Nepotism: Jeshi la Polisi na upendeleo kwa wana CCM huku likinyanyasa wapinzani. Hivi Sirro hamuoni Gwajima?

kagoshima

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,117
2,000
Hii inchi ina mambo ya kipumbavu sana na ndio maana haisongi mbele maana hata taratibu tulizojiwekea wenyewe zinatekelezwa kibaguzi.

Pata picha ingekuwa wapinzani ndio wanaopinga kifanywacho na serikali kuhusu chanjo na kutoa kashfa kejeli kwa serikali kama afanyavyo Gwajima. Wangekuwa Rumande siku nyingi na majeraha ya vipigo.

Mbowe yuko mahabusu kwa mashitaka ya kubambikia, kuna wapinzani wako mahabusu kwa kubeba mabango ya kupinga uonevu.

Kuna wapinzani wamekamatwa na kuwekwa mahabusu kwa kosa la kumuombea Mbowe.

Kuna wapinzani wako mahabusu kwa kufanya vikao vya ndani vya chama.

Wakati huohuo mchungaji Gwajima anaikashifu serikali na viongozi wake hakuna anayekohoa. Sio Sirro, wala askari yeyote. Sio Rais aliyeibuka kuongelea kesi Mbowe, si yeyote hata huko chamani wote wameufyata.
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
9,658
2,000
Aisee mbona mnamlalamikia tu huyo Gwajima! Wekeni na clip ya kusindikizia haya malalamiko basi.

By the way, Gwajima ni CCM! Kulindana na kubebana, ni jambo la kawaida.
 
Vessel

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
5,575
2,000
Gwajiboy hawezi guswa kwani alishatangaza akidanja wanakijani atamfufua,ndio maana anawaambia wakatae hata chanjo. 😆
 
Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
43,529
2,000
Anachofanya Gwajima ni Sabotage kubwa sana sana na haipaswi kuvumiliwa, badala ya kukemewa eti Bunge limetoa Barua ya kukanusha! I thought wangekuwa wakali ndio kwanzaaaa wanampetipeti.

Gwajima amewakalia pabaya
 
ujoka

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
2,504
2,000
Simuungi mkono Gwajima ila pia kosa lake silioni as far as freedom of speech and freedom of expression is concerned rashidi ana hoja na hoja hupingwa kwa hoja wakumjibu ni waziri wa afya na si IGP
 
Gangaboe

Member
Jun 26, 2021
13
45
Kifanywacho na mamlaka kumhusu gwajima ndicho kilitakuwa kifanyike kwa raia wote ,maana kwa mjibu ya katiba yetu,wanao Uhuru wa kutoa maoni,kutafuta habari na kutoa maoni.Na kama selikali iliyoko ni selikali yavwatu iliyowekwa na watu,basi hoja siyo kupigwa wala kuswekwa rumande,hao wenye maswali na hoja zao basi wajibiwe na hoja bora zaidi ili kukata kiu ya hofu na wasiwasi walionao.
 
Vessel

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
5,575
2,000
Huyo ananguvu ya sgang,hata kwa akina chiro wemekitamo mizizi Bila shaka ukimya huo sii wabure ni katika kutekeleza agenda zao.
 
Vessel

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
5,575
2,000
Simuungi mkono gwajima ila pia kosa lake silioni as far as freedom of speech and freedom of expression is concerned rashidi ana hoja na hoja hupingwa kwa hoja wakumjibu ni waziri wa afya na si IGP
Freedom gani yenye double standard za kubambikia hata ugaidi wanao itumia hiyo freedom. Almuradi ni mpinzani ila mwanakijani ruksa kufanya lolote. Huo ni udhaifu tena wakimfumo, hata uliokuwa organized kwa manufaa ya makundi nufaika, au yenye kuyatazama malengo yao.
 
kigogo warioba

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
5,981
2,000
Simuungi mkono gwajima ila pia kosa lake silioni as far as freedom of speech and freedom of expression is concerned rashidi ana hoja na hoja hupingwa kwa hoja wakumjibu ni waziri wa afya na si IGP
hivi mpotoshaji kama huyu anaeanzia miguuni i mean kwa waumini
je ni nani wa kumjibu mtu wa madhabahu?
 
Vessel

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
5,575
2,000
Kifanywacho na mamlaka kumhusu gwajima ndicho kilitakuwa kifanyike kwa raia wote ,maana kwa mjibu ya katiba yetu,wanao Uhuru wa kutoa maoni,kutafuta habari na kutoa maoni.Na kama selikali iliyoko ni selikali yavwatu iliyowekwa na watu,basi hoja siyo kupigwa wala kuswekwa rumande,hao wenye maswali na hoja zao basi wajibiwe na hoja bora zaidi ili kukata kiu ya hofu na wasiwasi walionao.
Hawawezi na hawathubutu kufanya hivyo sababu wanazijua wenyewe.
 
kagoshima

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,117
2,000
Simuungi mkono gwajima ila pia kosa lake silioni as far as freedom of speech and freedom of expression is concerned rashidi ana hoja na hoja hupingwa kwa hoja wakumjibu ni waziri wa afya na si IGP
Ni kweli . lakini huoni upendeleo wa wazi .ingekuwa wapinzani wangeoneshwa cha mtema kuni chief
 
Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,474
2,000
Simuungi mkono gwajima ila pia kosa lake silioni as far as freedom of speech and freedom of expression is concerned rashidi ana hoja na hoja hupingwa kwa hoja wakumjibu ni waziri wa afya na si IGP
Kweli kabisa, hoja hupingwa kwa hoja, ila mtoa hoja wala mjibu hoja asiwe mpinzani, hasa asiwe CHADEMA !!
 
ujoka

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
2,504
2,000
Hapa hakuna mrengo wa kushoto wala wa kulia. ccm wanajua kwamba hawana chao, ndio maana wanajificha kwenye mbeleko ya polisi
Hii mbeleko ni mbaya sana maana watu wakichoka wanachokaga mazima
 
Gerald .M Magembe

JF-Expert Member
Jul 17, 2013
2,390
2,000
Hii inchi ina mambo ya kipumbavu sana na ndio maana haisongi mbele maana hata taratibu tulizojiwekea wenyewe zinatekelezwa kibaguzi.

Pata picha ingekuwa wapinzani ndio wanaopinga kifanywacho na serikali kuhusu chanjo na kutoa kashfa kejeli kwa serikali kama afanyavyo Gwajima. Wangekuwa Rumande siku nyingi na majeraha ya vipigo.

Mbowe yuko mahabusu kwa mashitaka ya kubambikia, kuna wapinzani wako mahabusu kwa kubeba mabango ya kupinga uonevu.

Kuna wapinzani wamekamatwa na kuwekwa mahabusu kwa kosa la kumuombea Mbowe.

Kuna wapinzani wako mahabusu kwa kufanya vikao vya ndani vya chama.

Wakati huohuo mchungaji Gwajima anaikashifu serikali na viongozi wake hakuna anayekohoa. Sio Sirro, wala askari yeyote. Sio Rais aliyeibuka kuongelea kesi Mbowe, si yeyote hata huko chamani wote wameufyata.
Mara tuu unapo amua kwenda upinzani tayari u 4jitayarisha kwa vyovyote. Jee ulitegea kuwa upinzani halafu CCM wakuone wao na wakuokote??
 
kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
7,986
2,000
Hii inchi ina mambo ya kipumbavu sana na ndio maana haisongi mbele maana hata taratibu tulizojiwekea wenyewe zinatekelezwa kibaguzi.

Pata picha ingekuwa wapinzani ndio wanaopinga kifanywacho na serikali kuhusu chanjo na kutoa kashfa kejeli kwa serikali kama afanyavyo Gwajima. Wangekuwa Rumande siku nyingi na majeraha ya vipigo.

Mbowe yuko mahabusu kwa mashitaka ya kubambikia, kuna wapinzani wako mahabusu kwa kubeba mabango ya kupinga uonevu.

Kuna wapinzani wamekamatwa na kuwekwa mahabusu kwa kosa la kumuombea Mbowe.

Kuna wapinzani wako mahabusu kwa kufanya vikao vya ndani vya chama.

Wakati huohuo mchungaji Gwajima anaikashifu serikali na viongozi wake hakuna anayekohoa. Sio Sirro, wala askari yeyote. Sio Rais aliyeibuka kuongelea kesi Mbowe, si yeyote hata huko chamani wote wameufyata.
Mbowe anatuhumiwa kwa ugaidi. Tatizo nyie upinzani mnaona kama mbowe ndio rais wenu wa nchi. Hili lilileta shida kisiwani enzi zile hamad anataka na yeye vimulimuli na pikipiki barabarani.
And then hua hakunaga polisi ccm na polisi chadema. Hakuna mahali ukiomba kazi serikalini unaulizwa chama chako. Uwe na chama huna chama ni mambo yako binafsi.
Chadema mumekua a cult kama vile freemason ndio kitu kinawapa tabu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom