Netanyahu wa Israel kufungwa. Trump anaweza kupoteza urais wake. Magufuli anafanya analotaka haulizwi chochote

field marshall1

JF-Expert Member
Sep 17, 2017
1,171
2,730
Kuna taarifa leo kuwa Binyamin Netanyahu au Bibi ameshtakiwa na mwendesha mashtaka (DPP) pamoja na Mwanasheria Mkuu (Attorney General) wa serikali ya Israel kwa kosa la rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.

Kwa vyovyote vile hataweza kushinda, kama ilivyotokea kwa Ehud Olmert aliyekuwa mtangulizi wake ambaye pia alishtakiwa kwa rushwa na kuripoti kuuza nyumba kwa bei ya chini jijini Jerusalem. Olmert alifungwa kifungo cha mwaka mmoja.

Marekani, Donald Trump naye amekalia kuti kavu huenda likakatika wakati wowote, kosa lake ni kutumia madaraka yake vibaya na kutumia mbinu ovu ili kushinda uchaguzi mkuu kwa kuwahusisha Russia (Bado ya Ukraine, Rushwa nk).

Akipatikana na kosa ataondolewa na huenda akafungwa kulingana na katiba ya Marekani.

Hiyo ni mifano miwili tu ya mambo yanayoendelea wiki hii, Katika dunia iliyostaarabika hayo mambo ni ya kawaida.

Ukiiba unafungwa, ukitumia vibaya rasilimali za nchi unafungwa au unatolewa na bunge/congress/senate etc. Mifano ni mingi mno.

Kwa wizi na matumizi mabovu anayojifanyia bila vibali vya bunge huyo Magufuli angekuwa indicted tayari kama ingekuwa nchi zilizostaarabika.

Tangu alivyouza nyumba za serikali na kuwagawia nduguze na rafiki zake hadi anavyojipendelea kujijengea kiwanja cha kimataifa cha ndege kijijini kwake, kuwaonea wanaompinga, kumpendelea Makonda asiye kuwa na vyeti na kugawagawa fedha ovyo.

Tungekuwa nchi ya demokrasia huyo Magufuli angeshakuwa nje ya taasisi ya uraisi pengine angekuwa anatumikia kifungo gerezani, lakini kwa kuwa nchi yetu ni hovyo hovyo(Kinachotufanya Africa tudharaulike).

Ameshakuwa kama Mungu kwa jinsi anavyosifiwa na kutukuzwa kiasi kwamba tunaambiwa na viongozi waliovimbiwa kuwa Mungu amshukuru Magufuli.

WHAT A SHAME?
 
Mkuu kumbe hata kosa la tariff man Trump ambalo genge la wahuni wa democrats wanamtuhumu nalo hujui, sio mambo ya russia, ni mambo ya ukraine.. yale ya russia alishinda na hili anashinda. Hakuna namna trump atashindwa na mwakani anashinda tena uchaguzi.
 
Unaandika mambo yaliyokuzidi umri ndugu yangu Marekani wamepitia mengi na kama unajua huyo ni Raisi wa ngapi na nikukumbushe tu walichofanyiwa Black American,
Nayajua yote kuliko unavyofahamu wewe. Anaweza akashinda lakini anaenda kuwa impeached.
 
Mkuu kumbe hata kosa la tariff man Trump ambalo genge la wahuni wa democrats wanamtuhumu nalo hujui, sio mambo ya russia, ni mambo ya ukraine.. yale ya russia alishinda na hili anashinda. Hakuna namna trump atashindwa na mwakani anashinda tena uchaguzi.
Huyu jamaa ni wa kupuuzwa tu, hajui aliongealo
 
Nimegundua una chuki na Rais wala huna chochote

Unaongelea kuuza nyumba za serikali ukimtuhumu magufuli aliyekuwa waziri lakin umeshindwa kumtaja kilaza mwenziyo sumayi aliyekuwa waziri mkuu

Shwain
 
Kuna taarifa leo kuwa Binyamin Netanyahu au Bibi ameshtakiwa na mwendesha mashtaka (DPP) pamoja na Mwanasheria Mkuu (Attorney General) wa serikali ya Israel kwa kosa la rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.

Kwa vyovyote vile hataweza kushinda, kama ilivyotokea kwa Ehud Olmert aliyekuwa mtangulizi wake ambaye pia alishtakiwa kwa rushwa na kuripoti kuuza nyumba kwa bei ya chini jijini Jerusalem. Olmert alifungwa kifungo cha mwaka mmoja.

Marekani, Donald Trump naye amekalia kuti kavu huenda likakatika wakati wowote, kosa lake ni kutumia madaraka yake vibaya na kutumia mbinu ovu ili kushinda uchaguzi mkuu kwa kuwahusisha Russia (Bado ya Ukraine, Rushwa nk).

Akipatikana na kosa ataondolewa na huenda akafungwa kulingana na katiba ya Marekani.

Hiyo ni mifano miwili tu ya mambo yanayoendelea wiki hii, Katika dunia iliyostaarabika hayo mambo ni ya kawaida.

Ukiiba unafungwa, ukitumia vibaya rasilimali za nchi unafungwa au unatolewa na bunge/congress/senate etc. Mifano ni mingi mno.

Kwa wizi na matumizi mabovu anayojifanyia bila vibali vya bunge huyo Magufuli angekuwa indicted tayari kama ingekuwa nchi zilizostaarabika.

Tangu alivyouza nyumba za serikali na kuwagawia nduguze na rafiki zake hadi anavyojipendelea kujijengea kiwanja cha kimataifa cha ndege kijijini kwake, kuwaonea wanaompinga, kumpendelea Makonda asiye kuwa na vyeti na kugawagawa fedha ovyo.

Tungekuwa nchi ya demokrasia huyo Magufuli angeshakuwa nje ya taasisi ya uraisi pengine angekuwa anatumikia kifungo gerezani, lakini kwa kuwa nchi yetu ni hovyo hovyo(Kinachotufanya Africa tudharaulike).

Ameshakuwa kama Mungu kwa jinsi anavyosifiwa na kutukuzwa kiasi kwamba tunaambiwa na viongozi waliovimbiwa kuwa Mungu amshukuru Magufuli.

WHAT A SHAME?
Hii Impeachment inquiry unaifuatilia vizuri kweli?,Au unaongea tu with no facts...
 
Mkuu kumbe hata kosa la tariff man Trump ambalo genge la wahuni wa democrats wanamtuhumu nalo hujui, sio mambo ya russia, ni mambo ya ukraine.. yale ya russia alishinda na hili anashinda. Hakuna namna trump atashindwa na mwakani anashinda tena uchaguzi.
Mueller hakumsafisha Trump, kuna uwezekano mwakani Democrats wakachukua Senate na Congress (House) hivyo hata Trump akishinda hiyo kitu italetwa mezani. Trump inawezekana asishinde tena mwakani.
 
Hii Impeachment inquiry unaifuatilia vizuri kweli?,Au unaongea tu with no facts...
Kwa hiyo unamtetea Magufuli kuwa afanye tu analotaka maana sijajua kwanini una-mind mfano wa Trump. Lakini angalau umeona wanam-impeach rais......Kwetu Magufuli hata akiua kijiji kizima hatafanywa kitu. INABIDI UJIFUNZE KUTENDA HAKI.
 
Back
Top Bottom