Netanyahu: Jerusalem umekuwa mji mkuu wa Israel kwa miaka 3000

nankumene

JF-Expert Member
Nov 12, 2015
6,003
2,000

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa wapalestina ni lazima wakubali kuwa Jurusalem ndio mji mkuu wa Israel ili amani iweze kupatikana.

Netanyahu alisema Jerusalem umekuwa mji mkuu wa Israel kwa miaka 3,000 na haujakuwa mji mku wa watu wengine.

Aliongea huku maandamano yakiendelea kwenye ulimwengu wa kiislamu kufuatia hatua ya Marekani kuutambua Jurusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Ghasia zilizuka karibu na ubalozi wa Marekani nchini Lebanon na kwingineno siku ya Jumapili.

Jerusalem kwenyewe, mpalestina mmoja alikamatwa kwa kumdunga kisu na kumjeruhiwa vibaya afisa wa usalama wa Israel karibu na kituo kimoja cha basi.

Akiongea mjini Paris baada ya mazungumzo na rais wa Ufaransa Emmauel Macron, Bw Netanyahu alisema kuwa jitihada za kuwanyima wayahudi mji wa wa Jerusalem ni kitu kibaya.

"Unaweza kusoma katika kitabu kizuri zaidi, kinaitwa Biblia, alisema. Unaweza kuyaskia katika historia ya jamii wa wayahudi kote duniani… Ni wapi tena kuna mji wa Israel, isipokuwa Jerusalem?

Netanyahu: Jerusalem umekuwa mji mkuu wa Israel kwa miaka 3000
 

nankumene

JF-Expert Member
Nov 12, 2015
6,003
2,000
Netanyahu anakwambia kuna kitabu kimoja kizuri kinaitwa biblia, anakwambia kwny kitabu hicho hakuna ht sehemu moja ambako jersalemu imetajwa kuwapio sehemu nyingine tofauti na israeli..........vita imehamia kwe maandiko
 

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
15,687
2,000
  • Thanks
Reactions: BAK

laki si pesa.

JF-Expert Member
Jul 14, 2015
10,017
2,000
Mkuu hawa jamaa wayahudi wanafuata biblia kama ndo katiba yao! so usishangae.
huu mji watautaifisha tu wakishirikiana na mmarekani si unaona wanavyo enda kwa pasi trump to Netanyahu!,kumbuka wamerekani waliwasaidia waisrael kurejea hapo baada ya kile kipigo kikali toka kwa hitler.
Netanyahu ni tapeli, mnafiki mkubwa....Netanyahu ni myahudi na wayahudi hawaitambui biblia....anasema hivyo kutafuta huruma ya wakristo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom