NeuraLink: Kampuni iliyoanzishwa na Elon Musk yenye mipango ya kudukua Ubongo wa Mwanadamu

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
May 27, 2016
5,416
7,828
NeuraLink: Kampuni iliyoanzishwa na Elon Musk yenye mipango ya kudukua Ubongo wa Mwanadamu

1565009022085.png

Lengo la kampuni hiyo ni kutafuta mbinu za kuchochea ubongo wa mwanadamu aliyepooza kuwawezesha kudhibiti tarakilishi (Computer).

NeuraLink, kampuni ilioanzishwa na Elon Musk ili kutafuta mbinu za kuunganisha ubongo wa mwanadamu na tarakilishi imewasilisha ombi kwa wadhibiti wa Marekani kuanza kupima kifaa chake miongoni mwa wanadamu.

Mfumo huo umejaribiwa katika tumbili ambaye aliweza kudhibiti tarakilishi na ubongo wake kulingana na bwana Musk.

Kampuni hiyo ilikuwa inalenga kuwaangazia wagonjwa wenye matatizo ya uti wa mgongo, neva na ubongo miongoni mwa binadamu. Lakini hata hivyo lengo la bwana Musk ni kudukua ubongo wa mwanadamu kupitia tarakilishi.

Kifaa ambacho kampuni hiyo imekitengeneza kina kifaa kidogo kinachoweza kuchunguza chenye electrodes zaidi ya 3,000 zilizounganishwa na nyuzi zinazoweza kubadilika ambazo ni nyembamba kuliko nywele za binadamu na ambazo pia zinaweza kufuatilia shughuli za neuroni 1,000.

1565010215339.png

Elon Musk.

Umuhimu wa mfumo huo, kulingana na kampuni hiyo ni kulenga maeneo fulani katika ubongo hatua inayofanya upasuaji kuwa salama. Pia kinaweza kutathmini yaliorekodiwa kupitia mashine ambayo itaamua ni aina gani ya matibabu atakayopewa mgonjwa.

Neuralink hata hivyo haikutoa maelezo jinsi mfumo huo unavyoweza kubadilisha vitendo vya ubongo ama jinsi kifaa hicho kilivyoweza kuchochea seli za ubongo.

''Si kwamba tayari tutakuwa tuna uwezo wa kushirikisha ubongo wa mwanadamu katika tarakilishi na kudhibiti bongo za wanadamu'', alisema bwana Musk.

1565010090299.png

Picha (kushoto): Elon Musk.

Hiki ni kitu kitakachochukua muda mrefu. Lakini alisema kwamba wale watakaotaka kutumia mfumo huo utasaidiana na ule wa tarakilishi. Awali, Musk alisema kuwa intelijensia ya mashine inaweza kuharibu jamii ya wanadamu.

Uunganishaji wa ubongo na tarakilishi utaimarisha zaidi ubongo wa mwanadamu, alisema akiongezea kwamba tayari watu wamekuwa wakifurahia hilo kupitia simu zao.

Baadaye baada ya muda wa maswali na majibu, alifichua kwamba kifaa hicho cha Neuralink kinafanya kazi na kwamba tayari kimefanyiwa vipimo katika tumbili huku mnyama huyo akiweza kudhibiti tarakilishi na ubongo wake.

Sasa kampuni hiyo imewasilisha ombi la kutaka kuwajaribu wanadamu na mfumo huo ombi ambalo litahitajika kuidhinishwa na kitengo cha usimamizi wa chakula na dawa nchini Marekani.

Bwana Musk pia analenga kuajiri mwanasayansi mmoja zaidi katika kampuni hiyo ambayo kufikia sasa inaendeshwa na wafanyakazi wapatao 100.

1565010388082.png

Kifaa kilichopendekezwa kinachokaa nje ya kichwa chenye uwezo wa kuusoma ubongo wa mwanadamu.

Mpango wa kudukua ubongo wa mwanadamu kampuni hiyo inasema utachukua miaka mingi ya kazi kufanywa ili kukabiliana na changamoto za kiteknolojia pamoja na kimaadili, lakini teknolojia hiyo huenda ikawa hatua kubwa katika kukabiliana na matatizo sugu ya kiafya kama vile ugonjwa wa kifafa na ule wa kutetemeka.

Miradi mingi ya bwana Musk inajaribu kufanya yale yasiyowezekana.

Mradi wa Space X unalenga kuanzisha utalii wa kuelekea sayari ya Mars huku kampuni ya Boring ikijaribu kujenga mahandaki chini ya mji wa Los Angeles huku mradi wake wa Hyperloop ukilenga kuimarisha usafiri kwa njia nyingine.

Makala: BBC
Picha: Getty Images na vyanzo vingine
 
Na sisi tujivunie mwanasayansi wetu mzanzibari Aliyekuwa Makamu wetu wa Raisi mbeba Mikasi kwa kuzindua.. mtaalam wa Nuclear power
 
NeuraLink: Kampuni iliyoanzishwa na Elon Musk yenye mipango ya kudukua Ubongo wa Mwanadamu

View attachment 1172991
Lengo la kampuni hiyo ni kutafuta mbinu za kuchochea ubongo wa mwanadamu aliyepooza kuwawezesha kudhibiti tarakilishi (Computer).

NeuraLink, kampuni ilioanzishwa na Elon Musk ili kutafuta mbinu za kuunganisha ubongo wa mwanadamu na tarakilishi imewasilisha ombi kwa wadhibiti wa Marekani kuanza kupima kifaa chake miongoni mwa wanadamu.

Mfumo huo umejaribiwa katika tumbili ambaye aliweza kudhibiti tarakilishi na ubongo wake kulingana na bwana Musk.

Kampuni hiyo ilikuwa inalenga kuwaangazia wagonjwa wenye matatizo ya uti wa mgongo, neva na ubongo miongoni mwa binadamu.

Lakini hatahivyo lengo la bwana Musk ni kudukua ubongo wa mwanadamu kupitia tarakilishi.

Kifaa ambacho kampuni hiyo imekitengeneza kina kifaa kidogo kinachoweza kuchunguza chenye electrodes zaidi ya 3,000 zilizounganishwa na nyuzi zinazoweza kubadilika ambazo ni nyembamba kuliko nywele za binadamu na ambazo pia zinaweza kufuatilia shughuli za neuroni 1,000.

View attachment 1173001
Elon Musk.

Umuhimu wa mfumo huo, kulingana na kampuni hiyo ni kulenga maeneo fulani katika ubongo hatua inayofanya upasuaji kuwa salama.

Pia kinaweza kutathmini yaliorekodiwa kupitia mashine ambayo itaamua ni aina gani ya matibabu yatakayopewa mgonjwa.

Neuralink hata hivyo haikutoa maelezo jinsi mfumo huo unavyoweza kubadilisha vitendo vya ubongo ama jinsi kifaa hicho kilivyoweza kuchochea seli za ubongo.

''Sio kwamba tayari tutakuwa tuna uwezo wa kushirikisha ubongo wa mwanadamu katika tarakilishi na kudhibiti za bongo za wanadamu'', alisema bwana Musk.

View attachment 1173000
Picha (kushoto): Elon Musk.

Hiki ni kitu kitakachochukua muda mrefu. Lakini alisema kwamba wale watakaotaka kutumia mfumo huo utasaidiana na ule wa tarakilishi.

Awali Bwana Musk alikuwa amesema kuwa intelijensia ya mashine inaweza kuharibu jamii ya wanadamu.

Uunganishaji wa ubongo na tarakilishi utaimarisha zaidi ubongo wa mwanadamu , alisema akiongezea kwamba tayari watu wamekuwa wakifurahia hilo kupitia simu zao.

Baadaye baada ya muda wa maswali na majibu , alifichua kwamba kifaa hicho cha Neuralink kinafanya kazi na kwamba tayari kimefanyiwa vipimo katika tumbili huku mnyama huyo akiweza kudhibiti tarakilishi na ubongo wake, Kulingana na bwana Musk.

Sasa kampuni hiyo imewasilisha ombi la kutaka kuwajaribu wanadamu na mfumo huo ombi ambalo litahitajika kuidhinishwa na kitengo cha usimamizi wa chakula na dawa nchini Marekani.

Bwana Musk pia analenga kuajri mwanasayansi mmoja zaidi katika kampuni hiyo ambayo kufikia sasa inaendeshwa na wafanyikazi 100.

View attachment 1173002
Kifaa kilichopendekezwa kinachokaa nje ya kichwa chenye uwezo wa kuusoma ubongo wa mwanadamu.

Mpango wa kudukua ubongo wa mwanadamu kampuni hiyo inasema utachukua miaka mingi ya kazi kufanywa ili kukabiliana na changamoto za kiteknolojia pamoja na kimaadili, lakini teknolojia hiyo huenda ikawa hatua kubwa katika kukabiliana na matatizo sugu ya kiafya kama vile ugonjwa wa kifafa na ule wa kutetemeka.

Miradi mingi ya bwana Musk inajaribu kufanya yale yasiyowezekana.

Mradi wa Space X unalenga kuanzisha utalii wa kuelekea sayari ya Mars huku kampuni ya Boring ikijaribu kujenga mahandaki chini ya mji wa Los Angeles huku mradi wake wa Hyperloop ukilenga kuimarisha usafiri kwa njia nyengine.

Makala: BBC
Picha: Getty Images na Vyanzo vinginevyo

Mkuu hii thread ilitakiwa uiweke JI....ungekuwa umeitendea haki.
 
Back
Top Bottom