Netanyahu: Israeli inataka uhusiano na Afrika

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,314
33,108
160704113238_israeli_pm_lands_in_uganda_624x351_bbc_nocredit.jpg

Ndege ya waziri Netanyahu

Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ametua nchini Uganda katika ziara ya kwanza kabisa kwa kiongozi wa taifa hilo la kiyahudi kuzuru Afrika tangu mwaka wa 1987.

160704113557_israeli_pm_lands_in_uganda-_dignitaries_624x351_umc.jpg
Netanyahu anakutana na viongozi wa mataifa 6 ya Afrika
Ziara hiyo ya siku 5 imeanzia Uganda, na kisha waziri Netanyahu anatarajiwa kuzuru Kenya, Rwanda na kisha Ethiopia.

160704113359_israeli_pm_lands_in_uganda-_red_carpet_624x351_umc.jpg

Usalama uliimarishwa
Ilikuwa kihoja kwa wageni waalikwa kuingia kwenye uwanja huo wa ndege kwani usalama uliimarishwa huku maafisa wa usalama wa Israeli wakishika doria na mbwa na walenga shabaha, mbali na upekuzi wa kawaida wa maafisa wa usalama wa Uganda.

Bw Netanyahu ameandamana na mkewe Sarah na ujumbe wa wafanyibiashara wa sekta mbalimbali za uchumi wa Israeli.

160704114242_israeli_pm_lands_in_uganda-_entebbe_song_624x351_umc.jpg
Netanyahu alipata fursa ya kuhudhuria misa ya ukumbusho wa kakake Yoni mmoja wa makomando wa Irsaeli waliokufa katika shambulizi hilo.
Alipotua katika uwanja huo wa ndege wa Entebbe eneo kulikotokea operesheni ya kipekee miaka 40 iliyopita, ya kuwanusuru mateka wayahudi waliokuwa wametekwa na wanamgambo wa kipalestina, Netanyahu alipata fursa ya kuhudhuria misa ya ukumbusho wa kakake Yoni mmoja wa makomando wa Irsaeli waliokufa katika shambulizi hilo.

160704114416_israeli_pm_lands_in_uganda-_mwenge_624x351_umc.jpg

Mwenge wa ukumbusho uliashwa
Ndege iliyokuwa imewabeba wayahudi hao ilikuwa imetoka Israeli ikielekea Ufaransa.

Kabla ya hapo alikagua gwaride la heshima lililoandamana na makombora 19 kwa heshma yake.

Waziri Netanyahu anasema kuwa ziara hii inalenga kuimarisha uhusiano wa taifa hilo la kiyahudi na mataifa ya Afrika ambayo Israeli inatumai kuwavutia iliwasiwaunge mkono wanaharakati wa Palestina.

160704113457_israeli_pm_lands_in_uganda-_commemoration_624x351_umc.jpg

Baadhi ya mateka wa Entebbe walihudhuria ukumbusho huu
Mwenyeji wake rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amewakaribisha marais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Paul Kagame wa Rwanda Salva Kiir Mayardit, wa Jamuhuri changa zaidi duniani ya Sudan Kusini Edgar Lungu wa Zambia, rais wa Malawi waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn, na waziri wa maswala ya Kigeni wa Tanzania Augustine Mahiga katika kikao cha faragha kinachotarajiwa kujadili maswala ya ugaidi na Usalama wa taifa ambayo Israeli imeahidi kuyasaidia kukabiliana nayo.

160704113701_israeli_pm_lands_in_uganda-_herculean_624x351_umc.jpg

Ndege aina ya Herculean iliyotumika katika operesheni hiyo
Mwandishi wetu aliyeko Kampala anasema kuwa makomando wa Israeli wameshika doria kote mjini Kampala atakozuru Waziri Netanyahu.

Israeli haijakuwa na uhusiano mwema na mataifa ya Afrika ambayo yaliiona kuwa saliti kwa kushirikiana na serikali dhalimu ya Afrika Kusini iliyokuwa ikiwatesa waafrika weusi.

160704113855_israeli_pm_lands_in_uganda-_entebbe_624x351_umc.jpg

Eneo la mawasiliano lililoharibiwa katika makabiliano hayo ya Entebbe raid
Aidha mataifa ya Afrika yaliunga mkono jitihada za Uhuru wa wapalestina ambao wanakaliwa kimabavu na Isreali na hivyo kutenga taifa hilo la Kiyahudi haswa katika miaka ya 60 na 70 harakati za PLO ziliposhika kasi.

Ziara hii inatarajiwa kupunguza tofauti hizo na kuwapa chambo mataifa ya Afrika iliwalegeze misimamo mikali dhidi ya Israeli. chanzo.

Chanzo: BBC Swahili
 
Shujaa Netanyahu, Tunataka viongozi wenye "IQ KUBWA" kama "Netanyahu score 168 at MIT". U'r warmly welcomed.
 
Karibu Afrika Benjamin,ni bahati mbaya ziara yako hautofika Dar.
 
Mtoa mada pale ulipoandika wanamgambo umebadirisha ilikuwa inasomeka MAGAIDI naona wewe umerembesha sana hapo,Maana hao walioteka ndege hiyo walikuwa MAGAIDI na wala si WANAMGAMBO.
 
Waafrika ni wazuri sana kutumika,alikuja mwaarabu wakasilimu vita za waarabu hadi waafrika inawahusu sasa,kaja mzungu wakawa wakristo vita zawazungu sasa wakashiriki,sasa mwiisraeli kaanzisha ulokole kila mlokole abeba bendera ya israeli,utumwa uliiaza kifikira kisha kivitendo ya kitendo ilikwisha ya kifikira imebaki afrika.
 
Back
Top Bottom