Net za Kikwete

kansije

Member
Sep 16, 2010
50
10
sijui niziite neti za mbu au nyavu za kuvulia samaki, yaani mbu wanapita kama kawaida inasikitisha sana, hapa tumeliwa
 
sijui niziite neti za mbu au nyavu za kuvulia samaki, yaani mbu wanapita kama kawaida inasikitisha sana, hapa tumeliwa

Tumeliiwa vipi mkuu mbona kikwete alisamamia production mwenyewe kule new york?
 
Tumeliiwa vipi mkuu mbona kikwete alisamamia production mwenyewe kule new york?

Jana nimejifunika hiyo neti nimeamka usiku mrefu mkuu nakuta kuna mbuu kama mia na wengine nawashuhudia wanavyopita, so tumeliwa
 
net zina matundu makubwa.chonde chonde,mwanao kamnunulie chandarua kizuri.hapa tunadanganyana.chandarua chenyewe kwenye 5 kwa 6 hakikai.ni vidogo halafu mbu wanapita kama wananawa.kwa ukubwa ni vya kufunika watoto mabwenini shuleni tatizo matundu makubwa.tumeliwa.ndo maana wale jamaa wanavulia samaki na kufunikia mboga mboga zisiliwe na wadudu.mia
 
mwanzo nilidhani nakosea kuchomekea yaani naacha sehemu wazi...juzi nikahakikisha nimekagua sehemu zote ziko sawa na hakuna mbu nilioingia nao nikalala...kuamka utafikiri nililala nje ya net!.
Hizi net zina matundu makubwa na zinapitisha mbu na kama kweli zimewekewa dawa inayodumu kwa miaka 5 kama tunavyoambiwa, basi hiyo dawa ni fake.
Na kama kweli serikali ina nia ya dhati ya kutokomeza malaria ingewahamasisha wananchi kuua mbu na mazalia yao na kila kitu kinachohusu maisha ya mbu. Mbu kama ilivyo kwa wadudu wengi anaweza kuuawa kwa mafuta taa tu kerosene/paraffin. Serikali ingehakikisha bomba za ku-spray zinapatikana madukani na kwa wingi.
Lakini kwa utaratibu huu wa sasa ambapo mbu anaachwa huru ktk hatua zake zote za maisha kisha tutegemee hizi net kuangamiza malaria ni kazi bure. kabisa.
 
sijui niziite neti za mbu au nyavu za kuvulia samaki, yaani mbu wanapita kama kawaida inasikitisha sana, hapa tumeliwa
Ukisema tumeliwa unanitia uchungu sana, kwani hizo net zilifanya nikagawa kura yangu kwa ccm mwaka jana. Sasa unapozibeza unaniumiza moyoni.
 
Hzo net nlilalia cku moja,nlvoamka asubuh,nikaichoma moto..maana nlikuta mbu ka elfu tisa hvi.
 
Mimi nilizisitukia siku niliyopewa, hivi sasa nimeweka kwenye kakitalu kangu ka mchicha kuzuia kuku....
 
Jamani hizo net ziliingizwa kisiasa zaidi,Achana na kuwa na matundu makubwa,vilevile dawa wanayodai kuiwekea usalama kwa watumiaji upoje? Soma maelezo yake kwenye yake,nanukuu ukifua usimwage maji uliyofulia kwenye mito /visima ya maji na mimea, kwa maelezo hayo wameprotect mimea na wadudu,! Mwenzangu na mimi afya yako itakuwa salama kwasiku 366 na mbaya zaidi nyumba zenyewa madirisha yake kama vishimo vya panya,na wenye madisha makubwa kufungua dirisha labda mara 1 kwa mwaka ni hatari sana! Tatizo letu tupo makini na madhara ya nayoweza kujitokeza muda huo huo ya baadaye we never mind! Nawasilisha
 
Jk atalaaniwa kwa mambo aliyoyafanya kwa maslahi binafsi huku akipumbaza watanzania anayafanya kwa nia njema ya kuwakomboa watanzania.Hili swala lilishawahi kuengelewa kuwa huu ni mradi wa wakubwa .Sasa hii ni aibu kwa uongozi wake ,siku zote si mtu makini ndio maana hata watendaji wake wanalipua mambo.
 
Ukisema tumeliwa unanitia uchungu sana, kwani hizo net zilifanya nikagawa kura yangu kwa ccm mwaka jana. Sasa unapozibeza unaniumiza moyoni.

Ni bora tungeletewa suti pea mbili mbili inapofika usiku unajivalia suti zako mbu haoni ndani. Tatizo kwa wasiokuwa na AC hasa kwa Dar.
 
zile sio net matundu yake ka madirisha nawashauri msizitumie................nia ya wmarekani kuendelea kutupunguza,THERE IS NO LUNCH FOR FREE
 
chomekeni net vizuri acheni kulalamika. unapoingia kulala hakikisha hauingii na mbu pia weka net vizuri ili isijechomoka usiku bila wewe kujua, unapolala usigusane na neti. maleria haikubaliki.
 
chomekeni net vizuri acheni kulalamika. unapoingia kulala hakikisha hauingii na mbu pia weka net vizuri ili isijechomoka usiku bila wewe kujua, unapolala usigusane na neti. maleria haikubaliki.
watu wanapolalamika hivi ina maana hayo yote wamezingatia. Siamini kama watu hawajui kutumia net vizuri eti ndio maana mbu wanapita. We ukitaka kuthibitisha chukua kipande cha net fanya kama unaziba kwenye dirisha lisilo na wavu wa mbu yaani net ndio iwe kama wavu wa mbu. Kisha kaa hapo dirishani asubuhi au jioni muda wa mbu kutoka au kuingia chumbani utaona mbu wanavyopenya.<br />
Baada ya kuridhika na utafiti wangu nikaamua kutumia net yangu ya zamani yenye matundu madogo, na hakuna mbu ndani ya net niamkapo asubuhi.
 
chomekeni net vizuri acheni kulalamika. unapoingia kulala hakikisha hauingii na mbu pia weka net vizuri ili isijechomoka usiku bila wewe kujua, unapolala usigusane na neti. maleria haikubaliki.
Hizo net unazifahamu au unazisikia tu??
 
Back
Top Bottom