Neno "Uzalendo" linatumika vibaya awamu hii, haijapata kutokea

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,502
2,046
Inavyoonekana neno uzalendo linatumika kuwakilisha matakwa binafsi zaidi na si kama lilivyokusudiwa katika matumizi yake.

Mf. Mtu kaibiwa analalamika hasikilizwi, anataka aandamane kuonyesha hisia zake, anawekwa ndani, anaenda kushtaki kwenye jumuiya za kimataifa juu ya uonevu aliofanyiwa, anaitwa ni msaliti wa nchi si mzalendo.

Je, kuna uhusiano kati ya uzalendo na ujinga au kupotezea haki zako za msingi?

Je, kuna uhusiano kati ya uzalendo na kukubaliana na kila wanachofanya walioko madarakani?
 
Achana nao, wamenyimwa akili ili wajifunze kuna madhara gani ukimminya mtu haki hadi kukosa pumzi kuna madhara gani.

Wenye akili wameshajua humu ndani hawasikilizwi sasa wameamua kwenda nje ya Tanzania kwa watu wanaowasikiliza.

Siku si nyingi hadi wasio na akili wataelewa nani ni mzalendo kweli.
 
Ukiitwa au kama unajihita Mzalendo basi ujue hauko sawasawa Upstair, uzalendo kwa leo ni Kukubaliana na Ubabe/Umafia otherwise Upigwe Kofi shavu la Kulia na ugeuze la kushoto kitu alichokikata TAL.
 
Yaan tunapokwenda vitu vingi vitabadilika Leo hata wizi inakuwa halali. Embu angalia wizi walioiba CCM na viongozi wa dini wapo kimya hamna hata anaongea.

Ukiikosoa serikali ya awamu hii kwa kusema kweli unaitwa msaliti
 
Back
Top Bottom