema, na Mengineyo

Kwa ufupi, LowassaTeam is at work na kumpenyeza Meena Tanzania Daima ni Ushindi kwao ingawa Mbowe hajagundua hilo. Mkakati unaendelea
 
Last edited by a moderator:
Lowasa anahusika VP na MTU kubadilisha kituo cha kazi kupata maslahi zaidi.kama dau la Tanzania daima ni nzuri kwanini usiende.mambo ya ukabila sio fresh.
 
Jambo moja ambalo wengi wenu mtakuwa hamjalijua ni kwamba Kuhamia Tanzania daima kwa Meena ni mwendelezo wa mkakati wa Team Lowassa kuhakikisha ana kila Mhariri katika Kila Media Outlet.

Meena, Kibanda, Balile na Manyerere Jackton ndio ambao walipaswa kuanzisha Gazeti la Jamhuri mwanzoni kabisa wakati Gazeti lilianza huku baadae Kibanda akitakiwa pia kuanzisha Gazeti jingine liitwalo TUENDAKO. Magazeti yote haya mawili yana mkono wa Lowassa katika kujiandaa kwa 2015. Tuendako halijaweza kusimama lakini Jamhuri lilianza chini ya Manyerere na Deo Balile baada ya Meena na Kibanda kuamua kubaki katika magazeti yao ya awali wakati huo yaani Mwananchi kwa Meena na Tanzania Daima kwa Kibanda.

Mkakati ulisonga mbele kwa Kibanda kupeewa Mtanzania ikiwa ni baada ya TUENDAKO kusuasua huku ikitafuta namna ya kuyashika magazeti megine yenye ushawishi. Hatimaye wamelipata Tanzania Daim na amekabidhiwa Meena huku jitihada zikindelea kuyakamata Nipashe, Raia Mwema, na Mengineyo

Kwa ufupi, LowassaTeam is at work na kumpenyeza Meena Tanzania Daima ni Ushindi kwao ingawa Mbowe hajagundua hilo. Mkakati unaendelea

Ramli nyingine ni balaa. Moja ulilopatia ni la sisi wanne kuanzisha JAMHURI. Lakini kosa moja unalofanya ni kuamini kuwa nchi hii vijana hawawezi kufanya mambo ya kimaendeleo bila kujihusisha au kuhusishwa na vimelea vya matajiri na wanasiasa. Tulibuni wazo la kuanzisha JAMHURI kwa sababu tuliamini kuwa wakati umefika wa kujiajiri na kupanua wigo wa ajira pia. Watu wote wangekuwa na akili za kubaki pale pale, leo tusingekuwa na kina Mengi, Nimrod Mkono, Bakhresa na wengi walioajiri. Ombi langu moja kwako mleta mada na wengine wenye mawazo kama yako, msiendelee kuamini kuwa kuajiriwa tu ndiyo suluhu ya kukabiliana na maisha. Ondoeni fikra potofu kwa kujaribu kujiajiri. Inawezekana kabisa. Leo, asilimia 80 ya vijana wa Tanzania wanawaza kuajiriwa serikalini na katika taasisi zake nono. Asilimia 20 tu ndio wanaowaza kuthubutu kujiajiri. kenya ni kinyume, ndiyo maana unaona wanasonga mbele. Vijana wa Tanzania amkeni. Msidhani kila anayethubutu kabebwa na tajiri au mwanasiasa. Wakati ninyi mkikomalia kuomba michango ya harusi, wenzenu tuliomba fedha za kusajili na kuchapisha gazeti kutoka kwa watu wa kawaida kabisa. Tumethubutu, na tumeweza. Wake Up!
 
Heshima kwenu,

Nduui wanaJF nimeona nishirikishe habari hii. Mwandishi wa habari na mhariri, ambaye pia katibu wa Jukwaa la Wahariri, Nd. Neville Meena yuko hospitali ya Muhimbili, amelazwa.

Meena alianza kuugua akiwa Tanga karibu wiki mbili zilizopita. Anasumbuliwa sana na maumivu ya kichwa. Alihamishiwa Muhimbili kwa usafiri wa anga. Wenye mapenzi mema wamwombee na kwenda kumjulia hali ila wasiwe miongoni mwa 'wasiojulikana".Siwaamini hawa watu hata kidogo.
Huyu ni mmoja wa ma comredi wa ukweli kwenye tasnia ya habari.

Get Well Soon!.
P
 
Back
Top Bottom