Netanyahu anaangalia uwezekano wa msaada wa kijeshi wa Israel kwa Ukraine

Messenger RNA

JF-Expert Member
Jul 24, 2022
1,102
3,022
Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amesema Jumatano kwamba serikali yake haijaondoa uwezekano msaada wa kijeshi kwa Ukraine.

Awali, Israeli ilisisitiza kuwa itatoa msaada wa kibinadamu pekee, ambao nchi hiyo imekuwa ikiutoa kwa Ukraine tangu mwanzoni mwa vita.

Kulingana na Netanyahu, Israel hata iko tayari kuangalia uwezekano wa kupeleka mfumo wa hivi karibuni wa ulinzi wa anga, Iron Dome air defense, kulilinda anga la Ukraine, ingawa awali Israeli ilisistiza kuwa mfumo huu haukulengwa kutumiwa kwa matumizi ya aina hiyo katika maeneo kama Ukraine.

Netanyahu hakutoa ahadi za kipekee, lakini pia alisema kwamba yuko tayari kuwa mpatanishi katika mzozo iwapo pande zinazohasimiana na Umoja wa Mataifa watakubali kufanya hivyo.

Kulingana na Bw Netanyahu, alikuwa amepewa pendekezo la aina hiyo mwanzoni mwa vita, lakini wakati huo alikuwa ni kiongozi wa upinzani na hakuchukua jukumu la upatanishi.
 
Hiyo ni baada waziri wa mambo ya nje wa marekani kutembelea israel juzi . Leo anaibuka netayahu nakusema yuko tayari kuwa mpatañish kati ya russia na ukrein. Hapo kamchezo gani kanaendelea.,?
KARIBUNI.
 
Back
Top Bottom